CCM yakiri Jey Key amekwama. Hapo patamu

karibia nihamie nchi jirani humu tz mwishowe nitanunua gun nianze kuondoa fisadi mmoja baada ya mwingine aghhh
 
karibia nihamie nchi jirani humu tz mwishowe nitanunua gun nianze kuondoa fisadi mmoja baada ya mwingine aghhh

Taratibu mkubwa, mods watakusweka rumande, mi ndiyo nimefunguliwa dakika chache tu zilizopita,tena sikuelezwa sababu.Maisha ya jela mabaya ndugu yangu.
 
Mi katika vitu nisivyopenda kusikia ni pamoja na eti washauri wa jk wanamshauri vibaya, aliyesema chukua akili zako changanya na za mbayuwayu, ni nani, hili halikubaliki, kumbe hata yeye anajua falsafa aliyoisema iweje leo eti wapambe wake wanamshauri vibaya kwa nn asiwe yeye mwenyewe hebu muwe makini, baba akishndwa kuihudumia familia huwezi sema ndugu na jamaa ndio wanaleta shida kwa familia kwa nn asiwe baba mwenyewe??
 
Hapa sijui CCM watasema huyu Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam kapotoka, watu wenye akili waliishatambua hili zamani

watasema hayo ni mawazo yake binafsi na sio msimamo wa chama,subiria utamsikia makamba anakuja na hiyo single.
 
A good leader must be intelligent enough to gather, synthesize, and interpret information, and above all he or she must be capable of solving problems and making correct decisions.
 
Nawapapole sana wale waliopata tisheti, kofia,na kurukaruka kama wanasesere,mabingwa wa kuchakachua kura za wapinzani,lakini sasa tupo wote katika msoto,afadhari tuliokuwa tayari kwa hilo kwani uliliona hili ndiomaana hatukuwa pamoja nanyi.Poleni sana kwa
Umeme
Maji
Vyakula nadhani mnajutia sana.
 
ukweli ndo huo maisha sasa yamekuwa magumu tena kuliko ENZI ZA MWALIMU, mie Guninita na muona ka katumwa vile??? Muungwana nadhani hata ndani ya chama chake kuna makambale ambao wameshaanza kuota masharubu.Mrema enzi zake NCCR-Mageuzi alikuwa anapiga chini watu kama hawa. CCM ni chama tawala, kwanini wasiyaongelee haya kwenye vikao vyao??? Tutaona mengi kuelekea 2015 ( si juzi mlimsikia mwingine anasema Mishahara ni midogo????? kwa uzalishaji gani? watu wavivu, wapenda short cut nk)
Jay Kei mpe uwaziri mkuu Magufuli!!!! mpe support uone mambo yatakvyoenda. Ukifurahishwa nae mpe mbeleko 2015 abebe bendera ya CCM.
 
Jamani jambo la msingi ni nini kimesemwa na kina manufaa gani katika taifa letu, na wala sio nani kasema. Huyu jamaa aliishawahi kuwa Chadema... Sawa lakini alichokisema ni ukweli na wala sio kumbeza.
 
Ameonesha kuchambua mambo kwa kutumia Busara na wala siyo msukumo wa Ushabiki.. Kudos!!
 
Tulimchagulia hao washauri au kajichagulia mwenyewe? kama mbwa akikuuma utamlaumu mbwa au mwenye mbwa? wasilete habari zao za ajabu hapa, wakubali wameshindwa kazi

na kama akishauriwa vibaya na akashindwa kujua kwamba hapa nimeingizwa mkenge basi anatatizo kubwa.
 
Hapa sijui CCM watasema huyu Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam kapotoka, watu wenye akili waliishatambua hili zamani
Hapo ndiyo tujue kujadili hoja badala ya watu. Hoja hiyo hiyo ikitolewa na CHADEMA wanaitwa wachochezi, akisema Lowasa, magufuli, au sita hataki kupindua nchi. Akisema Dr. Slaa, Mbowe au Lisu wanadai wananjama. Uchovu ni uchovu tu tena uchovu wakufukili ni mbaya zaidi. CCM wanampaka Mafuta kwa mgongo wa chupa rais, eti kashindwa kuongoza kwa sababu ya ushauri mbaya, kwani alipokuwa anaombakazi ya urais aliomba na washuri wake?. Lakini kama rais anashauriwa vibaya na kwa kipindi chote na hajui kama anashuriliwa vipaya si anapaswa kupimwa bongo yake?
 
Wanajf hii nayo imekaa vizuri. inafikia hadi wenyewe wanakiri udhaifu wao



:hand:CCM Dar: JK amekwama
• Yataka mitambo ya Dowans kuwashwa haraka

na Betty Kangonga


amka2.gif
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi, Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, amesema Rais Jakaya Kikwete ameshindwa kutatua matatizo mbalimbali yanayoikabili nchi kwa sababu ya kushauriwa vibaya.
Guninita alitoa kauli hiyo jana wakati akitoa ufafanuzi juu ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kupunguza tatizo la umeme linaloikabili nchi kwa sasa.
“Mambo mengi hayafanyiki kwa kuwa wapo watu wanaoshindwa kumsaidia Rais vizuri,” alisema Guninita.
Guninita alikuwa akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akitoa tamko la Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa iliyokutana Machi sita mwaka huu, kujadili kero mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo tatizo la umeme, kupanda kwa bei ya bidhaa, ajira na bomoabomoa.
Alisema kamati hiyo inaunga mkono ushauri na mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini juu ya serikali kutakiwa kuwashwa mitambo ya umeme ya Dowans ili kukabili upungufu wa umeme kauli inayopingana na msimamo wa awali wa viongozi waandamizi wa serikali.
Guninita alisema tatizo la umeme limekuwa kubwa na hasa ukizingatia ndiyo uti wa mgongo wa uchumi hivyo serikali ichukue hatua kuondokana na tatizo hilo.
Kuhusu bomoabomoa, Guninita alisema wamesikitishwa na hatua iliyofanywa na watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ya kufanya uvamizi na kuvunja vibanda vya wafanyabiashara ndogo ndogo wa eneo linalojulikana kama, Big brother lililoko Manzese, jijini Dar es Salaam.
Alisema kamati hiyo imeutaka uongozi wa Wilaya ya Kinondoni kuwachukulia hatua watendaji waliotoa agizo hilo ambalo limewatia hasara wafanyabiashara hao na wanapaswa kuwalipa fidia kwa hasara waliyoipata.
“Kitendo kilichofanywa si cha kiutu pia kimekiuka makubaliano yaliyokuwepo ya kuondoa mabanda 150 ili kupisha mradi wa mabasi yaendayo kasi na badala yake wamevunja mabanda zaidi ya 350 tofauti na makubaliano,” alisema.
Alisema wamemuandikia barua Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda ya kumtaka kuchunguza kwa haraka uharibifu uliojitokeza pamoja na kuhakikisha wafanyabiashara wote wanalipwa haki zao.
Kuhusu mfumko wa bei ya vyakula, Guninita alisema wameishauri serikali kuhakikisha inaunda tume maalumu itakayowajibika kufuatilia na kusimamia bei ili kuhakikisha wananchi wanapata mahitaji yao kwa bei nafuu.
“Kamati imetafakari na kubaini kuwa hakuna sababu ya sukari inayoingizwa nchini na msamaha wa kodi kuuzwa kwa bei ya 1,700 kwa kilo wakati gharama za kuagiza hadi kufika nchini ziko chini,” alisema.
Alisema serikali inatakiwa kwa kipindi kifupi kutafuta ufumbuzi wa tatizo la kupanda kwa bei ya vyakula na kuhakikisha bei hizo zinashuka kwa haraka sambamba na kuagiza bidhaa muhimu kama vile sukari, mchele na maharage.
Guninita alisema pamoja na kushuka kwa bei, bado serikali inatakiwa kuwachukulia hatua wafanyabiashara wanaokwenda kinyume na bei zilizopangwa.
Kwa upande wake Mbunge wa Ilala Musa Zungu (CCM), alisema hakuna sababu ya bidhaa na vyakula vinavyopata msamaha wa kodi kuuzwa kwa bei ya juu maana kufanya hivyo ni kutaka kuwaumiza wananchi.
Aidha, juu ya tatizo la ajira nchini, alisema serikali inatakiwa itenge fedha katika bajeti ya mwaka 2011/12 zitakazotoa msukumo katika kuwapatia vijana ajira kama ilivyofanya mwaka 2009 ilipoamua kutenga kiasi cha sh trilioni 1.7 kusaidia kuinua uchumi.
“Kwa kuwa tatizo la ajira kwa vijana ni ajenda endelevu ambayo inahitaji utekelezaji usiokoma, hivyo bajeti zetu zote za kila mwaka lazima ziongeze fedha na kasi ya kuwapatia vijana ajira,” alisema.

Hii kamati itakuwa haijamsikia Mh. Chiza, " serikali haiwezi kudhibiti mfumuko wa bei ya vyakula"............Its a total System failure!
 
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi, Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, amesema Rais Jakaya Kikwete ameshindwa kutatua matatizo mbalimbali yanayoikabili nchi kwa sababu ya kushauriwa vibaya.
Guninita alitoa kauli hiyo jana wakati akitoa ufafanuzi juu ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kupunguza tatizo la umeme linaloikabili nchi kwa sasa.
“Mambo mengi hayafanyiki kwa kuwa wapo watu wanaoshindwa kumsaidia Rais vizuri,” alisema Guninita.

The buck stops at the president's hands; yeye ndiye mwamuzi, kukitokea kosa basi ni yeye ndiye anayelaumiwa, siyo washauri wala nini, kwa sababu President halazimishwi kuchukua ushauri wa mtu yeyote. Anatakiwa asikilize ushauri huo, auchambue, halafu atoe uamuzi wa mwisho. Kisingizio cha rais kushauriwa vibaya ni upuuzi nisiokubaliana nao. Tukubuali tu kuwa rais wetu ni kilaza
 
Hapa sijui CCM watasema huyu Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam kapotoka, watu wenye akili waliishatambua hili zamani
Nasikia Rais anajipanga kuhutubia taifa tena ili akemee kauli ya mwenyekiti huyo wa mkoa kuwa anachochea vurugu kwa kusema kuwa ameshindwa kutatua kero kwa wananchi.
 
Kama CCM wameyaona hayo nawashauri wamfukuze mwenyekiti wao wa Taifa na mnyang'anye uanachama kabisa kwa vile anakidhalilisha chama. Mfuteni uanachama kama mlivyotaka kufanya kwa Bashe.
 
Pandikizi la hali ya juu msimpe kichwa, angalieni the bottom line jamani hayo yote ni vuvuzela anachokifanya hapa ni kutaka kufufua matumaini ya tume ya January ya kuwasha dowans, huyu ni wa kulipwa kama alivyotumwa kwenda kutekeleza mkakati wa kumfukuza samwel sita chama wakati ule mpaka, ni mjinga wa darasa la saba anayeishi kwa makombo ya posho za mikutano. Hana akili hebu someni hizo arguments zao, hivi bei ya vyakula itapunguzwa kwa kuunda tume? yale yale, hakuna tatizo hapo linalojitegemea yote yanatokana na uongozi mbovu na unafiki wa wanachama wa CCM, hivi watu 4m watamuachaje mtu mmoja JK kuua chama chao hali wakiwa wamenyamaza kimya? na kwa nini wamejaa unafiki wa kusema JK anapotoshwa inamaana wao hawaoni kwamba JK hana uwezo na hajui anachofanya? kama bogi benda Guninita ana akili aende kwenye chama chao asimame aseme kwamba mwenyekiti umeshindwa umeua chama tunakuomba ujiuzulu utuachie chama chetu. Huku nje anajikomba tu na sisi tumeshamshitukie tena nashauri tuache hata kuchangia hii thread tusimpe kichwa katumwa na RA na wahanga wake. Hivi CCM inaanzaje kuiamuru serikali hawa hata katiba hawaielewi jamani tunakazi kubwa sana na vichaa hawa tusikubali kugeuzwa misukule down with him and his party rubbish kabisa
 
CCM wamchoka JK
• Wadai tishio la kumng'oa liko ndani ya CCM

na Mwandishi wetu
Tanzania Daima



KUNA kila dalili za wafuasi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kufikia hatua ya kumchoka mwenyekiti wao, Rais Jakaya Kikwete, kutokana na kushindwa kuchukua maamuzi mazito kukinusuru chama hicho na taifa kwa ujumla, Tanzania Daima Jumatano, limebaini.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili na maoni yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya vigogo wa chama hicho, wakiwemo viongozi wastaafu tangu alipotoa hotuba yake ya mwezi uliopita, umebaini kuwa Rais Kikwete amebebeshwa mzigo wa lawama kwa kushindwa kuchukua maamuzi mazito na kusababisha taifa na chama hicho tawala kuwa na wakati mgumu.

Maamuzi ambayo Rais Kikwete amekuwa akitakiwa kuyachukua ni pamoja na kuwatimua wanachama wote wanaokabiliwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi na kukisababisha chama hicho kupakwa matope ya ufisadi.
Lawama dhidi ya Kikwete zimekuwa zikitolewa na vigogo hao hadharani hasa kwenye mgahawa wa Falcon, ulioko jirani na ofisi ndogo ya makao makuu ya CCM, iliyoko mtaa wa Lumbumba, jijini Dar es Salaam.

"Hayo magoli tumejifunga wenyewe, tumepigwa magoli kwenye uchaguzi wa wabunge na madiwani, mwenyekiti ameshindwa kufanya maamuzi magumu, yaliyokifikisha chama hapa kilipo. Leo CHADEMA wanakwenda kwa wananchi kuelezea udhaifu wetu, tunakuja juu, eti uchochezi, uko wapi huo uchochezi, je, ni uongo kwamba gharama za maisha haziko juu, je, ni uongo kwamba Dowans tumeilea na wahusika tunawajua?" alihoji kada huyo ambaye ni mmoja wa makatibu wa mikoa ya Tanzania Bara.

Kiongozi huyo wa CCM mkoa, alisema wanasubiri kwa hamu kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, (NEC, kinachotarajiwa kufanyika mwezi huu mjini Dodoma ili kufanya mageuzi makubwa ya uongozi ndani ya chama kama alivyoahidi Rais Kikwete hivi karibuni.

"Safari hii NEC nadhani patachimbika, watu wana madukuduku mengi, tangu kumalizika kwa kura za maoni na hata uchaguzi hatujakutana, tutamuuliza Rais kama tuna sababu ya kuendelea kubaki na watu ambao leo wametufikisha hapa," alisema.

Kigogo mwingine aliliambia gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina lake kuwa mbali ya kufanya maamuzi mazito, Rais Kikwete pia anapaswa kutoa majibu ya kina ya kuwatosheleza Watanzania kutokana na matatizo mbalimbali yanayolikabili taifa badala ya kuelekeza lawama zake kwa CHADEMA.

"Kikwete ameendelea kukumbatia na kuwalinda mafisadi na watuhumiwa wa kashfa mbali mbali na mfano ni sakata la Richmond na baadaye Dowans. Hawa watu sasa waondoke na mwenye uwezo wa kuwaondoa ni yeye," alisema.

Kigogo huyo ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu (CC) ya CCM, alitaja baadhi ya mambo yanayohitaji utekelezaji au ufafanuzi wa kina ni pamoja na hatma ya haki za wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu ambao wamekuwa wakifanya maandamano kushinikiza kuongezewa fedha za kujikimu.

"Tatizo kama la kupanda kwa gharama za maisha na kuzidi kushamiri kwa ufisadi unaokingiwa kifua na Kikwete huyu huyu. Hapa hujagusa mfumko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha, haya yote wananchi wanayaona, sasa CHADEMA wakifanya maandamano kupinga hali hiyo, tunadai wachochezi uko wapi?" alihoji kigogo huyo na kumtaka Rais kujibu hoja.

Pili, mauaji ya raia wasio na hatia. Rejea mauaji ya Arusha, milipuko ya mabomu kule Gongo la Mboto na Mbagala, nayo alisema ni mambo yanayohitaji majibu ya kina. Kwa mujibu wa kigogo huyo, limo pia tatizo la kupunjwa, kunyonywa na kudanganywa kwa nyongeza ya mishahara ya wafanyakazi, ukosefu wa ajira kwa vijana tofauti na Ilani ya CCM aliyoinadi kwenye kampeni za uchaguzi mwaka 2005/2010.
Kauli za vigogo wastaafu

Kauli ya viongozi wastaafu kama aliyoitoa Waziri Mkuu mstaafu juzi, Frederick Sumaye, kwamba CCM ijibu hoja za CHADEMA, imezidi kumuweka njia panda Rais Kikwete.
Habari zinasema kuwa kauli ya Sumaye na zingine ambazo zimekuwa zikitolewa na viongozi wastaafu, zimekivuruga chama hicho na kinakusudia kuwaita baadhi yao kwenye Kamati ya Maadili kwa ajili ya kuwahoji.

Sumaye alikaririwa juzi akisema kuwa CCM inatakiwa kukabiliana kisiasa na hoja za CHADEMA na si kuiachia serikali ipambane nao.
Kwa mujibu wa Sumaye, kazi ya siasa ni ya chama na si serikali, hivyo CCM inapaswa kuwa mstari wa mbele kupambana na CHADEMA kwa sera na kujibu hoja zake zote ili kuongeza imani ya wananchi kwa chama hicho.
Sumaye alisema si ishara nzuri kwa CCM kukaa kimya wakati wapinzani wanaendelea kukishtaki kwa wananchi kuwa kimeshindwa kufanya kazi.

Wakati Sumaye akisema hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni John Chiligati, alisema kuwa nyendo za CHADEMA zina agenda ya siri ya kuking'oa madarakani kwa kutumia nguvu kinyume cha Katiba hivyo kuitaka serikali na vyombo vya dola kuchukua hatua za kisheria haraka. Sumaye hakuishia kuishauri CCM kuja na hoja za kisiasa kujibu mapigo ya CHADEMA, bali pia alieleza aina ya watu wanaofaa kukiongoza chama hicho tawala wakati huu wa mabadiliko makubwa ya kisiasa. Sumaye alisema CCM inahitaji viongozi waadilifu, wachapakazi na wasio waoga kumshauri Rais ili kuwa na mabadiliko ya kiutendaji yanayoendana na joto la kisiasa lililopo.
 
Back
Top Bottom