CCM yakatakaza wagombea wake kuonekana TBC1, Tido Mhando ataarifiwa

Ukimsoma Makamba ndio unaweza kuelewa ni kiasi gani viongozi wetu wana ufinyu wa kufikiri kwa kiasi gani.. Kisha tunashangaa kwa nini nchi yetu bado maskini..
Sikutegemea kabisa kusoma majibu hayo ya Makamba, na hakika inaonyesha wazi Makamba na chama CCM wanaamini kwamba sii kazi ya wananchi kuhoji na kuchagua mgombea wao bali ni kazi ya chama kuamua wao watamweka nani kugombea..Anashindwa kuelewa kwamba Mdahalo ni matakwa ya wananchi kwa vyama vya siasa kufuata ili wagombea wao wapate kuchaguliwa na sii maamuzi ya vyama vya kisiasa kutoa maamuzi ya kushiriki au kutoshiriki..

Kitendo cha Makamaba kuagiza wagombea wake kutoshiriki mdahalo wowote ni utovu wa nidhamu kwa kiongozi huyo kwa wananchi wake. Haina tofauti kabisa na yale maneno ya Jk alipowaambia wafanyakazi hahitaji kura zao. Naomba vyombo vya habari vizungumzie sana maamuzi haya ya Makamba ambaye anaonekana kufikiria kwamba CCM ndio mtawala yuko juu ya maamuzi yote hata ktk maswala muhimu kama ya uchaguzi.
 
Ndugu wanajamii kwanza niwapeni pole kwa shughuli za hapa na pale hasa mchakato wa uchaguzi wa 2010 tumekuwa busy tukifuatilia nini wanachokifanya wagombea wetu katika sehemu mbali mbali.
Kilichonisikitisha kuliko vyote ni kusikia ccm wamekataza wagombea wao kutoudhuria midahalo inayoendeshwa na chombo kikubwa cha mawasiliano tena cha TAIFA. K WA AKINA MIMI ambao kwenye siasa hatuelewi mambo mengi ila naamini hapa jamvini tunao wataalamu wa kutosha ambao wamekuwa wakielezea hoja tofauti na zikaeleweka! sasa hv ccm wametenda haki?

NAWATAKIENI CKUKUU NJEMA WANAJAMIII!!
 
sikuamini kabisaingewezekana Makamba akazungumza aliyoyazungumza kuhusiana na midahalo! Kumbe huyu niz ziro kiasi hiki!
Hawezi kujua nguvu ya TV katika kujinadi au ameamua kujifanya kiazi kwa kuwa watu wake wamekuwa wakichemsha!

Hivi ni kwa nmna gani tunaweza tukamshitaki, tukamwondoa; mimi naona anawadhalilisha CCM. WATETEZI WAKE SIJAWAONA HAPA .L OOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
 
Ndo tatizo la kuchakachua wagombea
Kwa vigezo visivyoeleweka
Sasa CCM Kazi wanayo

Matatizo ya wagombea wa CCM yameletwa na CCM yenyewe,Kukimbia mdahalo sio kutatua matatizo bali ni kuongeza matatizo,na mashaka juu ya upeo,uwezo,dhamila yao kisiasa.Warudi nyuma back to the drawing board,wajipange upya.Kila mwanachama wa CCM anaweza kuwa mpiga kura,lakini sio kila mwanachama anaweza kugombea udiwani,ubunge na uraisi.Vigezo vilivyotumika ndio hivyo vya kuchakachua gabbage in gabbage out.
 
Tanzania tuna viongozi wa ajabu kweli. Yaani Makamba anadiriki kucontrol wagombea wasionekane kwenye TV? Najua kuwa wagonbea wake wamekuwa wakizidiwa sana na wale wa upinzani kwenye midahalo, lakini asingewzuia wasiende kwenye midahalo bali angeaambia wawej wanajiandaa vizuri. Makamba ni bure kabisa, alikuwa mtoa burudani wa TPDF, na hiyo bado inajionyesha katika utendaji wake wa kazi za kisiasa.
 
TBSIIIIII Haya goma lipo kwenu lipeni fadhila kwa highest BIDDER KUDOS CCM kwa kujiona hamuwezi midahalo
 
I hopr vyama vya Upinzani watatumia nafasi hii kuwafahamisha wananchi jinsi CCM isivyotaka kuwajibishwa kwa sababu wanafikiri ndio wawajijibishaji kama mkoloni vile (Watawala)
 
Ndiyo chama cha mafisadi hicho, pamoja na kuwa wanapenda kubaki madarakani lakini wanaogopa kutetea hoja zao mbele ya Watanzania. Kama wangekuwa na sera nzuri na utendaji mzuri katika awamu inayokwisha basi wangekuwa mstari wa mbele kujipiga kifua kwa utendaji wao, lakini kwa kujificha huku ina maana hata mafisadi wenyewe wanajua hawana sera na awamu inayokwisha wamefulia. SHAME ON YOU CHAMA CHA MAFISADI.
 
Kama wapinzani wataweza kutumia vizuri mwanya huu wa kucontrol wagombea uliofanywa na CCM na ku-link na kucontrol wabunge hata kama watakao kuwa tayari kutetea masilahi ya waliowachagua basi huenda wananchi wakaelewa kitu hapa kuwa, Chagua CCM wakafanywe mabubu bungeni na rubber stamps au chagua upinzani wakatetee masilahi ya wananchi kwa nguvu zote.
 
ofcoz tutashinda bila hata ya TV! wapiga kura wetu wengi wapo vijijini hawa time na TBC1! tunaawachia chadema mjifurahishe
 
Makamba awaweka pabaya wagombea CCM
Thursday, 09 September 2010 07:23

“Tuna utaratibu mzuri wa kijinadi na kunadi sera zetu kwa wananchi; utaratibu wa mikutano ya hadhara na mikutano ya ndani. Utaratibu huo bado unakidhi haja. Tunaendelea nao,” alisema Makamba.

Akizungumza na gazeti hili jana, Makamba alisisitiza akisema: "Hatutaki. Tumekataa ndio. Sisi yetu ni mikutamo ya hadhara. Tutaeleza huko malengo, ilani yetu na sera zetu kwa wananchi. Hatuoni sababu ya kukaa katika chumba kidogo na kuwapa nafasi ya ushiriki watu wachache."

Aliendelea: "Hatuoni sababu ya kwenda kwenye huo mjadala kwa kuwa mikutano yetu ya hadhara inajitosheleza."

CCM kwa ujumla hawajiamini, hawawezi kukaa kwenye mdahalo na kujibu hoja za watanzania kwa vile wanajuwa watabanywa vilivyo kutokana na ahadi zao nyingi za uongo! Kwa vile wanapenda kujifananisha na taratibu za Marekani au Uingereza, mbona kwa hili hawajifananishi? Marekani na Uingereza wagombea walishiriki midahalo na sisi huku nchi masikini tuliwaona, iweje CCM? Wakati JK akitoka kuchukua form, Makamba alisema "...Kikwete ametoka vitani na kitu cha kuonyesha...", sasa kama wanaCCM wana kitu cha kuwaonyesha watanzania, siwashiriki midahalo ili wawaonyeshe wapiga kura wao walichorudi nacho toka vitani?
CCM imechokwa na watanzania wenye uchungu na nchi yao. Kama ndiyo hivyo-vyombo vya habari viache kuonyesha shughuli zao za kampeni kwenye TV kwa sababu wao wana taratibu zao ambazo Makamba amezisema!
Sisi wanawanchi tunaona kuwa, wataumbuka kwa vile inajua udhaifu wa wagombea wao katika kuleta maendeleo ya nchi. Wengi wa wagombea wa CCM watapita kwa kusaidiwa na nguvu ya dola ikiwemo ya kuiba kura. Hata kama wakatae Midahalo, wananchi WAMEWACHOKA!
icon8.png
 
ofcoz tutashinda bila hata ya TV! wapiga kura wetu wengi wapo vijijini hawa time na TBC1! tunaawachia chadema mjifurahishe

Wewe wewe njiwa wewe.... hivi umeruhusiwa na katibu Makamba kujiunga JF na hata kutoa maono yako hapa?! Au ndiyo hivyo tena umepeperuka tu baada ya kiota chako kutikiswa na wanaupinzani?!.... mweeeh, shauri yako... wee ngoja urudi ukute bundi wa Kinana wameshatotoa vichanga kwenye kiota chako!!!


Seriously, nawaonea huruma outspoken members wa CCM walio proponents wa openness na accountability ambao wangelipenda kujitokeza kwenye midahalo kama hii!!
 
Kitu ambacho kimeshangaza wengi ni CCM kuzuia wagombea wake kushiliki midalaho na wagombea wa vyama vingine.

Swali ninalo jiuliza ni kuwa CCM wanategemea kuwa watapataje kura bila kuwaeleza wana nchi nini watafanyia? Je hawaoni kuwa itawafikia asilimia kubwa ya wananchi kwa njia hii .
Nahisi wanafahamu umuhimu wa midahalo hii ila inaonyesha kiasi gani wanaogopa maswali toka kwa wananchi ,wanaogopa kuulizwa kuhusu ahadi zilizopita zimetekerezwaje .

Sisi kama wananchi ni vema tukaangalia jinsi CCM invyo tu treat ,na kutompa kura mtu anayeshindwa kujibu waswali ya wananchi wezako wa jimbo lako either hususani kwa kuto kuwepo kwenye mdahalo.

CCM mtapataje kura bila kupita kwenye mzani wa mdahalo? No mdahalo no kura,kwa maoni yangu
 
ofcoz tutashinda bila hata ya TV! wapiga kura wetu wengi wapo vijijini hawa time na TBC1! tunaawachia chadema mjifurahishe

Sasa hilo hashuwo la kuwazimia matangazo ya kampeni la nini?
 
Mimi nadhani TBC iwatengenezee kipindi chao maalum CCM wafanye mdahalo wao wenyewe tu nadhani watakubali.
 
hivi,ukimuangalia Makamba usoni, frankly speaking, unaweza kuona dalili zozote za umakini??
 
Nakubaliana na hoja ya NO Mdahalao NO kura.. kwani ni dharau kubwa kwa upande wa CCM kwa wananchi na wapiga kura wake. Tatizo hawajaelewa maana ya uongozi ambayo inahusisha ACCOUNTABILITY pia... ila nionavyo hawataki kuwa accountable ... hii ni pointi muhimu sana kwa uinzani kulizungumzia....
 
Back
Top Bottom