CCM Yajivua Magamba, CDM Yazindua Operasheni ya Twanga Kotekote; Sasa Kila Mmoja Atafsiri kivyake.

LINCOLINMTZA

JF-Expert Member
Mar 15, 2011
1,639
516
Siku chache zilizopita nilijaribu kubadilishana mawazo na wanajamvi katika tafsiri ya CCM kujivua gamba kwamba ilikuwa inapotoshwa kwa kufananishwa na nyoka badala ya lengo lake.

Sasa CDM wamezindua operasheni inayoikwenda kwa jina la "Twanga Kotekote" https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/131685-chadema-yazindua-operesheni-twanga-kotekote.html.

Tusipopata au tusipoamua kuangalia tafsiri ya lengo la operasheni hii na kujikita katika maandishi, si ajabu watu wengine wakapotosha lengo la operaheni hii either kwa makusudi au kwa kutokujua.

Naomba mwenye maelezo zaidi kuhusu lengo la Operasheni yenyewe atujuze na ninaomba wanajamvi kuangalie zaidi lengo la ujumbe siyo kutafsiri maandishi kama yalivyo.

Naomba kutoa hoja.
 
Back
Top Bottom