CCM yajiongezea CV ARUMERU

Mbona tbc hawajarusha hii au siku yake haijafika? huyu akizeeka atakuwa mchawi anaweza kuuwa kwa sababu umenunua bicycle tu
 
Dah, ama kweli CCM imeishiwa sera asilani.. yote yana mwisho. Ukweli utabakia tu hata kama Lusinde atapamba jukwaa kwa haya matusi. Nawashangaa wanaomsikiliza..Issue ya uzawa aliaanza wenyewe ndani ya ccm, ushoga walianza wenyewe kushutumu kuwa vyama vingine vinauhusiano na Dvd Cameroon, kutoga sikio si issue kwani mtu anachaguliwa kutokana na sera siyo matusi ndugu yangu Lusinde. Jaribu kufikiria ni siasa tu za kibongo zinakuondolea heshima ya kuwa baba wa familia bora. Unasahau wanakuangalia watanzania wangapi ambao hawafungamani na chama chochote, je hawa nao utawaambiaje? Umetukana hadi matusi yanguoni ambao ukiambia uthibitishe hutaweza. Unafika mahali unakikashifu chama chako kwa sera mbovu za magereza badala ya kuwa sehemu nzuri ya kuwahifadhi watuhumuwa, sera mbovu zimefanya mageraza kuwa sehemu ya kuendeleza mapenzi ya jinsia moja.

Nikukumbushe ndugu yangu, utawala wa kidikteta ndiyo unarithisha madaraka lakini si utawala wa democrasia. Ninsingependa kurudia maneno yako uliyosema katika clip hii fupi lakini ndugu yangu siasa na kampeni zinapita ila wewe utabaki sijui utaficha wapi huo uso wako..... CDM kitanshinda na wewe utakuwa mtanzania unayetegemea huduma serikali kutoka kwa hao hao unaowakashfu leo..... Sijui utasimama wapi, kumbuka utu ni dhamana hauuzwi super market, siyo tu wewe mwenyewe umeumbiwa matusi humu duniani/ au huko ccm ila jiulize mbona wenzanko hawatukani hadharani? Usijekujeuka kijago cha mpapure kwa wana CCM wenzako kwa mdomo wako mwenyewe..

Punguza jazba, nadi sera za CCM acha ugomvi binafsi ukitumia jukwaa la sihasa, sema ukimnadi Sioi akipita utafanya nini na siyo 'kuwalamba' chadema. Kampeni zinahudhuriwa na watoto wadogo ambao si chadema wala ccm kwani hawajafika umri wa kupiga kura, wewe kama mzazi mwanandoa unawafundisha nini na unawajengea nini katika akili yao watakapokuwa shuleni na pia kwa maisha yao baadae? usipende kujidhalilisha na kudhalilisha utu wako ndugu yako, hizo ni siasa tu, kaka zina mwisho......Fikiria kabla ya kutenda ndugu yangu....
 
Lusinde hata uchaguzi wake ameshinda kwa mbinde, ukijumlishia na matusi yake..namhakikishia 2015 hatakatiza kwenye ubunge. Ni bora akatumia huu muda vizuri kujenga marafiki na wala sio kuongeza maadui..coz soon itakiona cha moto..siasa za kujisahau.
 
Ukiacha Chama Cha Magamba, sasa ni Chama Cha Matusi huko ARUMERU. Loh!!

Ona Hapa: Mh. Livingstone Lusinde akimwaga Sera za CCM Arumeru - YouTube

Mkuu ahsante sana. Nimemsikia Lusinde akimwaga hayo matusi, hata sikuamini kweli huyu ni mbunge katika lile linalojulikana "Bunge Tukufu". Yaani CCM wameishiwa kiasi hiki? Mimi nauliza kwa Mhe Lema, hakuna namna tunavyoweza kufanya kumfikisha huyu jamaa mahakamani? Hivi tuna acha hivi hivi tu? No way.

Haya hongera Nape, hongereni CCM, lamsingi ni moja tu, msiibe kura na muwaache wana Arumeru wachague.
 
Lazima alikuwa keshalivuta........... Chama Cha Mabangi. Loh!!
 
Back
Top Bottom