CCM yaiteka Songea (picha)

Kwa wataalamu wa picha mmeshaelewa hapo namna picha ilivyopigwa,cha kuongezea tu mkutano haukuwa na watu wengi kama inavyotaka kuaminishwa hapa,zimanimoto ni uwanja mkubwa sana lakini watu walikuwa ni wachache mno waliokuwa wanaangalia mechi ya songea boys uwanja wa majimaji unaopakana na zimanimoto walikuwa wengi kuliko hao waliokuwa kwa Nepi
 
Salamu wana JF,
Napenda kujumuika nanyi kwa mara nyingine tena juu ya uwezo na ushujaa alionao kijana mzalendo Mh.Nape kwa kazi ngumu aliyokabidhiwa na CCM,kwanza kabisa amefanikiwa kuwatingisha mafisadi nguli ndani ya chama kwa kipindi kifupi alochoongoza pia anapambana na kelele za CHADEMA zenye nia ya kumkatisha tamaa ambazo bila shaka zinapata support ya MAGAMBA waliopo CCM ambao hawataki kutii amri ya kujivua ili chama kibaki salama bila kuleta chuki kama alivyofanya RA.

Kwa ujasiri alionao bila shaka anatakiwa apewe meno zaidi ya kuwashughulikia mafisadi pamoja na njama za CHADEMA kutumia mgongo wa MAGAMBA,CCM inaiimarika kila siku,watu wanafanyakazi kwa uadilifu,mfumo unabadilishwa ili kukidhi matarajio ya wananchi kupata huduma bora.
NAPE ni moto mkali kwa CHADEMA ndiyo maana hawalali bila kuuliza Mh.NAPE katoa kauli gani kila siku ili wabuni njia mpya ya kumkatisha tamaa...mfano mzuri ..VUA GAMBA VAA GWANDA.....huu ni upuuzi wa copy & paste !

Nilitegemea CHADEMA wawe focus kupata wanachama waadilifu badala ya kusubiri magamba wajiunge kwao.....HONGERA sana Mh.NAPE kwa kuwapa dozi nzito ya kuvua MAGWANDA wavae UZALENDO kama WEWE !

Tunahitaji viongozi wenye UTASHI wa KIZALENDO zaidi badala ya CHAMA kama Mh.ZITTO,Mh.KAFURILA,Mh.MACHALI,Mh.FILIKUNJOMBE,Mh.MKOSAMALI,Mh.MNYIKA nk
CHAMA kitumeke kama njia ya kupazia sauti tuuu na si ushabiki wakijinga kama anavyofanya WENJE,LEMA na baadhi ya wanaCDM....

Wewe ni miongoni mwa wale vijana wa chuo cha chap chap mlioandamana kumpongeza rais kwa uteuzi wa mawaziri.hivi nanyie payrol yenu haijaasirika kama watumishi wa umma?
 
hao watu wote ni matokeo ya fuso transport toka kila kata ya vijiji vinavyoizunguka songea.,halafu ccm mnalazimika kununua t-shirt kwa mamia kwa kila mkutano mtakaoufanya pamoja na kofia na ukodishaji wa fuso na pikipiki.je mtaimudu kasi ya cdm?
Ila subiri uone cdm itakapoingia hapo ndio utaona tofauti kati ya peoples power na jhao chumia tumbo na wafuata t-shirts na kofia

kuwa na huruma wewe unafikiri bila fuso hapo nape angekaa na nani?
 
nape anatamani akunje ngumi, kunyoosha mikono juu anamaanisha nini? masikini ya Mungu anataabika huyu jamaa, ubongo wake unafanana na mwili wake
 
Ccm wameiteka songea toka kwa akina nani ? Hapo ni sawa sawa na mtu anapigana na kivuli chake .Ngoja Makamanda wafike maeneo hayo utaona mpambano wa ukweli .
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom