CCM yaingiza kichwa CHADEMA katika mgogoro wa meya Arusha na kujitangazia muafaka bila idhini

Fasta fasta

JF-Expert Member
Feb 15, 2011
1,126
725
[h=2][/h]

Main(96).jpg

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamko la kuwafukuza madiwani wote wa chama hicho Jijini Arusha ambao walishiriki kukubali muafaka wa Umeya wa jiji hilo.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kuwatimua ndani ya chama madiwani wake wote watakaobainika kuhusika na mwafaka wa kilaghai kati yao na madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwafanya wakubali kupewa nafasi ya Unaibu Meya katika Jiji la Arusha.

Kadhalika, Chama hicho kimesema kitamweka ‘kiti moto’ Mbunge wa Maswa Magharibi kwa tiketi ya Chadema, John Shibuda, kwa kukiuka makubaliano ya chama na wabunge wenzake kwa kutangaza kwamba atachukua posho za vikao vya Bunge.

Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Willibrod Slaa alitangaza maamuzi hayo jijini Dar es Salaam jana kuwa kuna ushahidi unaoonyesha kwamba madiwani waliokubali mwafaka jijini Arusha walinunuliwa.

Hata hivyo, Dk. Slaa hakusema viongozi hao walinunuliwa na nani na kwa kiasi gani, lakini alisisitiza kwamba walipewa rushwa ndiyo maana walifanya maamuzi hayo kinyume cha msimamo wa chama.

Dk. Slaa aliwaambia waandishi wa habari kuwa Chadema kipo tayari kupoteza kitu chochote hata kama ni kitamu kiasi gani ikiwa kitabainika kilipatikana kinyume cha taratibu pamoja na demkorasia.

MARANDO KUONGOZA UCHUNGUZI
Dk. Slaa alisema kuwa kwa kutumia kifungu cha 11 cha Katiba ya Chadema, ameunda kamati ya watu watatu itakayoongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, na Mwanasheria gwiji, Mabere Marando, kuchunguza madiwani waliohusika na mwafaka huo na kila mmoja kwa kiasi gani ili Chama kiwachukulie hatua.

Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Razaro Maasai ambaye ni Mwenyekiti wa Mameya wa Majiji na Manispaa pamoja na Wenyeviti wa Halmashauri ambazo zinaoongozwa na Chadema na Ester Dafi, wanasheria wa Chadema Makao Makuu.

Kamati hiyo imepewa siku sita kuanzia jana ili kukamilisha uchunguzi wake na kwamba taarifa itakazopata zitasaidia kuongeza ushahidi wa kuwachukulia hatua madiwani waliohusika katika njama hizo.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, kuna watu wengi wanahitaji nafasi hizo hivyo Chama hakioni tatizo kuwatimua viongozi wanaokiuka taratibu na sheria.

Alisema Naibu Meya aliyechaguliwa kupitia mwafaka huo kwa tiketi ya Chadema, Estomiah Mallah, jina lake halikujadiliwa katika kikao chochote cha Chama kama ilivyo kawaida.

Aliongeza kuwa Chadema ni chama kinachosema ukweli daima na kukemea maovu, hivyo hakiwezi kusita kuwachukulia hatua wanachama wake wote wakiwemo madiwani, wabunge na hata angekuwepo Rais kama watabaini amekiuka taratibu.
Dk. Slaa alisema madiwani watatu kati ya wanane katika jiji la Arusha ndiyo walioingia kwenye mkutano ambao mwisho wake walitangaza kuwa wamefikia mwafaka na kukubali cheo cha Unaibu Meya.

Alisema kikao hicho kiliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini, Raymond Mushi, na kwamba idadi ya Madiwani wote ni 21, lakini anashangaa kusikia walioshiriki katika kupata mwafaka huo walikuwa tisa akiwemo mmoja wa TLP na wengine wanne wa CCM.

Alisema wananchi wa Jiji la Arusha wanachotaka ni kuona haki inatendeka na sio kupata viongozi ambao wamepatikana kinyume cha kanuni, taratibu na sheria za uchaguzi wa meya na naibu wake.
Aidha, alisema Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, waliomba kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ili kupata ufumbuzi wa suala hilo, lakini wameshangaa kusikia watu wachache wamerubuniwa na kukubali mwafaka kwa njia za mkato.
Mgogoro wa uchaguzi wa Meya katika Jiji la Arusha ulianza Januari mwaka huu baada ya Chadema walilalamikia mchakato wa kumpa kiongozi huyo.

Chadema walisema zoezi la upigaji kura kwa ajili ya kumpata Meya liliendeshwa vibaya ikiwemo mjumbe asiyekuwa na sifa za kupiga kura, Mary Chatanda, Mbunge Maalum wa Viti Maalum (CCM), kushiriki kumchagua kiongozi huyo.

Kutokana na hali hiyo, Chadema kilipinga hatua hiyo na kuandaa maandamano Januari 5, mwaka huu jijini Arusha, ambayo mwisho wake yalisababisha mauaji ya watu watatu yaliyofanywa na Jeshi la Polisi na wengine kujeruhiwa.
Kutokana na hali kuwa tete na watu kupoteza maisha, Dk. Slaa alisema Chama hakiwezi kukubali kuona mambo yakimalizika kinyemela kwa kivuli cha mwafaka na kwamba kinachotakiwa ni haki na sio kitu kingine.

Wiki iliyopita, madiwani wa Jiji la Arusha kutoka vyama vya CCM, Chadema na TLP, walitangaza kufikia mwafaka ambapo walikubaliana kwamba Gaudence Lyimo (CCM) aendelee kuwa Meya na Estomiah Mallah (Chadema) ashike Unaibu Meya hadi mwaka 2014 kisha diwani wa TLP achukue Unaibu Meya hadi mwaka 2015 kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu.

Katika mwafaka huo pia waligawana kamati za Baraza la Madiwani.

Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya itaongozwa na diwani wa Chadema; kamati ya Fedha na Utawala itakuwa na wajumbe tisa, wanne kutoka Chadema na mmoja wa TLP, huku CCM ikiwa na wajumbe wanne tu, itakuwa chini ya Meya (CCM) na kamati ya Mipango Miji na Mazingira itaongozwa na diwani wa CCM.

Taarifa za mwafaka huo ziliwekwa hadharani Juni 20, mwaka huu katika mkutano wa Baraza la Madiwani wa Jiji la Arusha ukihusisha madiwani wote wa CCM, Chadema na TLP.

Hata hivyo, Dk. Slaa hakusema viongozi hao walinunuliwa na nani na kwa kiasi gani, lakini alisisitiza kwamba walipewa rushwa ndiyo maana walifanya maamuzi hayo kinyume cha msimamo wa chama.
Dk. Slaa aliwaambia waandishi wa habari kuwa Chadema kipo tayari kupoteza kitu chochote hata kama ni kitamu kiasi gani ikiwa kitabainika kilipatikana kinyume cha taratibu pamoja na demkorasia.

Mie nashindwa kuelewa mbona wamekaa wiki nzima tangu muafaka utangazwe ndio wakaja kutoa tamko? something smell fishy here.....

Ngoja ninyamaze nisije pigwa BAN maana watu wanahasira sana.
 
Mie nashindwa kuelewa mbona wamekaa wiki nzima tangu muafaka utangazwe ndio wakaja kutoa tamko? something smell fishy here.....

Ngoja ninyamaze nisije pigwa BAN maana watu wanahasira sana.

Watu makini siku zote hawakurupuki kusema hili then kesho wakasema lile. Walikuwa wakitafiti kulikoni nini kimetokea nani kahusika na logistics nyinginezo.
 
Mbona nyie mmekaa miaka mitano na matatizo ya umeme tukisema mnasema wachochezi? nyaaaani haoni kunduleeeeeeeeee

Mbona wakisikia kuna kontena la karatasi za kupigia kura hawamakiniki wanaropoka hovyo?
 
Mie nashindwa kuelewa mbona wamekaa wiki nzima tangu muafaka utangazwe ndio wakaja kutoa tamko? something smell fishy here.....

Ngoja ninyamaze nisije pigwa BAN maana watu wanahasira sana.
Wee unashangaa wiki moja, sisi tunashindwa kuelewa siku 90 zilizotolewa na Nape. Siku 90 zinakwisha hizo, sijui mtawaambia nini watanzania.
 
Mbona nyie mmekaa miaka mitano na matatizo ya umeme tukisema mnasema wachochezi? nyaaaani haoni kunduleeeeeeeeee

Yutong heshima mkuu sie kina nani? mie sio tanesco wala sina chama chochote mkuu mie naangalia tu jinsi mnavyochezeshwa kwata na wanasiasa sio wa ccm wala wa cdm wote ni baba mmoja mama mmoja!
 
Nasubiri kwa hamu sana maoni ya watu humu, siku chache zilizopita baada ya muafaka kupitishwa wapo walio laani kitendo cha madiwani wale wa Chadema kufikia muafaka ule na CCM, hapo hapo very senior members in this forum walikuja juu kupinga hoja za wale wachache kwa nguvu zao zote wakisema kuwa hawapendi amani ya nchi hii, wametumwa, na maneno mengine mengi. Sasa kwa tamko la viongozi wetu wa juu wa Chadema, kauli waliyotoa ni sawia na kauli ya wale wachache waliokuja juu kupinga muafaka ule, sasa nasubiri kwa hamu kuona hawa very senior members of this forum ambao myself i appriciate they have very strong arguments watarudi na hoja zipi safari hii.
 
Sokomoko sikiliza chadema ni chama makini hakikurupuki lazima kichukue mda wiki hata mwezi ili wakusanye data,kwa hiyo hiyo ipo.
 
Mie nashindwa kuelewa mbona wamekaa wiki nzima tangu muafaka utangazwe ndio wakaja kutoa tamko? something smell fishy here.....

Ngoja ninyamaze nisije pigwa BAN maana watu wanahasira sana.
Walikuwa wanafanya utafiti yakinifu kujua mbivu na mbichi!!mbona magamba wanakaa siku 90 kutolea uamuzi jambo dogo?
 
Yutong heshima mkuu sie kina nani? mie sio tanesco wala sina chama chochote mkuu mie naangalia tu jinsi mnavyochezeshwa kwata na wanasiasa sio wa ccm wala wa cdm wote ni baba mmoja mama mmoja!
Mkuu SOKOMOKO kuwa wazi,onyesha hisia zako bila wasiwasi,sijawahi hata siku moja kuona posti yako hata moja inayokosoa CCM,au CCM haina mapungufu!!
 
Sokomoko sikiliza chadema ni chama makini hakikurupuki lazima kichukue mda wiki hata mwezi ili wakusanye data,kwa hiyo hiyo ipo.

Sokomoko ni CCM pure, halafu anajifanya hana chama anatuangalie tunavyo pelekeshwa na wasiasa wa CDM na CCM
unafiki mwingine bana haufai
 
Mie nashindwa kuelewa mbona wamekaa wiki nzima tangu muafaka utangazwe ndio wakaja kutoa tamko? something smell fishy here.....

Ngoja ninyamaze nisije pigwa BAN maana watu wanahasira sana.

Watu makini hawakurupuki na tuliokuwa wengi tulitilia mashaka mwafaka, na sasa ukweli unaanza kuja, niliona wale CCM B walivyokuwa wanachonga Bungeni sasa kitawashuka, maana Chadema wapo tayari kushindwa katika uchaguzi wa haki na democrasia ya kweli kuliko kugawana vyeo kama walivyofanya hawa madiwani.
 
Mbona wakisikia kuna kontena la karatasi za kupigia kura hawamakiniki wanaropoka hovyo?

kuna mambo mengine unatakiwa kufanya maamuzi ya haraka bila kuchelewa na mengine unatakiwa kufanya uchunguzi kwani muda unaruhusu.
 
Mie nashindwa kuelewa mbona wamekaa wiki nzima tangu muafaka utangazwe ndio wakaja kutoa tamko? something smell fishy here.....

Ngoja ninyamaze nisije pigwa BAN maana watu wanahasira sana.
mkuu ulitaka wakurupuke kutoa kauli bila uchunguzi, siwezi kukulaumu kwa sababu Watanzania bado tuna chembe chembe za yule katibu mkuu mstaafu wa chama kikongwe aliyekuwa akikurupuka katika kila jambo hadi kulazimishwa kujiuzulu/kustaafu.
 
Back
Top Bottom