CCM yahoji msimamo wa Chadema kuhusu ushoga

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutoa msimamo wao kuhusu ushoga hasa kutokana na urafiki uliopo baina ya chama hicho na Chama cha Conservative cha Uingereza kinachoongozwa na Waziri Mkuu, David Cameron.

Kauli hiyo ya CCM imetokana na kauli ya Cameron aliyoitoa hivi karibuni katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola uliofanyika Perth nchini Australia, akieleza kuwa Uingereza itasitisha misaada kwa nchi zisizotekeleza haki za binadamu ikiwemo yaki za ndoa ya jinsi moja.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Mnauye akizungumza na gazeti hili jana alisema kwa muda mrefu, Chadema imekuwa rafiki wa karibu wa chama cha Conservative, hivyo ni vyema ikafahamika msimamo wao ili wananchi na jamii ijue.

"Msimamo wa CCM haupingani na wa Serikali kwamba hatukubaliani na suala hilo kamwe, ila ndugu zetu hawa wa Chadema ni maswahiba zaidi wa Conservative, mwito wa CCM ni kuitaka Chadema itoe kauli yao waseme wanasimamia wapi katika hili, kama ujuavyo tabia za marafiki hufanana, ili Watanzania wajue wakiwapa dhamana itakuwaje katika hili," alisema Nape.

Lakini Chadema kwa upande wao, wameeleza kwamba msimamo wao ulishawekwa wazi na viongozi wa ngazi za juu akiwemo Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, John Mnyika kuwa hawakubaliani nalo na kamwe utamaduni wa kinyume cha maadili hawaukubali.

Mkurugenzi wa Sera na Utafiti, Waitara Mwikwabe, alikiri jana kwamba Chadema ina urafiki na Conservative na kueleza kuwa urafiki ni baina ya chama na chama na si Serikali na kwamba Cameron alizungumza kwa niaba ya Serikali ya Malkia Elizabeth II na si kwa niaba ya chama.

"CCM watofautishe mambo mawili, kuna kauli ya Serikali na chama, lakini pia waache unafiki, mbona mtoto wa Malkia (Prince Charles) alikuwa hapa nchini, amekuwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, amekunywa chai na Rais Jakaya Kikwete na misaada wamepokea, wala hajaja kusalimia Chadema? Hiyo ni Serikali na si chama," alisema Mwikwabe.

Miongoni mwa vyama vyenye nguvu nchini Uingereza ni Conservative, Liberal Democrats Party na Labour Party ambapo chama cha Labour ni rafiki zaidi wa CCM.

CHANZO.....GAZETI LA HABARI LEO
 
Slaa alishalitolea ufafanuzi jambo hilo kuwa Chadema haina muda wa kuanza kujadili sera za CCM.

quote_icon.png
By Dr.W.Slaa
wanaJF
nasikitishwa sana na utamaduni wa kujadili na kupoteza muda kwenye hoja zisizo na tija.
I. Taifa liko kwenye janga la umaskini, uchumi unazidi kuporomoka,shillingi yetu inapoteza thamani, watumishi wengi wa serikali hadi sasa hawajalipwa mishahara, oc haijatolewa na shughuli nyingi za serikali zimesimama. Hizi kwetu ni hoja nadhani hoja zingine zinapandikizwa ili ili watu wasahau Real Issues.
2. Ushoga uingereza si issue ya leo au jana.. Tunajua ilivyogawa Kanisa la Anglikana ambaye mkuu wake ni ni Malkia. Hili liliathiri hata hata Kanisa hilo hapa kwetu.wakati linaanza Cameroon wala wala Cons. Hawakuwa in power. Kuilink na Chadema ni upuuzi na kielelezo cha uvivu wa kufikiri na kutafiti.
3. Chadema ina utaratibu wake wa kutoa Tamko kwa mambo ambayo si sera yake.
4.kwamba ushoga kama ilivyo ufisadi unapingwa na Chadema haina mjadala.rejea. Rejea Kif.10 maadili viongozi na wanachama.
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutoa msimamo wao kuhusu ushoga hasa kutokana na urafiki uliopo baina ya chama hicho na Chama cha Conservative cha Uingereza kinachoongozwa na Waziri Mkuu, David Cameron.

Kauli hiyo ya CCM imetokana na kauli ya Cameron aliyoitoa hivi karibuni katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola uliofanyika Perth nchini Australia, akieleza kuwa Uingereza itasitisha misaada kwa nchi zisizotekeleza haki za binadamu ikiwemo yaki za ndoa ya jinsi moja.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Mnauye akizungumza na gazeti hili jana alisema kwa muda mrefu, Chadema imekuwa rafiki wa karibu wa chama cha Conservative, hivyo ni vyema ikafahamika msimamo wao ili wananchi na jamii ijue.
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutoa msimamo wao kuhusu ushoga hasa kutokana na urafiki uliopo baina ya chama hicho na Chama cha Conservative cha Uingereza kinachoongozwa na Waziri Mkuu, David Cameron. Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Mnauye akizungumza na gazeti hili jana alisema kwa muda mrefu, Chadema imekuwa rafiki wa karibu wa chama cha Conservative, hivyo ni vyema ikafahamika msimamo wao ili wananchi na jamii ijue.

“Msimamo wa CCM haupingani na wa Serikali kwamba hatukubaliani na suala hilo kamwe, ila ndugu zetu hawa wa Chadema ni maswahiba zaidi wa Conservative, mwito wa CCM ni kuitaka Chadema itoe kauli yao waseme wanasimamia wapi katika hili, kama ujuavyo tabia za marafiki hufanana, ili Watanzania wajue wakiwapa dhamana itakuwaje katika hili,” alisema Nape. Lakini Chadema kwa upande wao, wameeleza kwamba msimamo wao ulishawekwa wazi na viongozi wa ngazi za juu akiwemo Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, John Mnyika kuwa hawakubaliani nalo na kamwe utamaduni wa kinyume cha maadili hawaukubali.

Mkurugenzi wa Sera na Utafiti, Waitara Mwikwabe, alikiri jana kwamba Chadema ina urafiki na Conservative na kueleza kuwa urafiki ni baina ya chama na chama na si Serikali na kwamba Cameron alizungumza kwa niaba ya Serikali ya Malkia Elizabeth II na si kwa niaba ya chama. “CCM watofautishe mambo mawili, kuna kauli ya Serikali na chama, lakini pia waache unafiki, mbona mtoto wa Malkia (Prince Charles) alikuwa hapa nchini, amekuwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, amekunywa chai na Rais Jakaya Kikwete na misaada wamepokea, wala hajaja kusalimia Chadema? Hiyo ni Serikali na si chama,” alisema Mwikwabe.

Habarileo
 
Kama ni kweli Nape amezungumza haya basi natilia shaka uelewa wake! Yaani stori za irrational haters humu JF yeye anazipeleka ina a public square?
 
Ikiwa Nape kaongea haya shule yake haijamsaidia kitu na kweli NAPE atakuwa real VUVUZERA
 
Kuna matatizo makubwa ya taifa letu ambayo yanahitaji kutatuliwa ikiwa ni pamoja na serikali kufilisika, haya ya ushoga yapo miaka mingi tangu napata akili. Kuna baadhi ya watu wenye hulka ya wasichana kuozwa makikra wanaendekeza mahusiano kwa njia kinyume cha maumbile eti akiozwa aonekane bado bikra. Je, kuna tofauti gani na ushoga?
 
Suala la ushoga tayari llimeshafanywa propaganda za kisiasa tena? CCM bana.....!
 
Tatizo letu watanzania ni kutoelewa human rights. Hivi polisi akiwaona mashoga wawili wanapigana busu, atawakamata? Kwa sheria ipi?
 
C

Mkurugenzi wa Sera na Utafiti, Waitara Mwikwabe, alikiri jana kwamba Chadema ina urafiki na Conservative na kueleza kuwa urafiki ni baina ya chama na chama na si Serikali ............. waache unafiki, mbona mtoto wa Malkia (Prince Charles) alikuwa hapa nchini, amekuwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, amekunywa chai na Rais Jakaya Kikwete na misaada wamepokea, wala hajaja kusalimia Chadema? Hiyo ni Serikali na si chama,” alisema Mwikwabe.

Habarileo

What a response!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutoa msimamo wao kuhusu ushoga hasa kutokana na urafiki uliopo baina ya chama hicho na Chama cha Conservative cha Uingereza kinachoongozwa na Waziri Mkuu, David Cameron. Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Mnauye akizungumza na gazeti hili jana alisema kwa muda mrefu, Chadema imekuwa rafiki wa karibu wa chama cha Conservative, hivyo ni vyema ikafahamika msimamo wao ili wananchi na jamii ijue.

“Msimamo wa CCM haupingani na wa Serikali kwamba hatukubaliani na suala hilo kamwe, ila ndugu zetu hawa wa Chadema ni maswahiba zaidi wa Conservative, mwito wa CCM ni kuitaka Chadema itoe kauli yao waseme wanasimamia wapi katika hili, kama ujuavyo tabia za marafiki hufanana, ili Watanzania wajue wakiwapa dhamana itakuwaje katika hili,” alisema Nape. Lakini Chadema kwa upande wao, wameeleza kwamba msimamo wao ulishawekwa wazi na viongozi wa ngazi za juu akiwemo Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, John Mnyika kuwa hawakubaliani nalo na kamwe utamaduni wa kinyume cha maadili hawaukubali.

Mkurugenzi wa Sera na Utafiti, Waitara Mwikwabe, alikiri jana kwamba Chadema ina urafiki na Conservative na kueleza kuwa urafiki ni baina ya chama na chama na si Serikali na kwamba Cameron alizungumza kwa niaba ya Serikali ya Malkia Elizabeth II na si kwa niaba ya chama. “CCM watofautishe mambo mawili, kuna kauli ya Serikali na chama, lakini pia waache unafiki, mbona mtoto wa Malkia (Prince Charles) alikuwa hapa nchini, amekuwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, amekunywa chai na Rais Jakaya Kikwete na misaada wamepokea, wala hajaja kusalimia Chadema? Hiyo ni Serikali na si chama,” alisema Mwikwabe.

Habarileo

nani alikuwaambia kuana msimamo wa kichama kwenye suala la taifa huyo nape anatumia masaburi kuwaza wanasimamia mambo ya nje ni serikali ya tanzania inayoongozwa kwa sera za ccm sasa leo chadema watoe msimamo wasitoe inawasaidia nini haswa kwani wanaacha ya msingi polisi kutunyima haki ya kuandamana nchi nzima kwani magogoni kusingekalika wanakuja na ushoga waulize historia haya mambo enzi za mwalimu wasingeongea haya katika jumuiya ya madola ambayo tanzania ni mwanachama wangekaa kimya nakumbuka mwalimu alwawahi pewa mkono wa malkiia ukiwa na gloves akataka kumsalimu naye akamjibu kwa kumpatia kifimbo ikabidi malkie avue gloves kwanza sasa na hawa nawashauri waipe chadema uhuru wa kufanya mikutano na maandamano

nawasilisha nape acha kutumia masaburi tumia katiba na sera zenu kujenga hoja
 
Kuna thread nimesoma humu JF kwamba CHADEMA itoe msimamo kuhusu ushoga kwa vile inauhusiano wa karibu na chama cha conservative UK. Sijaona kiongozi yeyote wa CHADEMA akikubali au kukataa kwamba ni kweli wanauhusiano wa karibu na chama hiki. Ningependa kufahamu kama kauli hii ni ya kweli.

Kwa maoni yangu hawa Conservative party wameshiriki kwa kiasi kikubwa kufanya maisha ya wananchi wa UK kuwa magumu kupita kiasi na wanasera nyingi za kibaguzi hasa kwa watu weusi wakitaka kuwadhibiti wasifanye kazi nchini UK na hata kulimit idadi ya wanaoingia UK. Watu wengi wamepoteza ajira kutokana na sera za chama hiki na ningependa kujua kama kweli CHADEMA inakisupport chama hiki na sera zake.

Dk. Slaa au kiongozi mwingine wa CHADEMA ningependa kujua maoni yenu.
 
Kuna matatizo makubwa ya taifa letu ambayo yanahitaji kutatuliwa ikiwa ni pamoja na serikali kufilisika, haya ya ushoga yapo miaka mingi tangu napata akili. Kuna baadhi ya watu wenye hulka ya wasichana kuozwa makikra wanaendekeza mahusiano kwa njia kinyume cha maumbile eti akiozwa aonekane bado bikra. Je, kuna tofauti gani na ushoga?

Wewe unahoji hivyo lakini mimi nashangazwa sana jinsi waafrika tulivyo wanafiki. Na kimsingi ukiona community fulani wanakuwa too much homophobic kama ilivyo hapa kwetu ujue commnunity hiyo imejaa ushoga na kelele zetu ni kuficha hiyo syndromme. Mfano mwingine ni kule uarabuni ambapo mashoga wanapigwa mawe lakini la kushangaza mashoga wengi na wateja wao ni jamii ya kiarabu. Sasa kelele zote za nini? Kwanini ushoga linafanywa jambo la kisiasa? Kwa nini jamii yetu lisishughulikie suala la ushoga pasipo dharau, matusi na unyanyapao unajidhihirisha kupitia kauli za wanasiasa, watu wa dini na kwa mshangao wangu hata hapa JF?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
wakati zanzibar inapinga ushoga kumbe ktk tz ndiyo wanaoongoza. mabinti zao wanagawa nyuma kama hawana aikili nzuri eti kulinda bikira zao. what a shame
 
CHADEMA wanaweza kuwa na urafiki na Conservative party lakini Nape akumbuke Serikali ya ccm ina urafiki na imekuwa inapokea PESA zinzotolewa na serikali inayoongozwa na Conservative party. Hii spinning anayoleta hapa ni ya viwango vya chini sana.

Kuonesha ni jinsi gani Nape anaendesha siasa za kinafiki soma hii sentensi "...kama ujuavyo tabia za marafiki hufanana, ili Watanzania wajue wakiwapa dhamana itakuwaje katika hili,” alisema Nape. Hapa Nape anataka umma wa Tanzania uamini kuwa CHADEMA wanakubaliana na hoja ya kutambua kisheria ushoja kwa sababu ni marafiki na Conservative Party! Kama hii theory iko sahihi basi serikali ya ccm nayo itakuwa hatiani maana wamekuwa wanalishwa na kuvishwa na serikali ya Uingereza inayoongozwa na Conservative Party! Na akumbuke UK ndio biggest contributor kwenye bajeti ya serikali, (approx 30%). Hizi ni hela za walipa kodi wa Uiengereza wakiwemo mashoga!

Pamoja na crying wolf' za Membe kususia misaada ya Uingereza tumeshughudia mtoto wa malkia akila bata na rais wetu, na leo waingereza wa Songas walienda Ikulu kumjulia hali rais wetu. Kwa kifupi message ninayopata toka kwa Nape ni kwamba ccm na serikali yake hawana uwezo wa kufikiri wala hawajui wafanye nini hivyo wanaishi kwa kuiga (copy & paste) anayofanya rafiki yao e.g. Gadhafi alisema rats, Zuberi naye kasema rats! Mufilisi wa fikra!
 
Mwana malikia mama yake ndio anae abudiwa na serikali ya Uingereza, serikali hiyohiyo ndio inataka ushoga utambuliwe ili misaada izidi kumiminika. Mtoto wa malkia huyohuyo ameandaliwa dhifa ikulu tena akaonekana akimsabahi mtoto wa mkulu huku mkulu akitabasamu. Yaani akitabasamu mtoto wake kusalimiana na mtoto wa malkia kutoka kwenye serikali inayotaka ushoga uhalalishwe, inawezekana tamko nila Membe lakini Ikulu iko 50-50.

Nape anatakiwa kushinikiza ikulu kutoa maelezo kwa nini imetumia mamilion ya shilingi kuandaa dhifa ya mtu ambae serikali yake inataka ushoga uingie kisheria kwenye nchi yetu. Aache kutafuta pakutokea kwa kuishtumu chadema maana serikali hiyohiyo imeshindwa kuundoa ushoga.
 
Back
Top Bottom