CCM yahofia kupinduliwa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
na Salehe Mohamed na Danson Kaijage

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema kina hofu ya kupinduliwa madarakani na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinachoratibu na kufanya maandamano kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.

Wakati Chama hicho kikihofia maandamano ya Chadema, Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe (CCM), alisema maandamano ni miongoni mwa njia za kuwafanya watendaji wazembe wa serikali kuwajibika.


Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) (Uchumi na Fedha Taifa) wa CCM, Mwingulu Nchemba, amevitaka vyombo vya dola kuingilia kati maandamano yanayofanywa na Chadema kwa madai kuwa yanalenga kufanya mapinduzi ya serikali iliyopo madarakani.

Nchemba, alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa, ambapo alisema viongozi wa Chadema wana ajenda ya kufanya mageuzi kwa nguvu na kulifanya taifa lisitawalike.

Alisema viongozi wa chama hicho wamekuwa na kauli mbalimbali za uchochezi ikiwa ni pamoja na kutoa ushawishi kwa jeshi la polisi ili wasiweze kukubali amri za viongozi wao jambo ambalo alidai kuwa ni hatari kwa taifa.

"Mimi sikatai maandamano ni haki ya kila mtu lakini ninachosema ni kuwa na meno ya viongozi na ushawishi wa viongozi hao ni ya uchochezi na yanaashiria kupinga uongozi ulio madarakani," alisema Nchemba.

Alisema maandamano ya Chadema yamezidi maandamano ya vyama vingine duniani kwani wanapofanya maandamano wamekuwa na maneno yanalenga kuwahamasisha wananchi kufanya maandamano yanayoweza kuleta mageuzi kama vile, Misri, Libya na nchi nyingine ambazo zina machafuko na wananchi wanavutiwa zaidi na habari hizo.

Wakati CCM, ikihofu kupinduliwa, jana asubuhi katika kipindi cha Tuongee, kinachorushwa na televisheni ya Star Tv, mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe (CCM), alisema hata yeye angeingia mitaani kuhamasisha wananchi wa Ludewa kuandamana kama serikali isingeongeza fedha katika Wizara ya Uchukuzi.

Alisema serikali ina watendaji wazembe ambao wakati mwingine wamekuwa wakikwamisha shughuli za maendeleo hivyo wananchi wanapoamua kufanya maandamano huwaamsha katika usingizi.

"Juzi nilisema kuwa nitawahamasisha wananchi wangu kuandamana kama wanavyofanya Chadema kama shirika la meli lisingepatiwa fedha za kutosha mbazo zitatuwezesha watu wa Ludewa kupata meli mpya au kukarabati zile zilizopo," alisema.

Alibainisha kuwa hakuna sababu ya serikali kuogopa maandamano kama ingekuwa inatimiza wajibu wake wa kutimiza mahitaji ya wananchi lakini imekuwa ikihofia maandamano kwa sababu ya uzembe ulioko serikalini.

Filikunjombe pia alitetea kauli yake kuwa mawaziri na watendaji wazembe wanyongwe ili kujenga taifa lenye uwajibikaji hasa kwa watendaji wanaopewa kusimamia rasilimali za taifa.

"Adhabu ya kunyongwa si mpya hapa nchini, nilichokitaka mimi ni adhabu hiyo itolewe kwa mawaziri na watendaji wazembe na wabadhirifu, hakuna kigeni hapo," alisema.

Wiki mbili zilizopita Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde, (CCM), alisema watendaji wa serikali na chama chake ndiyo wanaopaswa kulaumiwa kwa kusababisha maisha magumu kwa wananchi badala ya kukilaumu Chadema.

Lusinde alisema kama CCM ingeboresha maisha ya wananchi kamwe wasingekubali ushawishi wa Chadema ambayo imekuwa ikifanya maandamano kupinga ugumu wa maisha, kupanda kwa gharama za umeme na mgawo unaoendelea hivi sasa.
 
I said this once and I'll say it again "CCM is a party in denial", hawaelewi, hawajielewi. Ni kama mgonjwa anaeumwa lakini hajui anachoumwa wala tiba yake.
 


Alisema maandamano ya Chadema yamezidi maandamano ya vyama vingine duniani kwani wanapofanya maandamano wamekuwa na maneno yanalenga kuwahamasisha wananchi kufanya maandamano yanayoweza kuleta mageuzi kama vile, Misri, Libya na nchi nyingine ambazo zina machafuko na wananchi wanavutiwa zaidi na habari hizo.

ukweli umechanganywa na uongo, na hoja gongana kwenye bold
misri hakuna machafuko kuna mapinduzi ya nguvu ya umma na aliyekuwa raisi yuko rumande
huyu anayewaongelea wamisri walioamua kukomboa nchi yao ni nani?

neno machafuko limetumika hapa kama uchochezi mbaya zidi ya CHADEMA lakini mwisho kwa nini wananchi
wana penda habari hizi

ina maana anashindwa kuelewa serikali lazima iwe na ushawishi na kama haina ushawishi imekufa na haifai

mimi nadhani siku moja kuwe na mdahalo kuhusu neno uchochezi naona linatumika vibaya kwa manufaa ya kisiasa
nilipokuwa mdogo baba yangu ALINICHOCHEA (uchochezi) ni na bidii ya shule maana elimu ni ufunguo wa maisha na walimu walifanya
hivyo pia
swali je uchochezi ni tatizo?
au tatizo ni serikali kukumbatia wezi na wala rushwa?
viongozi wa serikali/mashirika/taasisi za umma wanang'oa misingi ya umoja wetu kwa visingizio ni uchochezi
 
Bravo mwana JFs Tukuyu
naam ni kweli wameshikwa pabaya na wamepatikana hata pa kupumulia au kujigeuza hakuna!
 
Sasa kama hawana utendaji mzuri kwa wananchi na wananchi wanajua hilo kwa nini wasiwe na wasiwasi?acheni visingizio ninyi magamba na mlete maendeleo kwani ninyi ndiyo serikali iliyoko madarakani.acheni mambo ya kitoto
 
Haya maandamano ya operation sangara yatakuja lini dar? Tunataka tumshangaze kikwete kwani watumishi wa uma wote ambao sio mafisadi tutakua tunaandamana bega kwa bega.
 
Back
Top Bottom