makoye2009
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,638
- 1,218
Mimi nasema hivi kama CCM wamechoka na amani,utulivu na mshikamano wa nchi yetu tanzania wafanye haraka hicho kitendo cha kuwaondoa wabunge wachadema kwa azimio la bunge hiyo februari 8,2011. Nawahakikishia ccm kuwa kama hawajaona nchi inawaka moto basi ni wakti huo.ccm watajuta kwa huo upuuzi wao wanaotaka kuufanya. Wajaribu waone. Watanzania sasa hivi tumebadilika. Hatutakubali wabunge wetu waondolewa bungeni.
hayo maandamano ya watu milioni 14+ zidi ya milioni 5 wa ccm sijui kama kutakuwa na vifaru/risasi vya kuyazuia!!!
ccm tunataka mabadiliko ya katiba na si vitisho.
- tunachotaka ccm kwa sasa ni kuanza mchakato wa taratibu za kuunda katiba mpya ili kuondoa sheria ya kutopinga matokeo ya urais baada ya kutangazwa na tume ya uchaguzi. Sheria ambayo ni ya kidikteta! Kwanini matokeo ya ubunge na udiwani tu ndiyo yahojiwe na ya rais yasihojiwe wakati wapiga kura ni walewale????????????
- tunachotaka kuwe na tume huru ya uchaguzi ambayo mwenyekiti na mkurugenzi wake hawateuliwi na rais aliyeko madarakani. Hili ccm wanajua kabisa haliko sawa.
hayo maandamano ya watu milioni 14+ zidi ya milioni 5 wa ccm sijui kama kutakuwa na vifaru/risasi vya kuyazuia!!!
ccm tunataka mabadiliko ya katiba na si vitisho.