CCM yafuta kitengo cha Propaganda, Tambwe Hizza kwaheri

Nape ndio anatakiwa awe ofisa habari badala ya katibu mwenezi, Hili neno mwenezi limeshapitwa na wakati, hili lilikuwa na maana enzi za telegram. hapa wachague jina sahihi watakalopenda kutumia either PR au Ofisa habari, kitengo hichi hakiwezi kuwa na watu wote hawa wawili. BIG NO.

Mkuu sasa hapa tena itakuwaje? Mimi nimezoea kuona hawa PRs au Ofisa Habari huwa ni watu wenye weledi juu ya mambo ya uandishi wa habari ama kwa kifupi wanakuwa wamesomea uandishi wa habari (Professionals). Sasa huyu Ndg. yetu Nape Mozes Nnauye ana weledi wa uandishi wa habari kweli?
 
Nakubaliana na wewe Mkuu na niseme hawa ccm waishukuru JF na waendelee kusoma hoja zenye mashiko maana kuwa na kitu kinaitwa KITENGO CHA PROPAGANDA inabidi uwe na kichwa cha mwendawazimu hivi, but again ccm sio wazima vichwani are they?

Kwani ile meza yake (Hizza Tambwe) ya kuuzia mitumba pale sokoni Tandika alishaiuza?
 
Mkuu sasa hapa tena itakuwaje? Mimi nimezoea kuona hawa PRs au Ofisa Habari huwa ni watu wenye weledi juu ya mambo ya uandishi wa habari ama kwa kifupi wanakuwa wamesomea uandishi wa habari (Professionals). Sasa huyu Ndg. yetu Nape Mozes Nnauye ana weledi wa uandishi wa habari kweli?
Hao ndio magamba bwana ukisikia wengine ni wa kuchonga, wewe unashangaa hilo kwa nini usishangae la kamati kuu kulalamikia bei ya mafuta ya taa, wakati mwenyekiti wa kamati kuu ni Rais na mwenyekiti wa baraza la mawaziri ni Rais huyo huyo, hauwoni kama haya ndio maajabu zaidi?
 
Hii mwake mwake sanaaa huyu jamaa namwombea njaa kali hadi ajute,mtu yeyote msaliti,ndumila kuwili hafai,tambwe aliwahi kusema tena kwenye mkutano wa hadhara kuwa kuliko kurudi ccm bora kulala na mama yake.akala matapishi yake akidhani kwenda ccm kutamwondolea njaa aliyonayo.hayawi hayawi sasa yamekuwa,kitengo hichooooo! KIMEONDOKA.Atajijua arudi tanga tu akalime machungwa.
 
Mkuu hii Public Relations na Katibu Mwenezi itakuwaje hakutakuwa na mgongano?

Nadhani zina kuwa ofisi moja kama wana akili timamu!

Ila tatizo lililo hapa ni yale yale matatizo ya CCM ya siku zote, Makundi ya Kampeni basi, naona kama hii dhambi tayari imeimaliza CCM kabisa sidhani kama itakuja kusimama tena labda kwa kumwaga damu ya Watanzania.

Maana hapa ni kundi fulani lina lipa kisasi kwa kikundi kingine, nadhani wanachotaka kufanya hapa ni ule mtindo wa sasa zamu yetu kula!!
 
Hatimaye ccm imekifuta rasmi kitengo cha propaganda na kubuni kitengo kipya ambacho kitajulikana kama kitengo cha mawasiliano ya Umma. ( Public Relation ) taarifa hii ni kwa mujibu wa ofisa habari wa CCM leo kwa waandishi wa Habari, hii maana yake ni kwamba Tambwe Hiza sasa atafute shughuli ya kuganga njaa kwani wapo vija na wenye elimu nzuri ndani ya CCM wanaostahili kupewa nafasi hii ya PR.

My Take: Pamoja sikubaliani na CCM kwa mambo mengi lakini kwenye hili nawapa hongera maana hakuna mtu aliekuwa anakerwa na neno propaganda kama mimi, na ninaamini Nape ametoa mchango mkubwa kufikiwa uamuzi huu, maana niliwahi kumshauri hapa hapa JF kwamba aongee na magamba wenzake wafute hicho kitengo.

HAKUNA KITU HAPO Ngozi ya kondo kumbe ndani mbwa mwitu mkali zi Yaani na Maanisaha hapo ni kama kubadilisha jina la club ya michezo ya KUNGFU...Badala ya Kuita ""KUNGFU SPORT CLUB'' unaamua kuita ""KARATE SPORT CLUB"" Sasa hapo ni nini kimebadilika kama si jina tu!!!
 
Hii mwake mwake sanaaa huyu jamaa namwombea njaa kali hadi ajute,mtu yeyote msaliti,ndumila kuwili hafai,tambwe aliwahi kusema tena kwenye mkutano wa hadhara kuwa kuliko kurudi ccm bora kulala na mama yake.akala matapishi yake akidhani kwenda ccm kutamwondolea njaa aliyonayo.hayawi hayawi sasa yamekuwa,kitengo hichooooo! KIMEONDOKA.Atajijua arudi tanga tu akalime machungwa.

Mkuu umeona Mopaozi alichokisema hapo juu? Usije ukashangaa Tambwe akapewa Wilaya!! Kumbuka Danny Makangha, Mtemvu, Nsanzugwanko, Lamwai, Kaburu, Tyson, n.k. CCM na Serikali yake huwa ni vitu visivyotabirika.
 
Hao ndio magamba bwana ukisikia wengine ni wa kuchonga, wewe unashangaa hilo kwa nini usishangae la kamati kuu kulalamikia bei ya mafuta ya taa, wakati mwenyekiti wa kamati kuu ni Rais na mwenyekiti wa baraza la mawaziri ni Rais huyo huyo, hauwoni kama haya ndio maajabu zaidi?

Mkuu unajua usanii umejaa sana ndani ya CCM. Na kuhusu suala hilo mimi naona wale wenye ajenda ya kutenganisha kofia mbili ndio wamelipeleka CC suala la mafuta ya taa ili ionekane ni vyema sasa kutenganisha kofia ya Rais na Mwenyekiti wa Chama ili Chama kiisimamie vyema serikali!! CCM nao wameingia mtegoni kwani hapa CC imeonekana kupingana na serikali kwa maana hiyo wamemuweka pabaya Rais. Yaani akiwa anaongoza baraza la mawaziri anabariki bei ya mafuta ya taa ipande akirudi kuongoza kikao cha CC anakemea kupanda kwa bei ya mafuta ya taa. Sijui inawezekanaje hapa. Kwa hiyo wale wenye ajenda yao watakuja na ajenda ya kutenganisha kofia wakitumia mfano wa maamuzi juu ya kupanda kwa bei ya mafuta ya taa!
 
My Take: Pamoja sikubaliani na CCM kwa mambo mengi lakini kwenye hili nawapa hongera maana hakuna mtu aliekuwa anakerwa na neno propaganda kama mimi, na ninaamini Nape ametoa mchango mkubwa kufikiwa uamuzi huu, maana niliwahi kumshauri hapa hapa JF kwamba aongee na magamba wenzake wafute hicho kitengo.

Nondoo ni kwamba hiyo presentation juu ya reforms ndani ya Sekretarieti ikigusa timu mpya za PR na political strategy iliandaliwa na kuwasilishwa na January Makamba...
 
Inaandaliwaje na Januari wakati iko chini ya IDARA ya Uenezi AMBAYO mkuu wake NI Nape? Nilichosikia January ALIKUWA na yake nayo ilikwenda SHULE kuliko ya Nepi
 
TABWE hiza na Nape baba mmoja. Hili linaweza kuthibitishwa na hatua ya Nape ya kutomfahamu baba yake halsii.
 
Nikipigika sana "nitahamia ccm" kwa kuwa mwisho wa siku kuna tuzo ya ukuu wa nkoa au nkuu wa wilaya.!
 
labda wamuanzishie kitengo cha kupiga majungu ndio kinaweza kufit! maana watampeleka wapi huyu std seven!
 
Wana Jf,
Kusema ukweli nimemmisi sana aliyekuwa Mkurugenzi wa Propaganda CCM ndugu Tambwe Hiza. Hivi siku hizi yuko wapi? je kile kitengo cha Propaganda-CCM bado kipo? Na kama kipo, je nani anakiongoza kwasasa? Lakini ndugu Tambwe yuko wapi? kwani kwa hakika alikuwa wa maana sana katika kipindi cha Uchaguzi ndani ya CCM na kwasasa yuko wapi? NAPE UPO?????????
 
Back
Top Bottom