CCM yafika pabaya: Dk. Kigwangala, Bashe watishiana bastola Nzega!

Nilitamani kichwa cha habari kiwe ''TABORA SASA SILAHA NJE NJE''.kisha kiendelee ''BAADA YA RAGE SASA BASHE NA KIGWANGALA''.

Katika sakata hili, polisi wamekaa kimya kabisa, kama vile hawajui kitu !!
Baadaye watasema "...wahusika hao walikutana kwa bahati mbaya ofisini wakirudisha fomu, huku kila mmoja akiwa amesahau kuwa alikuwa amebeba bastola kiunoni..."
 
Huko CCM hizo bastola wanapewa bure? Rage aiitoa hadharani kwenye kampeni Igunga. Hawa nao wanatishiana na polisi wanawaangalia tu.

Another Silly movie

Kesho na kesho-kutwa utasikia polisi wakisema kuwa wawili hao wametozwa faini ya Tsh. elfu tano kwa 'kosa' la kuning'iniza bastola kiunoni wakati wa kurudisha fomu za kugombea ujumbe wa nec !!.
 
Are we really dealing with two grown ups or they are just kids who look like adults?
 
Nimewasikia wote kwa kauli zao, ila kwa msukumo wa fikra huru namsaport Bashe. Dr analialia tu hana ubavu kwa Bashe, hata ubunge si alipewa tu?
 
Kuna jamaa humu wanajaribu sana kupotosha mjadala wa hoja ya wana-ccm kutishiana kwa silaha za moto.
Wanajaribu sana kuupeleka mjadala huu uwe wa kujadili 'bastola' na 'bunduki'.

Upotoshaji huu unatumiwa sana na ccm. Ni kama vile kutokee tukio la mwizi aliyeiba pesa nyingi, halafu watu wakawa wanamkimbiza ili wamkamate. Hapo mwizi atatumia upotoshaji kwa kurusha mabunda ya pesa ili watu wanaomkimbiza waokote pesa badala ya kumkimbiza mwizi mwenyewe.

Lakini naona wachangiaji wengi wamepuuza upotoshaji wao, na wanaendelea kujadili hoja ya msingi.
 
Katika kile kilichoripotiwa hapa jf kwamba dr kigwangalla amtishia Bashe bastola si kweli bali bashe ndo aliye mtishia dr kigwangalla bastora, mods jf inachafuka Kwa wakurupukaji et jf imehongwa na bashe iripoti hivyo. Pia dr kigwangalla amesema siasa za chama cha mapinduzi zinakipeleka chama kubaya.

MDOS, Huu uzi umetolewa kwenye gazeti la Tanzania Daima la leo. Kama ni upotoshaji, tujadili namna vyombo vya habari vinavyopotosha umma, na si msomaji. Mimi nimesoma gazeti hilo la leo hii na ndio maana nimetoa post, sikutoa kichwani. Hao wanaoilalamikia hii post nadhani wangesoma souce ya habari yenyewe. Tutendeane haki:
 
Nimewasikia wote kwa kauli zao, ila kwa msukumo wa fikra huru namsaport Bashe. Dr analialia tu hana ubavu kwa Bashe, hata ubunge si alipewa tu?

Hivi pamoja na yote hayo swali kubwa ni je wanagombania kumtumikia mwananchi nchini mwetu au wanagombania maslahi binafsi? Na haswa ambaye alishashukiwa na chama chake mwenyewe kuwa si mtanzania?
 
yes, ccm ni chama kinachodumisha amani na mshikamano kasoro wachaga tu ndiyo wanawachukia...hehehehehe
 
Hivi ni kuutaka tu ujumbe wa NEC au kuna la ziada? Kwa sasa wote fomu zao ziwekwe pembeni kisha wajadiliwe wanachogombea nini na kina maslahi gani kwa Chama na Taifa kwa ujumla.
 
Halafu Gombe anadai CDM kufutwa kwa kusababisha vurugu. Wanaokutwa na mabastola, masmg, mapanga, sime ni wafuasi na viongozi wa CCM, ila uvunjifu wa amani CDM. Mungu ni wa ajabu kweli, badala ya kuwawekea ubingo hawa jamaa wa mabwepande, kawajaza kamasi tupu.
 
Kwani 2015 ishafika? Mbona wanaanza mapema hivi. Hivi hiki chama hakina mwenyekiti? Atoe tamko basi.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Hivi ni kuutaka tu ujumbe wa NEC au kuna la ziada? Kwa sasa wote fomu zao ziwekwe pembeni kisha wajadiliwe wanachogombea nini na kina maslahi gani kwa Chama na Taifa kwa ujumla.

Tusubiri Nape aje kutoa ufafanuzi hapa. Au naye atasema "...ccm makao makuu haijapokea taarifa yoyote kuhusu sakata hilo, wanalisikia tu kwenye vyombo vya habari..."
 
Nimewasikia wote kwa kauli zao, ila kwa msukumo wa fikra huru namsaport Bashe. Dr analialia tu hana ubavu kwa Bashe, hata ubunge si alipewa tu?[/QUOTE]

Unamsapoti kwa kuingia mtego wa kijinga vile? sasa elewa kuwa hapo ndio mwisho wa mchezo kwani tayari vingunge visivyomtaka Lowassa/Rostam vimepata sababu ya kumtoa huyo Bashe wako nje ya ulingo moja kwa moja na mpaka angojee uchaguzi wa 2015 ambao pia atauona kama mazingaombwe vile, taabu ya Bashe na Kigwangala wote akili zao kama punda, Binaadamu hawezi kumzuia punda anapotaka kutenda mambo yake binafsi kama kujaamiana lakini punda huyo huyo kamwe hawezi kataa kubebeshwa zigo la binaadamu hata liwe zito kiasi gani,...Namshangaa Bashe pamoja na kulielewa hilo la mabwana zake kunuka na kutokutakiwa yeye bado kang'ang'ana nao utafikiri walizaliwa pamoja,

Mechi hii mie naona Kigwangalla kashinda kwa kumuingiza mjini Bashe na yeye Dr kamaliza kazi aliyotumwa kiulaini kabisa
 
GreatThinkers...imesemwa mara kadhaa kuwa bila CCM imara Tanzania itayumba. Hapa tulipo nchi sio tu imeyumba, bali imepasuliwa vipande vipande. Huyu Dkt Kigwangala na Bw Bw Bashe wamekosa wa kuwaonesha bastola, hivyo wameamua kuoneshana wao kwa wao. Hii CCM dhoofu bin hali ife kabisa ili kunusuru Tanzania na watu wake.
 
Vijana wa Tz!!! Ujana bila maadili na makuzi mema sio suluhisho la matatizo ya uongozi wa nchi hii.

Just look at these spoilt brats and the likes of Zitto, January, Nape, Mtatiro et al.....can someone see any hint of light there?

As for me it really leave much to be desired for.
 

“Inashangaza kuona kugombea NEC tu watu wanataka kuuana, wanakimbilia nini huko ndani?” alihoji Mwenyekiti Taifa wa CCM.


“Ina maana watu hawa wanaonyesha dhahiri kuwa HAWANA NIA NJEMA NA CHAMA , bali wanaingia kwa maslahi yao binafsi, hivyo tuna kila sababu ya kuwakataa ili tujenge timu ya ushindi ambayo ndiyo nia yetu,” aliongeza mwenyekiti huyo.



NI NANI HAO WALIOTAKA KUUNA KWA JILI YA KUINGIA NEC?

Ni Bashe na Kigwangala. Refer to this below link

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wangala-bashe-watishiana-bastola-nzega-5.html

MY TAKE

Hekima na fikra za Mwenyekiti zidumu, Hakina hapa amecheza kama PELE na amekaba kama VIDIC...Hawa Watu Wawili Hawafai Kabisa Kwani Uchu Wao Madaraka Hauelezeki....Bashe na Kigwangala Tupa Huko.
 

“Inashangaza kuona kugombea NEC tu watu wanataka kuuana, wanakimbilia nini huko ndani?” alihoji Mwenyekiti Taifa wa CCM.


“Ina maana watu hawa wanaonyesha dhahiri kuwa HAWANA NIA NJEMA NA CHAMA , bali wanaingia kwa maslahi yao binafsi, hivyo tuna kila sababu ya kuwakataa ili tujenge timu ya ushindi ambayo ndiyo nia yetu,” aliongeza mwenyekiti huyo.



NI NANI HAO WALIOTAKA KUUNA KWA JILI YA KUINGIA NEC?

Ni Bashe na Kigwangala. Refer to this below link

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wangala-bashe-watishiana-bastola-nzega-5.html

MY TAKE

Hekima na fikra za Mwenyekiti zidumu, Hakina hapa amecheza kama PELE na amekaba kama VIDIC...Hawa Watu Wawili Hawafai Kabisa Kwani Uchu Wao Madaraka Hauelezeki....Bashe na Kigwangala Tupa Huko.

"Baniani mbaya Kiatu chake Dawa"
Maamuzi kama haya yanayoitwa Busara huwa yanafanyika pale ambapo uwezo wa kutafuta ukweli unapokwama au watu wanapotafuta njia za mkato za kutatua tatizo fulani.Hapa kuna Pande mbili zinakinzana,kuna mmoja aliyetenda kosa, na kuna aliyeonewa.Ukiwaondoa wote unakuwa umesolve tatizo permanetly lakini kuna mtu anayekuwa ameonewa kwa kunyimwa haki yake kwa kosa la mwingine.Na haya maamuzi yametatua tatizo kisiasa tu,je kijamii hawa watu itakuaje?Kuna tatizo naona limetengenezwa.Hawa watu watakuja umizana huko mbele ya safari.
 
Back
Top Bottom