CCM yafanya maamuzi mazito Kamati Kuu?

Mkuu wewe endelea kujidanganya unajua tu.

Mkuu Kakulwa,

Please naomba uache hizi, maana sasa hivi utaambiwa unaniogopa, na unaniabudu, na kwamba mimi ni Mungu, We do not need that, tafadhali naomba muache jamaa, tuendelee na kuhabarishana,

Kwa sasa nimechoka sana, naingia kulala lakini soon in three hours nitakwua na more uptodates dataz.

Let it go kusudi mjadala usifungwe ndio nia ya jamaa, maana ana hasira topic yake kufungwa ile ya kudai eti forum ianze kufuta topic za pororjo, wewe hujaiona kule members only eti yeye ana yuwezow a kujua topic mbpovu na nzuri kwa taifa, kwahiyo mkuu tuwe na busara, tusije tukageuka mawe na ku-lose the focus, Nitakupenyezea soon the dataz.

Mkuu Kakulwa Ubarikiwe, maana wewe ni mmoja wa wachahce wenye sura moja tu, sio kama wenzangu wengi wenye sura mbili.
 
Mzee FMES,
Yaani hapa nimesimama mbele ya laptop yangu na nguo zangu za kiraia na nimekukung'utia SALUTE moja saaaaaafi.Ningekua na magwanda ningeingia humu kwenye laptop na kupiga salute mikono miwili.Jamani kuna yule ambae huwa anahoji mi-dataz yako na kukubeza.Yaani mzee unatoa mi dataz iliyo ya moto kabisa.Hapa mkuu mimi sina neno
ILA tu
CCM
Mtamkumbuka Mangula SANA.

Keep the focus brother, tupo ukurasa mmoja soon nitakwua na more naomba kulala kidogo maana a long day leo, soon nitarudi na more, wazee wote kwenye e-mail msiwe na hofu zinakuja, nipeni time kidogo!

FMES Wazee Wa Sauti Ya Umeme!
 
Habari za ndani ya kikao cha CC nilizozipata sasa hivi ni kwamba, kamati kuu ya CCM iameamua kuwafuta wagombea wote wa UV-CCM kutoka Bara, na kuamua kuwachukuwa wagombea watatu toka Zanzibar tu kugombea kiinyanga'nyiro hicho.......... stay tuned kwa more dataz!

We will beright backkkkk! Ooh I love it! JF Where We Dare!

habari njema.

isije ikawa ni moja ya zana zinazotumika
kutusahaulisha mambo nyeti yanayolikabili taifa letu hivi sasa.

Ajiuzulu mapema and we hope huyo atakaye mreplace is far much better than him na siyo mtu wa porojo ila kwa CCM you can always expect nothing!

Kikwete, Msekwa na Makamba wote wajiuzulu Mwenyekiti wa Muda Warioba, Makamu Mwenyekiti Mwakyembe na Katibu Mkuu FMES :)

Umemsahau Anna Malecela,Dr Salim Ahmed Salim and Obviously Mimi kwenye allocation of those strategic seats!

Lakini huku kuwafuta wagombea wote toka Bara na kuwaacha wa visiwani tu si upendeleo ulio dhahiri? Kwani wagombea wote wa kutoka bara walihusika na utoaji rushwa ili kupata nafasi hiyo? Kwa nini uchaguzi usiahirishwe hata kwa miezi miwili ili kuwapa nafasi wagombea wa Bara kuomba upya nafasi hiyo? Kuna jambo kubwa lililojificha hapa.

Demokrasi imepigwa kikumbo kwa mara nyingine tena. Hivi hiki chama hakika kanuni kinaongozwa kwa hisia.

Hakuna kanuni wala demokrasi ndani ya CCM. Kama ingekuwepo basi Mgombea wa Urais toka CCM 2005 asingekuwa Kikwete, Makamba asingekuwa Katibu Mkuu wa CCM na Msekwa asingekuwa Naibu Mwenyekiti. Chama kinaendeshwa kifisadifisadi tu bila kufuata kanuni zozote.

CCM ni chama dola na ndio chama tawala hivyo sio lazima kiwe na washabiki wengi ila issues za CC na NEC ya CCM lazima zivutie ushabiki mwingi hata kutoka kwa wapinzani kwa sababu mustakabali wa siasa za Tanzania zinategemea kwa kiasi kikubwa nani ni nani ndani ya CCM,

Sawa sawa, tupo ukurasa mmoja nipenyezeee e-mail nitakupa more dataz ambazo ni za moto sana siwezi kuziweka hapa now,

Respect!

Mzee FMES,
Yaani hapa nimesimama mbele ya laptop yangu na nguo zangu za kiraia na nimekukung'utia SALUTE moja saaaaaafi.Ningekua na magwanda ningeingia humu kwenye laptop na kupiga salute mikono miwili.Jamani kuna yule ambae huwa anahoji mi-dataz yako na kukubeza.Yaani mzee unatoa mi dataz iliyo ya moto kabisa.Hapa mkuu mimi sina neno
ILA tu
CCM
Mtamkumbuka Mangula SANA.

Keep the focus brother, tupo ukurasa mmoja soon nitakwua na more naomba kulala kidogo maana a long day leo, soon nitarudi na more, wazee wote kwenye e-mail msiwe na hofu zinakuja, nipeni time kidogo!

FMES Wazee Wa Sauti Ya Umeme!

Well hii taarifa ya CCM , naona kuna ambao imewafurahisha sana, inaonyesha CCM wanaweza wakacheza trick au wakafanya jambo amablo watanzania wapenzi wa CCM wakalifurahia, quotes zote hapo juu zinapelekea

1. Kuwasifu CCM!!!
2. Kuwa alert CCM wasifanye makosa
3. Zinaonyesha ni za wapenzi wa CCM waliochoka na mwenendo wa CCM
4. Mpaka wengine wanamsaidia Kikwete amweke katibu nani!!!!

Hii inanipa picha kuwa CCM kuondoka madarakani ni kazi sana, maana wale wapinzani nao pia ni washabiki wa CCM, yaani ni kama Yanga anacheza na Arsenal huku kuna wachezaji wa Yanga ambao ni arsenal damu!!

Hii hali inatisha, inabidi tukae chini na kujiuliza CCM tangu mwaka miaka ya 60 mpaka leo imefanya nini au ndio kuwa excited na habari za UVCCM?

Kazi hipo, kuna somo kali inabidi litembee hapa

CCM inabidi iondoke madarakani kwa namna yeyote ile!!!! mpo!!!!!

Kama dataz ni hizi za kichama!! nina wasiwasi haya tupo!

what are you exciting for??

We have proved by any means CCM 'hawatatutoa' lets build our strategy how to remove them from power!!

Kesho Kikwete akisema anajiuzulu nafasi yake kuchukuliwa na fulani mnayempenda mtaandamana mtaani kuisifia CCM, kama Mkapa alivyomwachia madaraka Kikwete amekaa pembeni ametulia-anakula nchi na kiwira yake, ndivyo mtakavyofurahi eti kusikia Kiwete amejiuzulu, atakaa pembeni na kula nchi, hao mnaowaona wazuri SIO WAZURI WANGEKUWA WAZURI TU, KAMA WANGEONDOKA CCM, KAMA NYERERE ALIVYOSHAURI, angalau mrema alijaribu

sijaona mwanamapinduzi ktk post hizo hapo juu nimeona washabiki wa CCM waliojificha ndani ya mwamvuli wa wanamapinduzi! ambao wako tayari kutuaminisha kuwa hawaipendi CCM huku wa vinywa na matendo wakiipenda CCM. Sina maana hawatakiwi washabiki a CCM humu la, swala ni kuwa kama mshabiki wa CCM, bado una ndoto kuwa iko siku CCM watafanya mabadiliko naomba, nikuonee huruma sana, CCm ndio waliotufikisha hapa tulipo tukiwa nchi ya pili kwa umaskini duniani, lakini inayoongoza kwa mali asili!

Sorry ,my style of writing this kind of critics is ''message sent' huwa sina utaalamu wa kumuelewesha mtu anayebisha au kupinga nilichoandika


Someni tena post zenu, muwaleze watu kuwa maana yenu ni nini? FMES kweli hulali kisa CCM

haraka haraka naona ktk kundi hilo hapo juu kuna waliokuwa CCM walihama, lakini wana kadamu ka CCM, na wako tayari kurudi wakisikia kitu cha kuwafurahisha HATA KAMA NI KIINI MACHO!!! HATA KAMA HAKILENGI KUWASAIDIA WATANZANIA WOTE!!
''don't mind criticism. If it is untrue, disregard it; if unfair, keep from irritation; if it is ignorant, smile; if it is justified it is not criticism, learn from it''.


waberoya
 
Mmeacha kuzungumzia kushindwa kwake kuliongoza Taifa kwenye suala la wizi wa fedha za EPA mmebakia kuimba nyimbo za CCM. Hivi mnafikiri ni bahati mbaya kwa NEC kukutana siku moja baada ya suala la EPA na kuja na maamuzi mazito?

a. Kule kulikoibiwa fedha kwa mabilioni hakuna mtu aliyetimuliwa, kuitishiwa kikao wala nini
b. Kule ambako hakuna wizi wowote ule wala kughushi watu ndio inadaiwa hata kupoteza kazi watapoteza.

Tukisema Ibara 15:1 Iko kazini watu wanasema tunaionea CCM.
 
Pole Mkuu FMES! dataz unazoleta ni za moto mnoo..ndio maana wajumbe wengine wanafikiri wewe ni mjumbe wa cc.Usikate tamaa mchango wako unaeshimika.
 
Mmeacha kuzungumzia kushindwa kwake kuliongoza Taifa kwenye suala la wizi wa fedha za EPA mmebakia kuimba nyimbo za CCM. Hivi mnafikiri ni bahati mbaya kwa NEC kukutana siku moja baada ya suala la EPA na kuja na maamuzi mazito?

a. Kule kulikoibiwa fedha kwa mabilioni hakuna mtu aliyetimuliwa, kuitishiwa kikao wala nini
b. Kule ambako hakuna wizi wowote ule wala kughushi watu ndio inadaiwa hata kupoteza kazi watapoteza.

Tukisema Ibara 15:1 Iko kazini watu wanasema tunaionea CCM.
Mkuu umeshtuka eh?
 
1.
Mmeacha kuzungumzia kushindwa kwake kuliongoza Taifa kwenye suala la wizi wa fedha za EPA mmebakia kuimba nyimbo za CCM. Hivi mnafikiri ni bahati mbaya kwa NEC kukutana siku moja baada ya suala la EPA na kuja na maamuzi mazito?

2.
Mkuu umeshtuka eh?

3.
what are you exciting for??


Wakuu wote heshima mbele, na wakulu Mwanakijiji, Invisible, na Waberoya,

Ninaomba niseme hivi, mimi ni mwananchi M-Tanzania, ninatoka mbali sana na taifa langu hili, katika hii safari nimejionea mengi sana mazuri na mabaya. Katika siasa za sasa niliamua kwa makusudi binafsi kujiunga na kundi la kupinga ufisadi, na pia nikajiunga hapa JF ili kuendeleza mapambano hayo na kutoa mchango wangu hata kiduchu kwa ajili ya taifa langu.

Katika vita kuna kushinda na kushindwa, sina tatizo kukubali kushindwa lakini ni haki yangu kufurahi inapotokea ushindi hata kiduchu, regardless ule ushindi umekujaje au umeletwa na nani! Je leo nina furaha kwa sababu CCM imebadilika na sasa Tanzania ni safi ever? Hapana! Eti sasa katiba imebadilika hapana! Matatizo ya taifa langu yapo pale pale, lakini jana mafisadi wamepigwa kipigo kizito, tena sana. Jana kwa mafisadi ni siku ya huzuni kubwa sana kuliko hata siku Lowassa alipoondolewa kwa rushwa.

Tarime aliyeshinda ni Taifa langu, na ndio matokeo yake haya sasa yanashuka mpaka chini pole pole, sasa eti ninafurahia nini, ninafurahia kupigwa fimbo jana kwa mafisadi ambao toka Dr. Slaaa atanagaze rasmi majina yao na matendo yao maovu, tumekuwa katika heka heka kubwa ya kupigana nao, yes sometimes wanashinda, lakini na sisi wananchi walalahoi tunashinda pia, na this is one of huo ushindi.

Eti tunaishangilia CCM in general hapana, lakini pia tunakuwa samba samba with time, tunakua current with our national politics. Tarime Chadema iliposhinda tumeshangilia sana, na mimi CCM nikiwa mmojawapo sikusikia mtu hapa akinilaumu, eti ni kwa sababu Taifa litakuwa halina tatizo tena? Hapana, ila ni kwa sababu matokeo kama yale yanaweza kuwafanya CCM wakaanza kua na akili japo kidogo, na huu unaweza kuwa ndio mwanzo wenyewe.

Hapa tunashngalia uwezo wetu JF wa kuweza kupata habari nyeti, nzito, na muhimu za taifa mapema na fast kabla wananchi karibu wote wa Tanzania, hawajazipata, eti hiyo sio sababu nzito ya kua na furaha? No kwangu ni heshima kubwa sana kwetu wananchi hapa kuweza kuongoza kwa upataji habari muhimu za taifa, kama vile tulipokuwa mbele kwenye kupata habari za kipigo cha Chunya.

Sasa do I need to apologise kwa sababu ya furaha yangu kwa mafisadi kupigwa changa la macho, absolutely No! Je ninafurahia nini? Ninafurahia kitendo cha mafisadi kukataliwa nafasi ya kutuburuza na pia kutupelekewa ujumbe mzito na CCM kwamba mchezo wao finally unaanza sasa kuwaudhi hata wale waliokuwa wakiwapigia kifua. JF tumeshiriki sana kwenye huu uamuzi wa jana kwa sababu tulikwua wa kwanza hapa kwueka hata mkataba feki wa jengo la UV-CCM, ni maudhi kama yale ndio yamepelekea huu uamuzi against mafisadi.

Salaam kwa Wote tulioko mastari wa mbele dhidi ya mafisadi, na tufurahie huu ushindi mdogo huku tukielewa kwamba mapambano bado kabisaa, na huenda ndio kwanza yameanza.

Na ninaahidi kwamba tupo pamoja na sasa tunajaribu kuendelea ku-monitor yanayojiri katika huu mkutano, na ninashukuru sana kwamba the ishu hapa leo JF sio uongo au credibility ya dataz, ila ni mengine ya kawaida kwenye siasa ambayo kwa ushindi huu mdogo, tuko tayari kuishi nayo.

Mungu Aibariki Tanzania! na Tuwe na amani!

FMES Wazee wa Sauti Ya Umeme! na Soon tutakua na uptodates!
 
Pole Mkuu FMES! dataz unazoleta ni za moto mnoo..ndio maana wajumbe wengine wanafikiri wewe ni mjumbe wa cc.Usikate tamaa mchango wako unaeshimika.

Mkuu pole pole ndugu yangu, sisi wote hapa JF ni ndugu moja hatuna ubaya tuna mshikamano mzito tuliachiwa na baba yaetu wa taifa Mwalimu, tunapendana sana, na tunahabarishana tu yanayojiri ndani ya kikao nyeti cha CC that is all, hakuna ya zaidi.

Lakini ubarikwie kwa uwezo wako mkubwa uliouonyesha na hiyo analysis yako kiduchu, wa kuona nje ya box! Bwa! ha! ha! ha! ah! ah!
 
kazi kweli kweli, utabiri wa manabii utimie.

avatar_no issues.jpg
 
Kikwete, Msekwa na Makamba wote wajiuzulu Mwenyekiti wa Muda Warioba, Makamu Mwenyekiti Mwakyembe na Katibu Mkuu FMES

Mkuu Bubu,

Chonde chonde bro, mbona unataka kuniletea noma na "Wakulu" hapa? Bwa! ha! ha! ah! ah!
 
Tayari mbio zimeanza kwa ajiri ya uchaguzi mkuu mwaka 2010.

Lets,see........... baadaya ya kukisafisha chama,then what....? Bangusilo wa EPA........?,au Daraja la Kigamboni....? Hapana i guess this one itaua upinzani kabis TUTALIPA WALIMU NA WAZEE wa EAC .!!!!!!


Mkuu sanda no U turn for now .Hakuna hoja ya sasa inaweza toka CCM na ikaua upinzani .At least si kwa issues ambazo ziko mezani kwa sasa .
 
Habari za ndani so far za sasa hivi ni kwamba mwenyelkiti wa CCM leo ameamua kutengua jina la mgombea wa uenyekiti wa Wazazi, Mbunge Mkono.....Stay tuned tunarudi na more soon.....!
 
Habari za ndani so far za sasa hivi ni kwamba mwenyelkiti wa CCM leo ameamua kutengua jina la mgombea wa uenyekiti wa Wazazi, Mbunge Mkono.....Stay tuned tunarudi na more soon.....!

Hizi nguvu za mwenyekiti zinawalakini katika maamuzi muhimu ya wanachama, nadhani inabidi vyama viangalie upya katiba zao juu ya hizi nguvu/mamlaka.

Hili nalo linamtazamo ule ule wa mamlaka aliyopewa Rais wa nchi yetu kikatiba, Mungu bariki asije akageukia na mamlaka yake katika katiba ya nchi yetu kabla ya kumpunguzia.
 
The more dataz ni kwamba:-

1. CC imepitisha majina 3 ya wagombea uenyekiti wa UV-CCM toka Zanzibar, nao ni Yusuf Hamadi Masauni, Suleiman Haji, na Adila Vuai.

2. Mvutano mkubwa ulizuka katika kuamua nini cha kufanya na uchaguzi wa makamu wa mwenyekiti wa UV-CCM, ambapo katiba inasema wazi kwamba hapa ni lazima atoke bara,

- Baada ya mvutano mkali sana, ikaamuliwa majina ya waliokuwa wakigombea uenyekiti yachujwe na wachaguliwe kutoka kundi hilo kupata mgombea umakamu, kwa hiyo CC imewapitisha wagombea:- Beno Malisa, Hassan Bashe, na Bi Z. Kawawa.

3. Kwa upande wa Mwenyekiti wa Wazazi, leo jina la Mkono limetenguliwa, na kupitishwa majina matatu nao ni Bulembo, Mhina, na Mama Nyawazo.

4. Umoja wa kina mama, huko yameachwa majina yale yale matatu, yaani Mama Janet Kahama, Mama Sophia Simba, na Mama Masunga.

Kikao kinaendelea bado na tutaoa more dataz zitakapopatikana tu, ingawa sasa hivi ninapoandika ndio inajadiliwa agenda ya yaliyojiri Tarime, yaani Makamba na Msekwa on the hot seat.

So far hay ndio maamuzi muhimu yaliyofanyika, lakini baadaye tutakwua na more breakdown ya exactly yaliyojiri ndani ya kikao cha jana na leo.

Ahsante Wakuu!
 
Hapa ndipo bias ya serikali hii inapoonekana dhahiri kuwapa dole mafisadi. Ilishindikana nini kuchukua hatua za makusudi kuwajadili kwa kina mafisadi wa EPA, matatizo ya walimu, wazee wastaafu wa EAC kama la ccm limewezekana.

Kama majina hayo yaliyokuwa yakihusishwa na ufisadi yamepitishwa tena, kuna haja gani ya kuona kuwa mafisadi wamepigwa chini?

View attachment 2802
 
CCM inaongozwa na Mwenyekiti sio Msekwa. UV-CCM ilikuwa inaongozwa na Nchimbi mwenyekiti sio mwingine yoyote, na hayo yote yamejadiliwa kwa kina na makini,

Mwenyekiti ameahidi kuusimamia mwenyewe huu uchaguzi, na imeshafahamika wazi kwamba Bi Kawawa ndiye chaguo lake, huyu sio kundi la mafisadi, bado tunajaribu kuzipata dataz za yaliyojiri kwenye kikao cha mafisadi jana usiku. Tunategemea kuzipata soon!
 
Habari za ndani so far za sasa hivi ni kwamba mwenyelkiti wa CCM leo ameamua kutengua jina la mgombea wa uenyekiti wa Wazazi, Mbunge Mkono.....Stay tuned tunarudi na more soon.....!


Mkuu FMES hapa chumbani kuna habari za kutisha zina miminika juu ya tukio hili .Nataka kwenda pale Nyerere square nianze kuona nje ya ofisi za CCM kutakuwa na hali gani .Mkono tena ? Why ?Wacha nithibitishe hizi kwanza .
 
yale yale ya changa la macho, hongereni kwa ushindi mnaoitwa mafisadi

1. CC imepitisha majina 3 ya wagombea uenyekiti wa UV-CCM toka Zanzibar, nao ni Yusuf Hamadi Masauni, Suleiman Haji, na Adila Vuai.

2. Mvutano mkubwa ulizuka katika kuamua nini cha kufanya na uchaguzi wa makamu wa mwenyekiti wa UV-CCM, ambapo katiba inasema wazi kwamba hapa ni lazima atoke bara,

- Baada ya mvutano mkali sana, ikaamuliwa majina ya waliokuwa wakigombea uenyekiti yachujwe na wachaguliwe kutoka kundi hilo kupata mgombea umakamu, kwa hiyo CC imewapitisha wagombea:- Beno Malisa, Hassan Bashe, na Bi Z. Kawawa.
:eek:

danger.jpg
 
Mkuu sanda no U turn for now .Hakuna hoja ya sasa inaweza toka CCM na ikaua upinzani .At least si kwa issues ambazo ziko mezani kwa sasa .

Mkulu Lunyungu,

Nataka kuamini maneno yako,ila nahofia ya 2005 kujirudia.
Watu walisha sema kwamba huyu ni mbuzi kwenye gunia baadae ikawa ushindi kwa kishindo.
Na sasa itakua hivyo hivyo kwa issues ndogo ndogo kama hizi ndio watu wanajijenga.
Mwaka ule wauchaguzi watu alisema...."ooh sisi atuchagui chama ila Rais" haya yatokanayo na chaguo hilo tunayaona.
 
Back
Top Bottom