CCM yafanya maamuzi mazito Kamati Kuu?

1. Hatulipi kodi ya allowances. Tunalipa kodi ya mapato kwa mshahara. Tanzania hakuna anaelipa kodi ya allowances hata mmoja. Hii ni moja ya hoja ambayo Kambi ya upinzani Bungeni inasema kila mwaka. TRA walisikia hoja yetu na kuleta Bili kwa Katibu wa Bunge ya kodi kwa miaka 10 iliyopita ambazo wabunge wamekuwa hawalipi maana Income Tax Act inasema posho ni mapto na hivyo lazima zikatwe kodi (sitting allowances na sio per diems, maana per diems are simply transfers). Unajua tulichofanya? Tulikasirika ni kwa nini TRA inaleta Bili Bungeni na kuamua kutunga sheria kwamba income tax act 2004 isitumike kwetu.

Hali ni hiyo hiyo kwa Majaji, nao katika sheria ya majaji hawalipi kodi katika posho wanazopata.

Mimi ninaamini tunapaswa kulipa kodi katika allowances za vikao maana ni kipato kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato. Nimesema hivi wakati wa mjadala wa sheria ya Majaji mwaka jana. Nilisema hivyo (hata kama wenzangu walichukia) ndani ya Bunge mwaka huu wakati wa mjadala wa Sheria ya Bunge (National Assembly Bill, 2008).

Ninaamni kuwa kulipa kodi ni uzalendo - ishara ya uzalendo.

Swali lingine?

Nashukuru sana kwa majibu

Sio kweli kuwa hakuna watanzania hawalipi kodi ya allowances labda wafanyakazi wa serikalini ndo hawalipi kodi kwa hili. Hii ndo wanajizunia mana mshahara ni mdogo but allowances ni nyingi mpaka inapitiliza mshahara. If you personally or as chadema team mkalivalia njuga, i believe tanzanians will be responsible and accountable for their politics.

Nijuavyo kwenye baadhi ya makampuni binafsi ambayo yapo smart ni kuwa hakuna sitting allowances kwenye vikao wala warsha but kuna per diem ambayo wewe umeiita direct transfer. Ninaelewa kuwa ni direct transfer kwa kuwa unalipi malazi, chakula na may be bevareges. Makampuni hayo ambayo most of us hatuyapendi ni kuwa unaporudi unaretire na left over unarudisha kwa kampuni.

Any extra allowance ambayo host wa warsha au kozi anatoa. e.g. Bunge likimwita Mwanyika wa Barrick na mkampa posho hatakiwi kupokea mana ni double payment. I have no problem na majaji na wabunge to get xtra allowance cos sometimes you work on the difficult situations. But hili la kutokatwa kodi limenishangaza sana.... Can't chadema work on it? Makampuni smart wakitoa extra allowance e.g. Mwanyika tena akipewa likizo ya kwenda marekani na familia yake. akapewa advance ya million 10, anatakiwa akirudi aonyeshe risiti ya matumizi then iliyobaki anakatwa kodi as his income. Ninao ushahidi wa hili suala na huoni kama makampuni ya nje yanafuata sheria kuliko sisi wenyewe? Huoni kama chadema wakilishikia bango na ikawa implemented watu watakuwa makini na politics and huenda ndo mwanzo wa siasa za nchi hii kuwa rahisi?

Kwa mtazamo wangu ulipaji kodi bado ni tatizo. nahisi ni kutokana na mfumo uliopo. kama tukiwa na mfumo mzuri ambao kila mtu inambidi alipe kodi there is no way kuwa na mafisi na pia watanzania will get feelings of their accountability and responsibility of the local politics badala ya wanasiasa kuwa miungu watu simply ya ukwepaji kodi. CHADEMA wakianzia hapa katika mkakati huu, i believe ndoto zitatimia na pia there will be need kwa wafanyabiashara kuwa marafiki uchwara wa chama tawala.

Better bussinessmen work for politician rather than politician works for businessmen.
 
Back
Top Bottom