Elections 2010 CCM yabadili ratiba za kampeni

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Na Exuper Kachenje

ccmjk.jpg

CHAMA cha Mapinduzi(CCM), kimebadili ratiba za kampeni kwa mgombea wake wa urais, Jakaya Kikwete na sasa atafanya kampeni bila kupumzika tofauti na awali alipopangiwa siku za kupumzika.Agosti 20 mwaka huu, meneja wa kampeni wa CCM Abdulrahman Kinana katika mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari, alitangaza kuwa mgombea huyo wa urais atakuwa na siku 16 za kupumzika kati ya siku 68 za kampeni.

Kwa mujibu wa Kinana, Kikwete alipangiwa kufanya kampeni kwa siku 52 badala ya 68 na pia kupunguziwa uchovu wa safari kwa kuondolewa kilometa 58,000 ambazo angetumia kusafiri kwa barabara. CCM iliamua atumie pia helkopta kwa kampeni zake.

Katika kampeni zake kuwania urais mwaka 2005 kumbukumbu zinaonyesha kuwa Kikwete alisafiri kilometa 96,000 kwa barabara, na mwaka huu alipangiwa kusafiri kilometa 38,000 kwa barabara huku umbali uliosalia akipangiwa kutumia helkopta ili kumpunguzia uchovu.

Lakini habari kutoka vyanzo vya uhakika ndani ya CCM zinasema kuwa hatua ya chama hicho kuondoa siku za mapumziko kwa mgombea wake huyo wa urais, imekuja ili kukabiliana na upepo wa kisiasa ulivyo kwa sasa.

Vyanzo hivyo vimefafanua kwamba CCM imepokea taarifa za kiupelelezi zinazoonyesha kuwa iwapo Kikwete ataendelea na mfumo wa kampeni anaoutumia sasa wa kujipa siku za mapumziko, anaweza kupunguza kiwango cha kura anazotarajia kupata kumwezesha kuwa tena rais katika uchaguzi mkuu ujao, Oktoba 31.

"CCM imeamua kubadili mfumo wa kampeni za Kikwete... sasa hatapumzika kama alivyopangiwa awali, atafanya kampeni kila siku kwa siku zilizosalia," alieleza mpashaji wetuo.

Wapashaji habari hao walilidokeza gazeti hili kuwa taarifa ilizonazo zinaonyesha kuwa kuna wagombea urais wawili wa vyama tofauti ambao hadi sasa wameonyesha ushindani dhidi ya CCM, hali ambayo imekishtua chama hicho tawala na kuamua kuongeza nguvu katika kampeni zake kwa lengo la kulinda "ushindi wa kishindo".

Wagombea hao wametajwa kuwa ni Dk Willbrod Slaa wa Chadema na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF wanaoelezewa kufikisha kampeni zao hadi vijijini hivyo kuwa na uwezekano wa kupata idadi kubwa ya kura.

Katibu mkuu wa CCM, Yusuph Makamba hakupatikana jana kutoa ufafanuzi wa taarifa hizo, lakini katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, John Chiligati hakutaka kuzungumzia suala hilo.

Badala yake alisema: " Sasaa, ahh, hilo muulize mheshimiwa Kinana , mimi nipo jimboni Manyoni natafuta kura za CCM; napambana; anayetoa taarifa zote kitaifa kuhusu kampeni za uchaguzi za CCM ni Kinana."

Lakini Kinana alisema: " Si kweli, kuna siku chache ambazo ni lazima apumzike."

Alipoelezwa zaidi kuhusu lengo la kumwondolea Kikwete mapumziko, meneja huyo wa kampeni wa CCM alisema: "Haiwezekani akafanya kampeni siku zote bila mapumziko. Kama binadamu Kikwete lazima apumzike, bila kusahau huyu bwana (Kikwete) pia ni rais, lazima apumzike siku chache awepo pia ofisini, lazima arudi Dar kwa ajili ya kazi za ofisi."

Bila kufafanua zaidi Kinana aliongeza kuwa hata ikiwa wagombea wa upinzani wanafanya kampeni zao kwa nguvu kubwa sasa, siku zijazo watakwama na hawataifikia CCM hivyo kutoitia hofu ya kukosa ushindi wa kishindo.

Kikwete alipata ushindi wa kishindo mwaka 2005 wakati alipoingia Ikulu kwa mara ya kwanza baada ya kunyakua zaidi ya asilimia 90 ya kura zote, lakini mwamko wa wananchi katika miaka ya karibuni na kuzidi kuimarika kwa vyama vya upinzani kunaonekana kunaweza kuondoa uwezo wa CCM kurudia rekodi hiyo

Source:Mwananchi
 
Mtu mwenyewe ni mgonjwa huyo, bado wanataka kum"overwork!
Watalia kilio cha mbwa hawa!
 
Na Exuper Kachenje

View attachment 13425

Lakini Kinana alisema: " Si kweli, kuna siku chache ambazo ni lazima apumzike."

Alipoelezwa zaidi kuhusu lengo la kumwondolea Kikwete mapumziko, meneja huyo wa kampeni wa CCM alisema: "Haiwezekani akafanya kampeni siku zote bila mapumziko. Kama binadamu Kikwete lazima apumzike, bila kusahau huyu bwana (Kikwete) pia ni rais, lazima apumzike siku chache awepo pia ofisini, lazima arudi Dar kwa ajili ya kazi za ofisi."

Bila kufafanua zaidi Kinana aliongeza kuwa hata ikiwa wagombea wa upinzani wanafanya kampeni zao kwa nguvu kubwa sasa, siku zijazo watakwama na hawataifikia CCM hivyo kutoitia hofu ya kukosa ushindi wa kishindo.

Kikwete alipata ushindi wa kishindo mwaka 2005 wakati alipoingia Ikulu kwa mara ya kwanza baada ya kunyakua zaidi ya asilimia 90 ya kura zote, lakini mwamko wa wananchi katika miaka ya karibuni na kuzidi kuimarika kwa vyama vya upinzani kunaonekana kunaweza kuondoa uwezo wa CCM kurudia rekodi hiyo

Source:Mwananchi

Zilizopigwa zilikuwa ni asilimia ngapi za walio jiandikisha?
 
Ngoja wammalizie kabisa, lakini wasisahau kumtengenezea helment kwani kwa ugonjwa wake wa kuanguka hatamaliza salama kampeni.MASIKINI MUUZA SURA
 
Back
Top Bottom