CCM ya Nyerere Iko Wapi?

chuwaalbert

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
3,598
2,115
Sipendi staili ya kampeni wakati wa chaguzi kuu na ndogo hapa nchini. Kampeni maana yake ni KUSHAWISHI wapiga kura ili waone uzuri wa mgombea (na pengine chama chake) hatimaye kufanya UAMUZI wa kuchagua. Huyu akisha chaguliwa ANAPEWA DHAMANA ya kuwawakilisha waliomchagua na wasio mchagua katika chombo cha maamuzi (kama Bunge). Hapa mgombea anayefanikiwa kuchaguliwa kuwa mwakilishi wa Wananchi, anafanya kazi kwa mujibu wa ibara ya 63 (3) a-e, ya katiba ya JMT. Kwa maana hii kampeni ni NAMNA mgombea mmoja ANAVYOWASHAWISHI wapiga kura kwamba yeye ANAFAA zaidi ya wenzake, kuwa mwakilishi wao katika chombo husika, kama Bunge. Kwa sasa kumezuka mtindo wa Wagombea na/au Vyama vyao, HASA CCM, KUWARUBUNI wapiga kura kwa ahadi hewa ZISIZOTEKELEZEKA katika mazingira ya kawaida ya utendaji kazi. Pia kampeni hizi mara nyingi ZINALENGA kubomoa HAIBA ya mgombea mshindani badala ya NAMNA ambayo Mshindi atakavyo “wasemea” wale atakao wawakilisha. Nina mifano michache kutoka katika kampeni zinazoendelea huko Arumeru Mashariki. · Vincent J K Nyerere siyo wa UKOO wa Kambarage! · Dkt Slaa alikwiba fedha za kanisa wakati wa ziara ya Papa Yohana wa Pili hapa nchini. · BWM aliuza mashamba yaliyoko Meru kwa Walowezi. nk nk. Hapa napenda kusisitiza kuwa CCM imepotoka kutoka katika misingi ya AHADI zake zilizolenga kusukuma maendeleo ya jamii na maisha binafsi ya Watu. Tujikumbushe Ahadi hizi: · Binadamu WOTE ni ndugu zangu. · NITAITUMIKIA nchi yangu na watu wake WOTE. · NITAJITOLEA nafsi yangu kuondoa umasikini, ujinga magonjwa na dhulma. · Rushwa ni ADUI wa HAKI, sitapokea wala kutoa rushwa. · Cheo ni DHAMANA, sitakitumia cheo change wala cha mtu mwingine kwa faida YANGU. · NITASHIRIKIANA na wenzangu KUJENGA nchi yetu. · Nitasema KWELI DAIMA fitna kwangu mwiko. (Ziko kumi nakumbuka hizi saba). Kimsingi, kama kiongozi mtarajiwa anaongozwa na MAUDHUI ya ahadi hizi, HATATUKANA, HATAZUSHA, HATATOA AHADI HEWA ama kufanya namna nyingine ya “sarakasi” kupata cheo! Nakumbuka mwaka 1980, wagombea Ubunge walipewa alama za Jembe ama Nyumba, kama msingi wa kujenga hoja wakati wa kuomba dhamana ya Uongozi. Walipimwa na wapiga kura kwa uwezo BINAFSI (siyo wa wapiga debe) wa kujenga hoja ya namna ya kuwatumikia wanaowawakilisha kwa FALSAFA ya alama husika kila mmjoja aliyopata katika hizi mbili. HALI HII IMEPOTELEA WAPI? Siku hizi haya hayaonekani. Yanebaki matusi, kuibuliana kashfa, kufanya fujo, kuhonga wapiga kura kwa fedha, fulana, kofia, pilau (na nyama?) na kusombwa kwenye malori ili kujaza mikutano ya kampeni! Msingi mkubwa wa ushindi wa CCM umekuwa fedha na mitandao ya kibaguzi na kimaslahi binafsi, bila kujali mustakabali wa nchi. Kwa minajili hii, viongozi waadilifu hawapatikani ndani ya Chama na katika nafasi za uwakilishi. Wananchi wanakosa watetezi bora katika masuala yanayohusu mustakabali wao. Nihitimishe kwa kusema kuwa umefika wakati kwamba katiba ya JMT itamke wazi (na ufuatiliaji uwepo) kuwa mchakato wa kuwapata wawakilishi uongozwe na MISINGI ya vipaumbele vya maendeleo ya wananchi na mustakabali wa UMOJA na AMANI ya Nchi. Hii itaifanya usimamizi wa demokrasia ya Uwakilishi kuzingatia UTU wa Mtanzania na siyo maslahi ya kundi dogo linalotumia nafasi ya uwakilishi kwa maslahi binafsi!

 
Wazee ambao ni wa ccm kama mkapa ambao wao ndio wahasisi wa vyama vingi wangekuwa free na washauri wa vyama vyote,lakini kutokana na ufisadi,uwizi mauji kama ya pemba anaogopa upinzani ukishika nchi watashtakiwa na kufungwa na kufilisiwa wako radhi demokrasia ibakwe kwa manufaa yao.
 
Back
Top Bottom