CCM ya Leo ni Sawa na Supu ya Kongoro, haina ladha

The Prophet

JF-Expert Member
Mar 17, 2011
682
94
haina ladha kabisa.

kila kitu wanachojaribu kubuni kuwashawashi Watz kioaonekana ni kioja kama si kiroja. kama hii ya kujivua ga,mba ilionekana kama itakuwa kitu maarufu, lakini kama mimi binafsi (nadhani ata Watz wengine watasapoti) sijaona mantiki yake; wala sijakunwa kabisa. kusema ccm inajiumba upya kama chiligati alisema mimi naona maigizo tu. kwa sababu hakuna kitu kinachojiumba pekee isipokuwa kwa Mungu kila kitu huumbwa. sasa hawa wanasema wanajiumba upya maana yake nini?

na hii hoja ya nape ya kusema ati watoto walizaliwa 1997 mwaka 2015 watakuwa wapiga kura; sawa ni kweli . mimi na madogo zangu walizaliwa miaka hiyo, lakini nape asahau kabisa kupata hata kura iliyoharibika kutoka kwao.

ccm kama inataka kuumbwa upya, ikubali kuachia madaraka. miaka hii si ya kutawala kwa propaganda. ccm ni chafu. imeoza inanuka. haisafishiki kwa ghilba za kujivua gamba.

sounds like a joke, huh?

wait and see......................
 
ndo maana wako bize kukamulia mindimu na pilipili kuweka ladha lakini wapiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Hapo umekosea kwa kufananisha CCM na supu ya kongoro! Ninachokijua mimi supu ya kongoro ina ladha nzuri sana na ni best!!! Kwa mantiki hiyo CCM itakuwa BEST
 
Ni ngumu kuwakubali hata mkisema mmevua gamba , mnaendeleza ufisadi,mkutano wa kutambulisha viongozi wapya pale Dom kibali kilikuwa na uhalali???? Watu waliopewa posho ili wajaze mkutano ni haki na halali?? Nawachukia hamjui tuu.mimi ni mpenda haki sina chama .
 
Back
Top Bottom