Elections 2010 CCM wnapiga kampeni mpaka siku ya Uchaguzi!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,543
Wanabodi, niko mahali nafuatilia matangazo ya moja kwa moja ya uchaguzi kupitia tv zetu ambazo zote ziko live, Mgombea wa CCM jimbo la Monduli, Edward Lowassa ameendeleza kampeni za uchaguzi kupitia
matangazo ya moja kwa moja toka Monduli.

Mzee Lowassa akihojiwa na Mtangazaji wa Channel Ten Arusha, na kuunganishwa moja kwa moja na mtangazaji wa studio akiwa live, amesema zoezi la kupiga kura, linaendelea vizuri kabisa huko Monduli.

Alipoulizwa ana maoni gani kuhusu uchaguzi, alijibu, " Naendeea kuusisitiza ule wito wetu, wananchi tuchague mafiga matatu ili CCM iibuke na ushindi wa kishindo!"

Mtangazaji akamshukuru na kumuaga.
wajameni, hii sio kampeni kweli mpaka siku ya uchaguzi?.

kafulia huyo....anaona mambo yameshakuwa magumu....hakuna kitu hapo

Angalizo, nimeitaja CCM kama chama kwa kosa la member wake mmoja, kwa vile member huyu sio just an ordinary member, ni mjumbe wa CC, Mjumbe wa NEC, former PM na waziri aliyeshika wizara mbalimbali, hivyo he should have known better!.

kafulia huyo....anaona mambo yameshakuwa magumu....hakuna kitu hapo

Pretty Girl Preta, Lowassa hawezi kufulia Monduli, kwa Monduli, baada ya Mungu, ni Lowassa ndipo wengine wanafuatia. Tangu issue ya Richimonduli, leo nimemsikia tena akizungumza kwa uchangamfu wake, alihamanika na kuteleza ulimi.

Cha Msingi ushahidi ukusanywe ili baada ya Uchaguzi watu wacheki naye mahakamani

Kama ni kweli basi NEC itaarifiwe ili imuengue -- kama makamishna hao wanazo balls!!!!!

Cha Msingi ushahidi ukusanywe ili baada ya Uchaguzi watu wacheki naye mahakamani

Ndege ya Uchumi, kwa Monduli, the margin will be huge, hivyo kumfungulia mashitaka will be a waste of time and resources. Ushahidi upo, off-air footage inapatikana.

Ndege ya Uchumi, kwa Monduli, the margin will be huge, hivyo kumfungulia mashitaka will be a waste of time and resources. Ushahidi upo, off-air footage inapatikana.

Mkuu wastage of time kivipi? kwani Mtu akienguliwa kwa kosa lolote uchaguzi ukirudiwa na yeye anagombea?

Mkuu wastage of time kivipi? kwani Mtu akienguliwa kwa kosa lolote uchaguzi ukirudiwa na yeye anagombea?

Kuna makosa ya kuvunja sheria, taratibu na kanuni, mwisho wa kampeni ni jana, hiyo ni kanuni sio sheria. Ukivunja kanuni mahakama itaangalia impact ya kuivunja kanuni ile kwa wananchi wa Monduli, jamaa ametangazia Channel Ten ambayo haina impact kwa wapiga kura wake japo ina impact kitaifa.

Vipi kuhusu Mabango ya CHagua Kikwete Jijini Dar mbona wameondoa baadhi na mengine yameachwa? kwa mfano pale round about ya BP kuelekea Kurasini, na pale Roundabout ya Jitegemee Secondary, kwanini hayo mabango hayajaondolewa?

ushahidi huo

Naomba nieleweshwe kwani kidogo hii inanitatiza...kama kupiga campaign siku ya uchaguzi (leo) ni kinyume na taratibu za NEC natumaini basi hii ni katika ujumla wa media zote; yaani TV, News Papers, Podiums, and Radios. Je kwa sisi tunaoendelea kufanya hivyo kwa namna moja au nyingine kupitia kwenye media hii ya Internet je ni kwamba tunavunja sheria au vipi?...naomba nifafanuliwe.

Naomba nieleweshwe kwani kidogo hii inanitatiza...kama kupiga campaign siku ya uchaguzi (leo) ni kinyume na taratibu za NEC natumaini basi hii ni katika ujumla wa media zote; yaani TV, News Papers, Podiums, and Radios. Je kwa sisi tunaoendelea kufanya hivyo kwa namna moja au nyingine kupitia kwenye media hii ya Internet je ni kwamba tunavunja sheria au vipi?...naomba nifafanuliwe

Kwa upeo wangu Lowassa kushindwa Monduli ni kitu ambacho hatuta kaa tukione.Tujifariji lakini tujue ukweli ndio huo.
Lowassa anajua hatima ya ndoto yake inaweza kuwa leo kama upinzani wakifanya vizuri kwenye ubunge.Labda ndio sababu ya kusema hayo.

CCM wanaendelea na kampeni Dar-es-Salaam.

Afande Kapinga wa Kinondoni amethibitisha mgombea udiwani wa CHADEMA kata ya Kinondoni na wapambe wake wanashikiliwa na jeshi la polisi kituoni Oysterbay kwa kupigana na wapambe wa CCM kwa madai ya CCM kuendesha kampeni siku ya uchaguzi.

TBC imeripoti.

Hapo tuseme CHADEMA waanza fujo.
Kama ni hivyo kwani yeye huyo mgombea hajui wapi pa kuripoti hilo tukio?.

hakuna mafiga matatu kwa mafisadi. Wamefilisi vya kutosha nchi hii. Sasa yatosha!! Tanzania sasa ni mali ya watanzania

hizi ni dalili za kuzidiwa ndio maana wana piga kampeni mpaka sasa, wanaona muda haukutosha, na wenye nchi ni wao

Wanabodi, niko mahali nafuatilia matangazo ya moja kwa moja ya uchaguzi kupitia tv zetu ambazo zote ziko live, Mgombea wa CCM jimbo la Monduli, Edward Lowassa ameendeleza kampeni za uchaguzi kupitia
matangazo ya moja kwa moja toka Monduli.

Mzee Lowassa akihojiwa na Mtangazaji wa Channel Ten Arusha, na kuunganishwa moja kwa moja na mtangazaji wa studio akiwa live, amesema zoezi la kupiga kura, linaendelea vizuri kabisa huko Monduli.

Alipoulizwa ana maoni gani kuhusu uchaguzi, alijibu, " Naendeea kuusisitiza ule wito wetu, wananchi tuchague mafiga matatu ili CCM iibuke na ushindi wa kishindo!"

Mtangazaji akamshukuru na kumuaga.
wajameni, hii sio kampeni kweli mpaka siku ya uchaguzi?.

Ushahidi utafutwe/uhifadhiwe na Mpinzani/Wapinzani wake. Utajasaidia kumuengua kimahakama kama akishinda kwa njia hizi.

Back
Top Bottom