Ccm watumia mbinu za baba moi na kuvuruga chadema, mbwa wenye njaa warushie mfupa tu wataacha lindo

Chilisosi

JF-Expert Member
Oct 19, 2008
3,051
747
Wandugu zangu,
Mnakumbuka enzi za baba moi na akina oginga odinga, saitoti, njonjo nk, au kule kwa mzee robati mugabe??
Hawa jamaa ni kiboko , walipoona wapinzani wanazidi kupata nguvu basi waliangalia nani anayeweza kuingilika na anakubalika na jamii, basi wanamkatia kitu kidogo aanzishe vurugu, hapo kitakachofuata ni madongo kila kona na baadae chama cha upinzani kinagawanyika kila mtu kivyake, ukifika uchaguzi kama upinzani walikuwa wapate jumla ya aslilimia 60 tawala 40 basi itakuwa hivi
chama tawala 55 upinzani A = 30 upinzani B= 25 na ile 5% either wataamua kuachana na siasa kwa kukata tamaa au watarudi chama tawala au watajiunga na vyama vya kichovu kama pona.
Hivyo ndio CCM wanafanya. wameamua kutumia njaa ya Zitto kuivuruga chadema ili chama kipangaranyike wao wachukue tena 2015 kwa sababu bila hilo kwa nguvu ya chadema bila migogoro wangeweza kuingia ikulu kama wanasukuma mlevi. wao wakaangalia nani rahisi kumdanganya, wakamuona zitto wakamwambia kijana hapa hupati kitu kuna mbowe, slaa na labda hata magamba makubwa toka ccm ni bora ukamate mshiko wako vuruga upinzani utulie si unakumbuka mrema?? Mie nina uhakika wamefanya hivyo kwa sababu walikuja na dili ya shibuda likachemsha kwa sababu shibuda hana wafuasi wengi. kama vile jambazi likiingia kwenye nyumba yako inayolindwa na mbwa wenye njaa likitupa mfupa wale mbwa badala ya kulikamata jambazi wataanza kugombaniana mfupa. na hii ndio inayoendelea chadema sasa.
 
Back
Top Bottom