CCM wapoka sera ya Elimu ya Chadema?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Magazeti mengi leo yakiwemo Mtanzania na Majira yameripoti Waziri mwenye dhamana ya kusimamia maendeleo ya elimu hapa chini Profesa Jumanne Maghembe akinena ya kuwa sera ya elimu ya chama chake cha CCM ni kuruhusu wahitimu wa darasa la saba kuendelea kidato cha kwanza bila ya mchujo.

Hii inamaanisha ya kuwa kufanya vizuri darasani sasa siyo sera ya CCM ili mradi tu CCM wapate idadi kubwa ya wahitimu wa kidato cha nne bila ya kujali ujuzi ambao watakuwa wameupata: Quantity vs Quality..........CCM opts for quantity and trivialize quality in the process.

Vile vile Prof. Maghembe alitofautiana na viongozi wa ngazi ya juu ndani ya chama tawala pale alipodai ya kuwa elimu bure ni sera ya CCM. Hili linashangaza kwa sababu viongozi wengi wa ngazi ya juu ndani ya chama hicho wameendelea kuviponda vyama vya upinzani ya kuwa elimu bure haiwezekani na ni njozi za alinacha...........Ikumbukwe mahitaji ya miundo mbinu ya kutimiza njozi hii ya Prof. Maghembe ni kubwa maradufu na kama miaka mitano iliyopita mashule na zahanati bado zilizokusudiwa bado hazijakamilka na nyumba za waalimu ni ahadi nyingine hewa ya miaka mitano ijayo. Sijui ni lini CCM wataanza kujifunza kuacha kudharau uwezo wa watanzania katika kupambanua mambo.......

Hili linatia mashaka ya kuwa pengine Prof. Maghembe baada ya kuona upepo mkali wa matarajio ya raia kutaka elimu iwe bure basi ameamua kuigeuza sera ya chama chake bila ya ridhaa ya Kamati kuu au Halmashauri Kuu ya chama chake.

Vile vile si katika ilani ya uchaguzi ya CCM ambapo suala la elimu bure limewekwa bayana hata kidogo.

Prof. Maghembe anaonekana hana mawasiliano na uongozi wa juu ndani ya chama chake kwa sababu hakuonyesha ni elimu ipi ambayo CCM itatoa bure na kuanzia lini na itagharimu nini ukizingatia ahadi za mgombea uraisi wa CCM hadi hivi sasa zimezidi trilioni 90 na huku akidai elimu na afya havitakuwa bure.

Ni dhahiri kama elimu nayo ni bure kwa CCM basi jumla ya ahadi zake sasa zitazidi trilioni tisini ambazo hata hapo zilipo hazitekelezeki hata wapigakura wangeliamua kuipa CCM miaka mingine ishrini madarakani.......... Kwa hiyo CCM ni danganya toto.........
 
MI sishangai wakuu, maana hata Dr Kamara hakuwa anajua katibu mkuu wizara ya viwanda, Biashara na Masoko kaagiza cement ishushwe bei huku akishangaa ni kwa nini cement inapanda hovyo hovyo. Sasa Majembe naye anasahau wenzake walishakataa kuwa elimu bure haiwezekani. What the hell is this? Ni kama anaamka toka usingizini.
 
Ukweli kwamba CCM wameshikwa pabaya, elimu sasa ni bure baada ya kukejeli ahadi kama hizo zilipotolewa na Chadema na CUF. Na inavyoonekana hakuna ilani tena bali ni twanga kanyaga kwa kwenda mbele, ili mradi kura zipatikane. 2015 tutabuni uongo mwingine, na uzuri ni kwamba watz hawanakumbukumbu
 
CCM imekwisha kufa, maana hata makada wake hawaelewi sera ya CCM ya elimu - ni bure au sio bure.
 
Siku ya kufa MANYANI, Miti yote huteleza.
Baada ya Miti yote ya CCM Kuteleza(Sera), sana naona wanaanza kudandia sera za CHADEMA.

Kaazi Kweli Kweli

CCM is dead,...Kwishney..
 
Jana Waziri wa Elimu Prof.Magembe amesema kuna mchakato unafanywa na serikali ili Elimu ya lazima iwe hadi darasa la kumi na mbili (form four) na serikali itagharamia kama ilivyo kwa elimu ya msingi kwa sasa.Mwenye taarifa zaidi atupe.
 
Ingefaa Chama kinapochukua Sera ya chama kingine kilipie kama ilivyo kwa hati miliki.
 
Slaa alishasema kwamba ccm wanatekeleza yale anayoyasema yeye. Kimsingi Slaa ndiye amekuwa kiongozi wetu kwa miaka mingi tu; ccm wakiwawatekelezaji. Hawana jipya wale. Kwisha habari yao.
 
Babuyao,

Watanzania tumemtambua kiongozi wetu huyu wa siku nyingi,yaani dr slaa.Tutakachofanya ni kumdhihirisha hiyo tarehe 31 Oktoba,2010 ili atekeleze sera zake. Hao wanaoiga mawazo hawawezi kuyatekeleza vizuri kwani hawana mpango mkakati(strategic plan) hivyo watayumba kwenye mpango wa utekelezaji(Operational plan) hasa kwenye hizo sera walizoiga.
 
Hili la CCM kupoka sera ya Elimu ya CHADEMA sio la kushangaza. WanaJF naomba niwakumbushe, na kama mtaweza mlifanyie kazia hili. Ukiingalia kwa uzuri ilani ya CCM ya Mwaka 2005 ni yakudurufu kutoka kwenye ilani ya uchaguzi ya NCCR-mageuzi ya mwaka 1995. hiyo inaleta tafisiri gani? kwamba wao, kwa ujinga wao na uwezo wao mdogo wakufikiri, hawawezi kutengeneza vitu vizuri, but they are very good at plagiarizing..na huo ndiyo umekuwa mtindo wao wa kuendesha nchi. Sasa unategemea KINGUNGE awe na uwezo wa kufikiri vizuri kiasi cha kutoa ilani ambayo ni pro-poor? I don't think so....Na hao ndiyo wazee walishika chama, akifungua mdomo utatamani uzimie, maana hana busara, hana substance, hana maadili..yupo yupo tu.

GHOSH..CCM IS A DEVIL
 
Magazeti mengi leo yakiwemo Mtanzania na Majira yameripoti Waziri mwenye dhamana ya kusimamia maendeleo ya elimu hapa chini Profesa Jumanne Maghembe akinena ya kuwa sera ya elimu ya chama chake cha CCM ni kuruhusu wahitimu wa darasa la saba kuendelea kidato cha kwanza bila ya mchujo.

Hii inamaanisha ya kuwa kufanya vizuri darasani sasa siyo sera ya CCM ili mradi tu CCM wapate idadi kubwa ya wahitimu wa kidato cha nne bila ya kujali ujuzi ambao watakuwa wameupata: Quantity vs Quality..........CCM opts for quantity and trivialize quality in the process.

Vile vile Prof. Maghembe alitofautiana na viongozi wa ngazi ya juu ndani ya chama tawala pale alipodai ya kuwa elimu bure ni sera ya CCM. Hili linashangaza kwa sababu viongozi wengi wa ngazi ya juu ndani ya chama hicho wameendelea kuviponda vyama vya upinzani ya kuwa elimu bure haiwezekani na ni njozi za alinacha...........Ikumbukwe mahitaji ya miundo mbinu ya kutimiza njozi hii ya Prof. Maghembe ni kubwa maradufu na kama miaka mitano iliyopita mashule na zahanati bado zilizokusudiwa bado hazijakamilka na nyumba za waalimu ni ahadi nyingine hewa ya miaka mitano ijayo. Sijui ni lini CCM wataanza kujifunza kuacha kudharau uwezo wa watanzania katika kupambanua mambo.......

Hili linatia mashaka ya kuwa pengine Prof. Maghembe baada ya kuona upepo mkali wa matarajio ya raia kutaka elimu iwe bure basi ameamua kuigeuza sera ya chama chake bila ya ridhaa ya Kamati kuu au Halmashauri Kuu ya chama chake.

Vile vile si katika ilani ya uchaguzi ya CCM ambapo suala la elimu bure limewekwa bayana hata kidogo.

Prof. Maghembe anaonekana hana mawasiliano na uongozi wa juu ndani ya chama chake kwa sababu hakuonyesha ni elimu ipi ambayo CCM itatoa bure na kuanzia lini na itagharimu nini ukizingatia ahadi za mgombea uraisi wa CCM hadi hivi sasa zimezidi trilioni 90 na huku akidai elimu na afya havitakuwa bure.

Ni dhahiri kama elimu nayo ni bure kwa CCM basi jumla ya ahadi zake sasa zitazidi trilioni tisini ambazo hata hapo zilipo hazitekelezeki hata wapigakura wangeliamua kuipa CCM miaka mingine ishrini madarakani.......... Kwa hiyo CCM ni danganya toto.........
Hatuwashangai, Lipumba aliwambia wafute kodi ya maendeleo, waka mwambia prof uchwara, wamefuta wanadai ni sera yao. chadema walianza tumia helicopter wakasema chadema wanatumia vibaya pesa, leo Jk anatumia helicopter 3, hutashangaa kusikia wao ndio wamebini. Kinana amekuwa akipinga kwa nguvu zake zote sera ya elimu bure, Prof magembe anadai niyao. Juzi nimemskia katibu mkuu wizara ya viwanda anashangaa kwanini bei ya Vifaa vya ujenzi iko juu, baada ya kusikia Slaa atashusha bei.
 
Wanafahamu CHADEMA wanayoyahubiri yanawezekana..hawakuwa wamepewa challenge before..
Sasa katika kukurupuka labda jahazi halizami ndo kila mtu anaibuka na lake..kumbe ndo wanawaamsha wananchi wawafahamu true colour yao...
 
Back
Top Bottom