CCM wapinga pongezi za Museveni kwa Kibaki

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,003
Posted Date::1/6/2008
CCM wapinga pongezi za Museveni kwa Kibaki
Na Boniface Meena
Mwananchi

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kauli ya Rais Yoweri Museveni ya kumpongeza Rais Mwai Kibaki wa Kenya ni yake kama Rais wa Uganda na si kama Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, John Chiligati alipokuwa akitoa salamu za mwaka mpya za chama hicho jijini Dar es Salaam.

"Tamko la Museveni lilikuwa la Uganda tu na si la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambalo yeye ni Mwenyekiti wake," Chiligati alisema wakati akijibu swali lililoulizwa na gazeti hili.

Chiligati alisema pia kuwa, kumekuwepo na hoja kuhusu ukimya wa Rais Jakaya Kikwete katika ama kumpongeza Kibaki au kuungana na hoja ya kutambua uchaguzi huo kutokuwa huru na wahaki; na akafafanua kuwa ukimya wa Kikwete unatokana na yeye kujihusisha na usuluhishi wa tatizo lililopo na hivyo ameona ni busara kukaa kimya ili pande zote mbili ziweze kumuamini.

"Rais anashughulikia suala la usuluhishi ndio maana hajatoa salamu za pongezi. Siyo kwamba hajatoa pongezi kwa sababu hajakubaliana na matokeo."

Katibu huyo alieleza pia kuwa, CCM kama chama haikujihusisha na jambo lolote katika uchaguzi huo bali waliutazama tu kama majirani.

"Sisi kama chama hatukuhusika na chochote katika uchaguzi huo. Mchakato mzima ulikuwa ni mzuri maana kulikuwa na matatizo ya kawaida tu. Tatizo kubwa limekuja wakati wa kuhesabu kura," alisema.

Akitumia uzoefu wake alioupata nchini Lesotho ambapo alikuwa mmoja wa waangalizi wa uchaguzi, Chiligati alisema nchi hiyo ina utaratibu wa kuleta wakaguzi wa matokeo wa nje na lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha kuwa haki inatendeka.

"Kutokana na tatizo lililopo Kenya, nadhani wangeleta wakaguzi wa kimataifa maana hawafungamani na upande wowote. Kwa sasa hali ya Kenya imeshajionyesha kuwa hakuna uwezekano wa kuaminiana kati yao kwa wao."

Katibu huyo pia alifafanua kuwa, hali ya vurugu iliyopo Kenya inakwamisha harakati za kuelekea kufikiwa kwa Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki.

Mbali na hayo, Chiligati alielezea changamoto ambazo CCM inakabiliana nazo kwa mwaka 2008 kuwa ni; tatizo la mfumko wa bei, kupanda kwa gharama za mafuta, vita dhidi ya rushwa na ufisadi, ushirikiano na vyama vingine katika kujenga demokrasia na suala la muafaka wa Zanzibar.

Akifafanua kuhusu muafaka, Chiligati alisema; "mazungumzo ya muafaka yatafikia tamati muda mfupi ujao."
 
hata mimi nashangaa. anamkanusha mwenzake wakati na yeye
anafanya hicho hicho. labda angekuwa msemaji wa ikulu au
dk. msabaha ningeelewa.
 
Hawa bado wanafikiri "Chama Chashika Hatamu"

Hivi CCM ndiyo msemaji kwenye foreign policy yetu? Membe na Msabaha wako wapi?
 
Mwanakijiji una kauli ya Membe yenye msimamo kama huo wa CCM? Mara ya mwisho nimeona kauli ya Membe ilikuwa inasihi usuluhishi.
 
Lakini waongo wote. Mbona Ikulu ilipeleka afisa wake wa ngazi ya juu Nairobi wakati kura zinahesabiwa, na alikuwa kwenye kambi ya Kibaki mpaka Kibaki alipoapishwa? Alikwenda kufanya nini?
 
Back
Top Bottom