Hebu tuwe Wakweli na kuacha Ushabiki wa Kisiasa na kuangalia Mustakbali wa nchi yetu Kama kweli tuna Uchungu nayo, Maandamano ya Chadema as Such si tatizo kubwa, si Watu wanaandamana Kisha by Rae end of The day Wanaenda kulala? Lakini kauli zinazotolewa na Viongozi wa Chadema kwenye Mikutano ya Hadhara ya kuhitimisha maandamano hayo, Kwa kweli si Njema kwa Usalama wa Nchi yetu, k.m. kauli za Freeman kule Mwanza baada Maandamano, aliwahamasisha watu Wamkatae Rais wa Nchi (Kikwete) na Wawe tayari kwa lolote. Yanini? Kule Tunisia na Misri, maandamano hayakuongozwa na Vyama vya Siasa bali Wananchi waliochoshwa na Viongozi wao waliokaa Miaka mingi na Hawakuwa na Dalili za kuondoka Madarakani, Wananchi wakiamua, hakuna nguvu za Dola zinazoweza kuwadhibiti, lakini Wawe wameamua Wenyewe kwa kuona Hali imeshindikana, Sio kwa kuchochewa na Chama Fulani cha Siasa kinachotaka kushika Madaraka kwa Kuwaingiza watu Barabarani wala Msituni, angalieni Huko Tunisia na Misri mnakopenda kutolea Mfano, hakuna Chama kilichoshika Madaraka na Wala hakuna kinachoelekea kushika, Bali Misri ni Jeshi (la Mubarak) ndilo linaongoza, na Tunisia ni Vurugu Tupu zinaendelea kwani Waandamanaji hivi Sasa wamegeuka Vibaka wanapora Ovyo maduka na Kila Biashara iliyo Mbele Yao, Hali ni mbaya mno na Hakuna Mwelekeo wowote, Kama Chadema inadai inataka Kufanya hivyo, haitafanikiwa, Watanzania tulio Wengi hatutakubali. Savimbi aliposhindwa Uchaguzi alikuwa na Madai Kama ya Slaa na Chadema na alikuwa na wafuasi Wengi katika Maeneo mengi ya Nchi yake ya Angola kuliko ilivyo Chadema kwa Tanzania (Msisahau Chadema imeshindwa hata Kusimamisha Wagombea tu katika Majimbo Takriban 50! Na imeshinda 9% ya majimbo yote, basi hata Kama ni kuibiwa Kura lakini si kwa Kiasi hicho!) alianza Kama Chadema inavyoanza sasa, akapata Support ya nchi za Magharibi na akaanzisha Mapambano ya kisawsawa ya Kuondoa utawala wa MPLA, lakini wafuasi wa MPLA walikuwa wengi Zaidi, hivyo damu ilimwagika Kisawasawa Kuliko maelezo, kwa Miaka mingi. Savimbi alipochinjwa, Amani ikapatikana Angola kwa Kiasi kikubwa, hata Wafuasi wa Savimbi wanajutia walichofanya, hivi sasa wako Pamoja wanajenga Nchi Yao, Vyama vya Siasa vipo vinaendelea na Siasa na wanaamini Wakitaka kuiondoa MPLA wataweza kufanikiwa ikibidi kwa njia za Kisiasa na Sio Kama hivi Chadema inavyotaka kufanya.
Matamshi yatolewayo na Viongozi wa CDM baada ya Maandamano ndiyo yenye Utata, hakutakuwa na Mwisho mwema, Kwani wasiokubaliana na Matamshi hayo nao pia wapo na ni Wengi pia, Jee nao Wakiingia barabarani Hali itakuwaje?mbona maandamano kanda ya ziwa yameenda shwari jamani? Hawa ccm wanataka wawapangie cdm ratiba ya kuendesha mambo yao?
Hebu tuwe Wakweli na kuacha Ushabiki wa Kisiasa na kuangalia Mustakbali wa nchi yetu Kama kweli tuna Uchungu nayo, ....
Chama tawala,CCM kinaonekana kufikwa na maji shingoni na sasa kinatapatapa huku na kule ili kukidhibiti chama kikuu cha upinzani-CHADEMA ambacho kinafanya maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima.Maandamano na mikutano hiyo,kwa mujibu wa viongozi wa CHADEMA yana malengo ya kupinga malipo ya fidia ya sh.bilioni 94 kwa kampuni ya kufua umeme ya dowans,kupinga kupanda kwa gharama za maisha,kupinga kupanda kwa gharama za umeme,kupinga vitendo vya ufisadi,kuishinikiza serikali ya jk iweke ratiba ya mchakato utakaohakikisha uchguzi wa mwaka 2015 unafanyika chini ya katiba mpya.
CCM na serikali yake hawana majibu kwa hoja hizi nzito za CHADEMA,sasa wanakimbilia kuomba msaada wa dola.Kwa CCM kujifanya ionekane inaomba msaada wa dola badala ya kuviagiza vyombo vya dola ni unafiki mkubwa wa kisiasa,CCM wanataka waonekane machoni pa watanzania kuwa"hawatumii vibaya vyombo vya dola kuudhibiti upinzani,wakati inajulikana ni tabia yao kuvitumia vyombo vya dola kuwadhibiti wapinzani wao.
Kitendo cha CCM kuomba msaada wa dola kuwamaliza CHADEMA kisiasa ni ishara ya kufilisika kihoja na kisiasa,CCM sasa hawana hoja wanakimbilia kutumia nguvu za dola ambazo ziko chini ya udhibiti wao. CCM kutaka waeleweke na watu kwamba wanaomba msaada wa dola ni uzandiki na hadaa kwa watanzania.
Alichokiongea bwana Chiligati leo na wandishi wa habari alipokuwa anatoa tamko la kuomba msada wa dola kuidhibiti CHADEMA,hakina tofauti na kile alichokiongea bosi wake Kikwete.Kwa maana hiyo dhamira ya kuwabana CHADEMA ilishaanza kusukwa kabla hata kikwete hajaiweka hotuba yake yenye vitisho kwa CHADEMA hadharani kwa taifa.
Wakati katibu mkuu wa CHADEMA DK Wilbrod Slaa akisisitiza kwamba maandamano yanafanywa na CHADEMA ni ya amani ya yenye shabaha ya kuihimiza serikali iitikie kilio cha Umma ofisi ya msajili wa vyama vya siasa chini ya bwana tendwa imeungana na CCM kuwatisha na hatimaye kuwadhofisha CHADEMA kwa kuwasingizia kwamba wanafanya "UCHOCHEZI" katika mikutano yao.
Kudhihirisha kwamba anataka kuwafurahisha CCM au anatekeleza matakwa ya kisiasa ya CCM,Tendwa amefikia hatua ya kutamka maneno ya kukifuta CHADEMA na kuzungumzia uwezekano wa mkurugenzi wa mashita ya jinai kuwafungulia mashitaka CHADEMA.
Mtiririko wote huu unaonesha jinsi serikali ilivyojipanga kuwadhibiti CHADEMA.Fikiria Mtiririko wa mambo haya;"Kikwete anatoa hotuba leo ya kuwatuhumu CHADEMA bila sababu kesho wakuu wa CHADEMA wanakatwa kwa kisingizio cha uchochezi.CCM watangaza hadharani kuomba msaada wa dola na Tendwa anaingilia kati kutumia ofisi ya umma kuwasaidia CCM" yote haya ni ya kupangwa.
Jambo moja la faraja ni hili "CHADEMA kama watetezi makini wa watanzania walishajua yote haya kabla na walitarajia yangefanywa" Kwa hiyo kwa CHADEMA"MWENDO ULEULE MPAPAKA KIELEWEKE"
Mindi, maelezo yako yana Ukweli kiasi fulani ila yana Lack Proportionality. K.m. Mtu akipewa dhamana ya Kusimamia kilimo cha Shamba la Mahindi, shamba ambalo Normaly linatoa Gunia 500, yeye akalisimamia likatoa Gunia 2,000, lakini wenzake aliofanya nao kazi Wakaiba gunia 20! Sasa nyie wenye Shamba mkianzisha zogo kwa Wizi huo wa Gunia 20, na kudai kuwa Msimamizi hafai, Mkakataa katakata Kutambua kuwa kuna Gunia 1,800 ambazo ni ziada ya Gunia 1,300 kulinganisha na Awali. Sasa wenye Shamba wakihamasishwa Kumlaani na kumkataa Msimamizi huyo ndipo tunasema Kunakosekana Rationality, Waswahili wanasema Hasidi Hana Sababu, Lengo la Kuu la Chama chochote cha Siasa ni Kushika Dola, CDM is no Exception, huku CDM ikijua fika kuwa CCM haiongozwi na Malaika, lazma itafanya makos ya hapa na pale, ikaamua kuPortray makosa hayo kwa Jamii kana kwamba ndio kazi Pekee iliyofanywa na CCM na hakuna zuri hata Moja lilofanyika, labda wakishika Dola wao (Malaika?) maisha Yatakuwa mazuri Ghafla! Hebu piga Total ya fedha zote Unazojua zimeliwa na Mafisadi kupitia hujuma zote ulizozisikia, Kuanzia EPA, Kagoda, Meremeta, Dowans nk (ambazo zote Zina Miaka 5 au zaidi iliyopita, linganisha na Kiasi ambacho Serikali imezipata kutoka Vyanzo mbalimbali kwa Miaka 5 iliyopita na Zikatumika kwenye miradi mbalimbali ya Maendeleo Nchi nzima, Mijini na Vijijini ambayo inaonekana Waziwazi. Kijijini kwangu hivi Sasa kumepitishwa Barabara ya Lami, tumepata Mikopo kupitia SACCOS yetu, Tumepewa fedha za TASAF tukajenga Soko zuri linaongeza mapato ya Kijiji,Tuna Kituo cha Afya cha kata Kipo kijijini kwetu, tuna Sekondari ya Kata ipo kijiji Jirani, haina Walimu wala Vifaa vya Kutosha, lakini vyote hivi miaka 5 iliyopita havikuwepo, Kwanini tusiwape waliotufanyia Yote haya Muda zaidi ili warekibishe Mapungufu yaliyopo Kama ya Sekondari na Mengineyo badala ya Kuwatimua kwa Sababu ya Wizi wa 'yale Magunia 20?'