Kibona Dickson
Member
- Feb 13, 2011
- 37
- 14
Chama tawala,CCM kinaonekana kufikwa na maji shingoni na sasa kinatapatapa huku na kule ili kukidhibiti chama kikuu cha upinzani-CHADEMA ambacho kinafanya maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima.Maandamano na mikutano hiyo,kwa mujibu wa viongozi wa CHADEMA yana malengo ya kupinga malipo ya fidia ya sh.bilioni 94 kwa kampuni ya kufua umeme ya dowans,kupinga kupanda kwa gharama za maisha,kupinga kupanda kwa gharama za umeme,kupinga vitendo vya ufisadi,kuishinikiza serikali ya jk iweke ratiba ya mchakato utakaohakikisha uchguzi wa mwaka 2015 unafanyika chini ya katiba mpya.
CCM na serikali yake hawana majibu kwa hoja hizi nzito za CHADEMA,sasa wanakimbilia kuomba msaada wa dola.Kwa CCM kujifanya ionekane inaomba msaada wa dola badala ya kuviagiza vyombo vya dola ni unafiki mkubwa wa kisiasa,CCM wanataka waonekane machoni pa watanzania kuwa"hawatumii vibaya vyombo vya dola kuudhibiti upinzani,wakati inajulikana ni tabia yao kuvitumia vyombo vya dola kuwadhibiti wapinzani wao.
Kitendo cha CCM kuomba msaada wa dola kuwamaliza CHADEMA kisiasa ni ishara ya kufilisika kihoja na kisiasa,CCM sasa hawana hoja wanakimbilia kutumia nguvu za dola ambazo ziko chini ya udhibiti wao. CCM kutaka waeleweke na watu kwamba wanaomba msaada wa dola ni uzandiki na hadaa kwa watanzania.
Alichokiongea bwana Chiligati leo na wandishi wa habari alipokuwa anatoa tamko la kuomba msada wa dola kuidhibiti CHADEMA,hakina tofauti na kile alichokiongea bosi wake Kikwete.Kwa maana hiyo dhamira ya kuwabana CHADEMA ilishaanza kusukwa kabla hata kikwete hajaiweka hotuba yake yenye vitisho kwa CHADEMA hadharani kwa taifa.
Wakati katibu mkuu wa CHADEMA DK Wilbrod Slaa akisisitiza kwamba maandamano yanafanywa na CHADEMA ni ya amani ya yenye shabaha ya kuihimiza serikali iitikie kilio cha Umma ofisi ya msajili wa vyama vya siasa chini ya bwana tendwa imeungana na CCM kuwatisha na hatimaye kuwadhofisha CHADEMA kwa kuwasingizia kwamba wanafanya "UCHOCHEZI" katika mikutano yao.
Kudhihirisha kwamba anataka kuwafurahisha CCM au anatekeleza matakwa ya kisiasa ya CCM,Tendwa amefikia hatua ya kutamka maneno ya kukifuta CHADEMA na kuzungumzia uwezekano wa mkurugenzi wa mashita ya jinai kuwafungulia mashitaka CHADEMA.
Mtiririko wote huu unaonesha jinsi serikali ilivyojipanga kuwadhibiti CHADEMA.Fikiria Mtiririko wa mambo haya;"Kikwete anatoa hotuba leo ya kuwatuhumu CHADEMA bila sababu kesho wakuu wa CHADEMA wanakatwa kwa kisingizio cha uchochezi.CCM watangaza hadharani kuomba msaada wa dola na Tendwa anaingilia kati kutumia ofisi ya umma kuwasaidia CCM" yote haya ni ya kupangwa.
Jambo moja la faraja ni hili "CHADEMA kama watetezi makini wa watanzania walishajua yote haya kabla na walitarajia yangefanywa" Kwa hiyo kwa CHADEMA"MWENDO ULEULE MPAPAKA KIELEWEKE"