CCM waomba kuandamana Dar.. kesho kama CHADEMA, wakataliwa na Polisi; washukuru!

images

aisee..........
kaa.jpg
 
Ni vigumu kuamini kama nchi hii tuna viongozi wenye akili finyu kiasi hiki.CCM wamefilisika kiasi kwamba sasa hivi wanaishi kwa ku-copy & paste toka kwa CHADEMA. Ni hivi: CHADEMA wanatangaza kuandamana na sababu ya kuandamana wanatoa, pia wanatoa taarifa kwa vyombo husika kama taratibu zinavyosema, ghafla CCM nao wanatangaza kuandamana then police wanatangaza tumesitisha maandamano yote na kutaja kifungu walichotumia! Anatokeza msemaji wa ccm na kushukuru kwamba police wamekataza maandamano kwa sababu (tu) wamesema kifungu cha sheria walichotumia! Hivi mtu akisema uwezo wa ccm wa kufikiri ni wa ujima atakuwa amekosea?

Kwanza, ccm walikuwa wanaandamana kwa sababu gani?
Pili, ni lini hawa ccm waliamua kuandamana? Ni baada ya CHADEMA kutangaza kuandamana?
Tatu, hata kwa elimu ya kata, kama CHADEMA walitoa taarifa za kuandamana mapema, ccm wakatoa taarifa baadae si ni yule aliyewahi kutoa taarifa ndio ataruhusiwa? Kwa nini polisi wasiwajulishe ccm kuwa siku wanayotaka kuandamana tayari CHADEMA walishaiwahi hivyo wachague siku nyingine?

Lakini kitu ambacho sijaelewa hadi sasa, ni kwanini wakubwa hawa wanakuwa waoga watu kuandamana? CCM wanaweza kusema kama Tanzania ni nchi ya demokrasia? Na kwa kuzuia maandamano ina maana hisia za watu na maudhi waliyonayo au madai waliyonayo yanapotea au? Watu wazima wanafunika uso kwa viganja vyao wakifikiri umma hauwaoni - utoto!
 
Kibali cha Maandamano CCM wameomba kama geresha tu ili ionekane wote wamenyimwa na CCM wameheshimu amri ya polisi. Ni ujanja wa kitoto kiasi fulani na haulengi kuondoa tatizo bali kulilinda

Uko sahihi kabisa. Hizo ni mbinu tu zimetumika. Ila kwa ukweli kazi ya polisi ni ngumu sana. Katika kazi zote ambazo binadamu hapa duniani anafanya lakini ukichagua kuwa polisi nafikiri ndiyo umefikia ..........usione hawa hanaonyanyasa wenzao na kuwapiga mabomu ya machozi, kuwamwagia maji ya kuwasha na mengine mengi kwamba wao wanapenda kufanya hivyo, kwa kweli si wote wanaopenda kuyafanya hayo ila polisi ni kama robot. Robot linaendeshwa na kufanya kazi kwa kadiri anayelimiliki anavyopenda. Kadhalika na utendaji wa polisi wote unatokana na amri anazopokea kutoka kwa mkubwa wake. Na kibaya zaidi hatakiwi kuuliza kwa nini afanye lile analoambiwa akalifanye, yeye anatakiwa kutekeleza agizo/amri. Kinyume chake ni kuasi na unajua tena kuasi maana yake nini. Polisi akiamrishwa ashinde hapo juani atashinda hapo hapo kumsubiri kiongozi. Polisi akiambiwa kamata atakamata, ua ataua. Kwa hiyo pamoja na kwamba wana hali duni na kila mmoja anaona na pia wana kila hali mbaya ya maisha kama walala hoi wengine lakini kwa "nature" ya kazi yao usiwashangae kuona wanayoyafanya. Wakati mwingine roho zinawauma lakini lazima watekeleze. Kwa hiyo hawa wakati mwingine tuwasamehe bure tu
 
Back
Top Bottom