CCM waomba kuandamana Dar.. kesho kama CHADEMA, wakataliwa na Polisi; washukuru!

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
Katibu wa CCM Mkoa wa DSM Ameandika barua polisi akiomba kibali cha wana CCM kuandamana kutoka Vijana mpaka Kidongo chekundu eti kulaani viongozi wa CDM kukiuka sheria halali huko Arusha.

Ijulikane kuwa CDM waliandika barua tangu jana , na ilipofikia leo majira ya saa tano asubuhi huko Arusha Paul Chagonja ambaye ni kamishna wa Operesheni za Polisi alitoa tamko la kuzuia maandamano ya CDM nchi nzima .

Jioni hii Kova , ametoa barua kwa CDM na CCM akisema eti masuala hayo yapo mahakamani na wote wameshapewa dhamana ,

Kichekesho: Katibu wa CCM mkoa wa DSM ameongea na vyombo vya habari na kushukurui jeshi la polisi kusitisha maandamao yao .

Ndio maana CDM tunalalamika kuwa polisi wanashirikiana na CCM kutuhujumu kwenye kazi yetu ya siasa.

Mwenyekiti Mbowe mpaka sasa yupo Polisi huko Arusha akihojiwa tangu asubuhi saa tano kamili.
 
Kwenye red: "AKILI ZA KITOTO" Fumbo mfumbie mjinga, mwerevu..........
 
CCM Hoyeeeee!!!
Z
 
yn ndani ya miaka 4 ijayo viongozi weng sn wa ccm watakua wameiaga dunia kwa presha
 
Ikifika Mahali haki ikatendeka kila mahali wala hutasikia lawama wala maandamano. Tuombe Mungu awape hekima wale wenye mamlaka ya kuto haki ili nchi yetu iwe mahali salama pa kuishi.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Jeshi la polisi limepiga marufuku maandamano ya CCM ambao walitaka kuandamna ili kulaani vurugu za chadema Arusha. Marufuku hiyo inakwenda sambamba na marufuku ya maandamano ya chadema
 
Kazi ya polisi siyo kutoa au kunyima kibali. kazi ya polisi ni kulinda usalama wa raia, pamoja na kusimamia maandamano yanafanyika katika hali ya usalama.
 
Kibali cha Maandamano CCM wameomba kama geresha tu ili ionekane wote wamenyimwa na CCM wameheshimu amri ya polisi. Ni ujanja wa kitoto kiasi fulani na haulengi kuondoa tatizo bali kulilinda
 
Kibali cha Maandamano CCM wameomba kama geresha tu ili ionekane wote wamenyimwa na CCM wameheshimu amri ya polisi. Ni ujanja wa kitoto kiasi fulani na haulengi kuondoa tatizo bali kulilinda

CHADEMA wakikosa kibali cha polisi, watatumia nguvu ya umma itafanya kazi.
Duniani kote, haki haijawahi kushindwa na dhuluma hata siku moja.
 
Kuandamana ni haki ya kikatiba kikundi chochote cha watu wana weza kuwahalifu polisi kuwa tunaandamana polisi si kazi yao kuzuia ila ni kuweka ulinzi .Hao polisi kukataa maandamano kwani wao ni mahakama? Mpaka waseme kesi ipo mahakamani?
 
Hao ccm hawana lolote wanafiki tu, watakuwa wameambizana na polisi huo mpango ili ionekane kuwa polisi wakizuia ccm wanakubali ina chadema ni wabishi! Iko siku polisi mtaja gundua kuwa mnatakiwa kutumikia wananchi na sio watawala peke yao!
 
Hao ccm hawana lolote wanafiki tu, watakuwa wameambizana na polisi huo mpango ili ionekane kuwa polisi wakizuia ccm wanakubali ila chadema ni wabishi! Iko siku polisi mtaja gundua kuwa mnatakiwa kutumikia wananchi na sio watawala peke yao maana tawala hubadilika lakini wananchi wataendelea kuwapo!
 
Hawa CCM wanajifanya wajanja kumbe ni wapuuzi tu,hiyo nayo waliona giaaaa
 
Back
Top Bottom