CCM wananunua shahada za kupigia kura

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,412
Kuna taarifa tumepata kutoka sehemu mbalimbali hapa Arusha kuna watu wanapita wakishawishi watu wawauzie shahada za kupigia kura
najiuliza kama taarifa hizi ni kweli je ni njia mojawapo ya CCM kushinda tena 2015??
kama wanafanya hivi ina maana daftari la wapiga kura halitaboreshwa kabla ya 2015 ili waliopoteza vitambulisho vyao wapate vipya?
maswali ni mengi kuliko majibu,na kama hii ni mojawapo ya mbinu za awali je Chadema inalijua hili?
 
Uelewa wangu ni kwamba "watawala" wanakaratasi za kura ambazo wataziingiza kwenye masanduku ya kupigia kura wapatapo nafasi. Ili kura zisizidi idadi ya wapigakura walio jiandikisha njia rahisi ni kununua shahada za wapiga kura. Kwakua utamaduni huu umeshakomaa hapa nchini na kila kunapokua na uchaguzi nashauri chama cha upinzani kilichopo(Chadema) kupata msaada wa namna ya kudhibiti wizi wa aina hii na aina nyingine iliyopo. Kwa hakika bila jitihada za makusudi na utumiaji wa akili (sio kukesha kulinda maboksi tu) 2015 raisi ajaye atakua anaitwa Edward Lowasa.
 
Ndiyo maana daima nawaza kuwa ccm ni lazima iondoke madarakani na ni lazima ife, tusifanyane wajinga kwa upumbavu huu wa kukiuka sheria za nchi kwa makusudi ya kubakia madarakani wakati wananchi wamekwisha wakataa.
 
mbinu hiyo imepitwa na wakati,sana sana inasaidia mahali ambapo tofauti ya kura haizidi kura 100.kama wamepitwa na kura 6000 kama arumeru hata wanunue shahada 5000 bado watashindwa!
 
Arusha kuna makamanda wengi mnashindwaje kuwawekea mtego mkawabamba na kuwapa kisago cha nguvu ikawa fundisho maana hata mkiwapeleka polisi ni sawa na kumpeleka mgonjwa hospitali!!
 
Kam wananunua sasa ujue wamenusa kwamba rufaa ya Lema imejibu na uchaguzi pengine utarudiwa hapo AR!!!!
 
Uelewa wangu ni kwamba "watawala" wanakaratasi za kura ambazo wataziingiza kwenye masanduku ya kupigia kura wapatapo nafasi. Ili kura zisizidi idadi ya wapigakura walio jiandikisha njia rahisi ni kununua shahada za wapiga kura. Kwakua utamaduni huu umeshakomaa hapa nchini na kila kunapokua na uchaguzi nashauri chama cha upinzani kilichopo(Chadema) kupata msaada wa namna ya kudhibiti wizi wa aina hii na aina nyingine iliyopo. Kwa hakika bila jitihada za makusudi na utumiaji wa akili (sio kukesha kulinda maboksi tu) 2015 raisi ajaye atakua anaitwa Edward Lowasa.

nina imani uongozi wa chadema umepata hiyo taarifa,ni muhimu kafanyia kazi haraka iwezekanavyo
 
mada yako haiko sawasawa hao watu wanaopita na kukusanya shahada wanajitambulisha wanatokea chama gani? na wananunua shahada za wanachama wa chama gani? na hao wanaozinunua wanataka kuzifanyia nini? vinginevyo hayo ni mazungumzo ya kahawa.
 
Back
Top Bottom