CCM wanajidanganya kuwa Mbowe atang'ang'ania kugombea urais!

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,545
550
Ukizungumza na watu wa CCM, CUF, NCCF et al, wanasema CDM itabomoka maana Mbowe atalazimisha kugombea urais na chama kitagawanyika. Mimi simfahamu sana Mbowe lakini sioni kama atafanya hivyo. ningekuwa mshauri wa chadema ningesema demokrasia ipewe nafasi kubwa. Kama demokrasia isipohujumiwa, na maamuzi yote yakatokana na vikao, hakutakuwa na uwezekano wa migigoro. Dr Slaa anakubalika sana na kama Zitto na Mbowe watataka wagombee wasinyimwe. Kura za wanachama zipigwe atakayeshinda ndio apewe tiketi ya chama
 
tehetehe mbowe ndio wakati wake huu kugombea kama mlikuwa hamjui basi ndo hivyo mbowe ni presidetion candidae wa cdm
 
Wengine we hate majungu na sasa si muda wa majungu kuna watu Dodoma leo wamelala nje sijui kama watapona na wengine wamekufa ndiyo akili zetu ziko huko.Mawazo haya na wasi wasi peleka ofisi ya Chadema hapa ni JF
 
muda huu utumike kujenga chama na kuweka mazingira ya uchaguzi huru muda ukifika, lakini nani atagombea is another issue kuwe na katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ili huyo atakayegombea ashinde au ashindwe kwa haki sio ashinde au ashindwe kwa kugawa mahindi vitisho na mambo mengine bila kusahau wizi wa kura!!
 
tusiwe na mawazo hayo kwani ata viongozi wa chama hawafikiri haya unayoyafikiria. tunachokijua nakukiwaza na kukifanya ni kukijenga chamaa kwenye mising imara zaid na zaid ikifka 2015 serikali tuichukie, tafadhali embu akikisha wewe una kadi ya chama ongeza na wezako mia na hao mia waingeza wezao mia mia hapo ndipo utajua nguvu ya umma na tuachane na nguvu ya maneno.
 
Nadhani hizo ni hisia tu, kwakuwa huko CHADEMA hizo sarakasi za nani agombea hazipo, labda mtoa mada anataka kutuaminisha hayo. La mhimu hapa ni kuwa na mfumo bora wa uendeshaji nchi yetu. Tumsimjenge mtu bali tuimarishe taasisi na mifumo ya nchi iwe bora ili yeyote akiingia madarakani atufikishe tunapotaka, tukianza kuhangaika sijui Slaa, Mbowe, Sitta tutapoteza mwelekeo na nchi inakwenda
Na hiyo taarifa kuwa CCM wana hisia hizo umeitoa wapi?
 
Ukizungumza na watu wa CCM, CUF, NCCF et al, wanasema CDM itabomoka maana Mbowe atalazimisha kugombea urais na chama kitagawanyika. Mimi simfahamu sana Mbowe lakini sioni kama atafanya hivyo. ningekuwa mshauri wa chadema ningesema demokrasia ipewe nafasi kubwa. Kama demokrasia isipohujumiwa, na maamuzi yote yakatokana na vikao, hakutakuwa na uwezekano wa migigoro. Dr Slaa anakubalika sana na kama Zitto na Mbowe watataka wagombee wasinyimwe. Kura za wanachama zipigwe atakayeshinda ndio apewe tiketi ya chama
Ndugu, Mbona tumekuwa watu wa kuwaza next election tu! Uchaguzi umepita takribani mwaka mmoja! Tunachotakiwa kufanya sasa ni kufuatilia ahadi za walioshinda uchaguzi, Je Kigoma inakuwa Dubai? Je Airport zilizoahidiwa kujengwa zinajengwa? Je maisha yamekuwa Bora kwa kila Mtanzania? Hilo ndilo la muhimu kujiuliza kwa sasa! Sio nani atagombea next election!
 
mijadala ya namna hii waachie ccm wenye focus ya mwaka 1 hadi 5 na icho kimekua chanzo cha baadhi ya migogoro ndani ya ccm
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom