CCM Wanagawa Bendera Na Pesa Arumeru

Puppy

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,995
2,494
Leo Mida hii ya saa nne katika mitaa ya Leganga na Usa-River chama cha ccm kinagawa bendera na pesa kwa waendesha Toyo(pikipiki) na mikokoteni.

Bendera moja unagaiwa na shilingi elfu tano mpaka sabini kutokana Uongeaji wako. Wanafanya hivi ili kuongeza idadi ya watu kwenye mikutano yao ya Kampeni

Wanatumia gari aina ya Land Cruiser Nyeusi kufanya hiyo biashara.

Vijana wanapokea halafy wanasema "tunakula ccm, tunachagua chadema".
 
Acha uongo wako kama una ushahidi, note number ya gari, unajua namba za TAKUKURU wapigie then watakuja, ni vema na wewe ukajitambulisha kwao manake mtoa rushwa na mpokea rushwa wote wana kesi ya kujibu.
 
TAKUKURU? Acha utani bwana!
Labda red brigades
 
Acha uongo wako kama una ushahidi, note number ya gari, unajua namba za TAKUKURU wapigie then watakuja, ni vema na wewe ukajitambulisha kwao manake mtoa rushwa na mpokea rushwa wote wana kesi ya kujibu.

Mbona issue ya Sioi mliwamata wale jamaa na hakuna kesi? TAKUKURU ni kama imekufa na inafanya kazi kwa wapinzani tu.
 
Wakishatoka kwenye mikutano, hizo bendera wanazitupa.
Hamna kijana anayethubutu kuonekana na bendera za ccm kitaa!
 
Kama wewe umebakia kufuata sheria nchi hii utaumia. Sasa hivi ni kujichukulia tu sheria mkononi maana ni ukweli usiofichika kwamba Takukuru hamna kitu na polisi ndio kabisaa. Ukizingatia viongozi walioko madarakani ni wazee ambao wameharibu nchi na hawako tayari kuachia kwa amani. Kilichopo ni machafuko tu ndio sheria zitafuatwa na hapo vijana wataongoza nchi wakiwa na fikra mpya.
 
Acha uongo wako kama una ushahidi, note number ya gari, unajua namba za TAKUKURU wapigie then watakuja, ni vema na wewe ukajitambulisha kwao manake mtoa rushwa na mpokea rushwa wote wana kesi ya kujibu.

Mkuu sizushi wala nini, ni kweli kabisa. Nenda Tengeru sasa hivi utayaona. Wametoka leganga muda sio mrefu wanaelekea huko.
 
mkoa wa arumeru mashariki sio mkoa wa igunga nyie magamba. nasari juuuu zaidi.
 
TAKUKURU ni sawa na 0 hapa Nchini.

Tuna hasara kila idara ktk Nchi yetu!

Ila nina imani mwisho wao wa ubwenyenye kwa hawa mafisadi haiko mbali hata punje!

MUNGU TUSAIDIE!
 
semeni yote mwisho wake tar mosi April. Sina mashaka na Arumeru. Barcelona ikicheza na Kibangu united hata ukashifu, uwatukane ama uwazomee barca watashinda tu. Mtu anayetamani kuona CCM INAPOTEZA ASUBIRI SEHEMU NYINGINE SIO ARUMERU
 
Acha Porojo wewe
Mchakato unaoendelea Arumeru ni kitu cha msingi sana kwa watu wa Jamii hiyo, acha kabisa kupeleka maneno yako
ya bla bla zisizowasaidia wana arumeru kitu chochote.

Kinachofanyika hapo ni kitu kinachobeba mstakabali mzima wa elimu, afya, ardhi, uchumi na democrasia kwa Jamii hiyo
kongwe lakini iliyotopea kwenye Umasikini kwa sababu ya Uongozi Mbovu chini cha chama cha Magamba.

Sasa wewe unapoanza kuleta inferences za Barcelona sielewi kabisa dhamira yako kwa maendeleo ya watu hao. Mwenzako Mkapa Mzimu sijui Mzuka wa Nyerere umeanza kumuandama bado wewe. We Fanya siasa chafu tu huko tutakutana uzeeni.
 
semeni yote mwisho wake tar mosi April. Sina mashaka na Arumeru. Barcelona ikicheza na Kibangu united hata ukashifu, uwatukane ama uwazomee barca watashinda tu. Mtu anayetamani kuona CCM INAPOTEZA ASUBIRI SEHEMU NYINGINE SIO ARUMERU

acha kuidhalilisha timu ya barca kwa kulinganisha na magamba mlojichokea kwan mshabakiza mifupa tu but minofu kwisha.Kwa taarifa yako cdm inawagalagaza na hamtasahau ktk maisha yenu na 2015 ni kwa heri ccm hata kwa ngumi mtasepa tu,michezo yenu yoote mshalamba chini kwani hamjui kuongoza nchi mnajinufaisha wenyewe tu.Hv unafkiri ni mwananchi gani taahira wa kuchagua magamba kwa karne hii si tunawaoneni mlivyo goigoi,wababaishaji,matapeli na mafisadi tena kwa kushuhudia kwa macho yetu?Hatudanganyiki tena na ukae ukijua kuwa Joshua Nassari ndo mbunge wa Arumeru mash.Over!.
 
semeni yote mwisho wake tar mosi April. Sina mashaka na Arumeru. Barcelona ikicheza na Kibangu united hata ukashifu, uwatukane ama uwazomee barca watashinda tu. Mtu anayetamani kuona CCM INAPOTEZA ASUBIRI SEHEMU NYINGINE SIO ARUMERU

Mwigulu unasera gani zaidi ya kugawa pesa na khanga?
Kwa taarifa yako wameru ni werevu sana, pesa watakula, mikutano watahudhuria sana, kura kwa chadema.
Sisi tuna Mungu, Wao wana pesa tusiogope tutashinda!
 
semeni yote mwisho wake tar mosi April. Sina mashaka na Arumeru. Barcelona ikicheza na Kibangu united hata ukashifu, uwatukane ama uwazomee barca watashinda tu. Mtu anayetamani kuona CCM INAPOTEZA ASUBIRI SEHEMU NYINGINE SIO ARUMERU

Samahani

Mimi nikiona sura yako nataka kutapika:A S-frusty2:
 
Back
Top Bottom