CCM wamechanganyikiwa??

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,906
22,003
Hivi haya maandamano ya kila siku ya wana ccm wamechanganyikiwa ama nini
jamani tbc tumechoka kuwaona kama chama kina matapeli kwa nini usihame
nilitarajiaa maandamano haya yangeongozwa na watu wakiwa wanakusanya kadi za ccm

kwanini msichane hizo kadi na kuwatupia kwa makamba, kama mmemchoka hizo kelele azisaidii ndugu zanguni wale vichwa vyao anavijua nyerere mwenyewe so hapa ni ku act basi..........
 
Inasaidia kubadili historia. "Kwa mara ya 'kwanza' maandamano ya kupinga matokeo ya CCM yaliyofanywa na wanaCCM yalifanyika mwaka 2010. Maandamano hayo yakiwa na sura tata yalishindwa kubainisha umuhimu samaki wa kufurukuta ndani ya chungu cha moto wakati alikuwa na uwezo wa kuchoropoka kikaango....

Nawaza tu
 
Wataandamana sana kabla ya tarehe 15 maana wanajua ndio majina ya nani ni nani yatajulikana. Kuna waliotoa rushwa kama kawaida ya ccm na bado wakashindwa hivyo bado hawajakata tamaa. Sasa hivi wanashinikiza rushwa za maandamano ili warudishwe. Isitoshe baadhi yao walioangushwa ktk kura za maoni mametia kambi Dodoma kuijaribisha rushwa kwa vigogo kwani pale takukuru haisubutu kuwafuatilia kwa karibu. Kifupi ni hivi, siku ya kufa nyani miti yote inateleza. Ccm inachomwa mikuki ndani ya chama na nje ya chama. Msaada wao haupatikani tena maana wamechelewa mno kujirekebisha.
 
CCM! CCM! CCM! Shika hataamu! Nakumbuka zamani sana.....teh teh teh
 
Back
Top Bottom