CCM walipotua Njombe, Toa Maoni Yako.

Losambo

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
2,612
864
3.JPG

Msafara wa CCM huo kuelekea mkutanoni.

03.jpg

Nape akifanya vitu vyake Njombe.

08.jpg

Vijana wakimsikiliza Nape kwa makini

01.jpg

Picha hii ya mwisho naamini kama ingekuwa kwa CDM baadhi ya watu wangesema mbona tunaona watoto tu?

Nakaribisha maoni,
 
Tayari kiko kaburini, tunachofanya sasa ni kutupia udongo tu.

Sijui hiyo anayoendeshq Nape ni operation ipi? Licha ya kupata coverage ya kutosha lakini bado haina mvuto, na naona Nape anatekeleza kauli yake kwa matendo kuwa hata CCM akibaki peke yake haifi na sasa anajaribu kuikoa.
 
NA BASHIR NKOROMO, NJOMBE


KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, CCM, Nape Nnauye amewananga CHADEMA kwamba aliyewapa wazo la kuanzisha kauli mbiu ya 'Vua gamba vaa gwanda' amewaingiza 'mkenge'.


Alisema, Chadema wameingizwa mkenge kwa kuwa inajulikana wazi kuwa kaulimbiu hiyo ililianzishwa na CCM, kukisafisha chama kiondokane na mafisadi wa aina zote, na kwamba kwa Chadema kuanzisha 'vua gamba vaa gwanda' maana yake wanafanya kampeni ya kubembeleza watu wa aina hiyo wasiotakiwa CCM na Tanzania kwa jumla wahamie kwao.


Nape alisema hayo, jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mlangali, wilaya ya Ludewa mko mpya wa Njombe, akiwa katika ziara ya kikazi katika mikoa mbalimbali kuimarisha uhai wa chama.


"Itakumbukwa, CCM kwa kuwa ni chama halisi cha siasa kwa kutimiza sifa, kinaendelea na mageuzi makubwa ya ndani, yanayoitwa 'Kujivua Gamba', ikiwataka wale wote wanaojihusisha na ufisadi wa ina zote kuondoka ndani ya Chama. Lakini Chadema kwa kujua au kwa bahati mbaya wameamua kupotosha maana halisi iliyo wazi ya zoezi hili kwa kuanzisha operesheni eti ya 'Vua Gamba, Vaa Gwanda'", alisema Nape na kuhoji;


"Je, kwa maana hiyo Chadema kama wamedhamiria hivyo na siyo bahati mbaya, wamemua kuutangazia umma wa Watanzania na dunia nzima kwamba wako tayari kuwapa hifadhi mafisadi wa aina zote ambao ni tishio kwa ustawi wa taifa letu la Tanzania, ili mradi tu wapate idadi kubwa ya wanachama?".


Nape alisema, kama Chadema wangetumia busara wangeanzisha operesheni 'Vua Gamba vaa Uzalendo', kwa sababu hakuna ambaye angeshangaa, kwa kuwa kinachosababisha watu kuwa mafisadi ni kutokana na kukosa uzalendo ndani ya mioyo yao.


"Kumwambia mtu avue nguo ya ina moja avae nguo ya rangi nyingine huo ni upuuzi, maana aina ya nguo inaweza kuwa utambulisho tu, lakini haisaidii kubadili wala kujenga tabia ya mtu kiasi cha kuachana na ufisadi akawa mwadilifu na mzalendo kwa nchi yale toka moyoni, mtu anaweza kuivaa na kuivua wakati wowote, lakini kama watu wakihimizwa kuvaa uzalendo wakauvaa sawa sawa, watakuwa nao mioyoni mwao daima, na hawatauvua muda wowote kama nguo", alisema.


Nape alisema kutokana na hali hiyo Wana-CCM wadilifu wasiwe na wasi wasi kuhusu 'magamba' yanayohamia Chadema, kwa sababu kwa kujiingiza katika kuyaona 'magamba' ambayo yamekubuhu kwa ufisadi kuwa ni mtaji kwao sasa chama hicho kinajichimbia kaburi.


"Wewe umesafiri kwa muda mrefu na gari lako, ukaliona mwendo wake umeanza kuwa wa ndivyo sivyo, ukaamua kuondoa oil chafu kusafisha injini, sasa wakati unasafisha akatokea mtu kuikinga akidhani itamfaa, wewe una hasara gani? si unamuacha tu akahangaike nayo?, alisema Nape.


Katika mkutano huo ambao ulijaa watu licha ya kufanyika kijijini, Nape aliponda operesheni iliyoambana na 'vua gamba vaa gwanda' ya 'Momement for Change-M4C', akisema hiyo ni operesheni ya kukusanya fedha tu, wala siyo ya kuleta mabadiliko kama Chadema wanavyodanganya watu.


Alisema, ni operesheni ya kutafuta fedha, na ndiyo maana kila wanapoitangaza operesheni hiyo, wanachangisha watu fedha ambazo baadaye huwa wachangishwaji hawaambiwi ni fedha kiasi gani kimepatikana.


"Ukinunua kitu ukahitaji fedha iliyobaki si unasema nipatie 'chenji' yangu? sasa wananchi muwe macho, msidhani hiyo ni operesheni ya mabadiliko, ni operesheni ya wanaharakati kutafuta fedha, maana hata wao walishakiri kwamba Chadema ni chama cha harakati na sasa kinajaribu kujitoa kwenye uana harakati kiwe chama cha siasa cha kutafuta kutawala nchi" alisema na kuongeza;


"Lakini nawahaapia, hawa watakuwa wanaharakati kwa muda mrefu sana, itawachulua muda mrefu kuwa chama cha siasa kwa kuwa historia inathibitisha kuwa makundi mengi ya harakati yalichukua miaka mingi sana ndipo yakawa vyama vya ssembuse hawa,watakula fedha zenu mpaka mtachoka", alisema Nape.


Nape jana alitarajiwa kufanyika mikutano mingine ya hadhara katika mkoa wa Njombe kabla ya kujerea Dar es Salaam kwenye maandalizi ya mkutano mkubwa wa CCM wa wajumbe wa mashina, matawi na viongozi mbalimbali wa CCM na wanachama, utakaofanyika kwenye viwanjan vya Jangwani, Juni 9, 2012.
 
Sasa juu ya nini kuifanya Njombe kuwa wilaya wakati ina watu 60 tu? Nikijumlisha na hao watoto jumla 180 na Nape mwenye 181.

Na juu ya nini imekuja shule moja kwani shule zingine hazikutaarifiwa kwamba kuna mkutano wa kujazia jazia?
 
Suppose kila gari lilikuja na watu wawili kwenye msafara ina maana watu wa hapo hapo ni hao watoto tu?

Kweli ukimwi umeimaliza Njombe, mweh! Yaani wamebaki watoto tu hata walimu hakuna!
 
Watu nyomi. Hapa namaanisha watu wengi nikimaanisha watu zaidi ya mmoja
 
pesa za wizi zinawapa watu mbwembwe,mh, haya,najua vijana wa boda wamepata chao tayari,ila sasa,mkutani wake unawatoto kibao,au kwenye ilan ya nyinyiemu waliahidi kufanya mikutani ya watoto.maskini napeeeeeeee,angalia wasije wakakuachia mazishi ya chama mwenyewe!
View attachment 55578

Msafara wa CCM huo kuelekea mkutanoni.

View attachment 55579

Nape akifanya vitu vyake Njombe.

View attachment 55580

Vijana wakimsikiliza Nape kwa makini

View attachment 55581

Picha hii ya mwisho naamini kama ingekuwa kwa CDM baadhi ya watu wangesema mbona tunaona watoto tu?

Nakaribisha maoni,
 
Mbona hakuna picha inayoonyesha mkutano mzima? Hapo kuna watu wazima wanaonekana wamepanda juu ya mbao ili waweze kuona mbele, hii inaashiri kuwa si kweli kuwa kulikuwa hakuna watu, ila aliyeleta thread, kwa sababu maalum, ameamua kuleta picha nusunusu! Well, this is JF of today!
 
Back
Top Bottom