CCM walipanga kulichukua jimbo la Arusha Mjini Kilaini

CCM are so smart lakini chadema are smarter. Nilikuwa na mtu mmoja wa CCM akaniambia mission ilikuwa ni kumwekea lema pingamizi ili ccm wapite kilaini. Kwamba walimhukumu kwa kifungu batili ila jaji hakusema kama anaruhusiwa kugombea au la. Hata kama ilikuwa kosa la jaji lazima ukate rufaa kuliondoa. Kama Lema angedanganyika kugombea jimbo lingeenda kwa technicalities. CCM wanajua kwa kura hawawezi kushinda.
Siku ya Alhamisi, nilianzisha uzi wa ''Chadema na Lema lazima wakate rufaa kupinga hukumu'', nilishambuliwa sana, lakini nilisimama imara kuelezea ni kwa nini Chadema na Lema lazima wakate rufaa mahakama ya rufaa. Hoja hizi hapa:
quote_icon.png
By Atigi
Hukumu iliyotolewa ya kumvua ubunge Mh. Lema haikutarajiwa kwa kuzingatia mwenendo wa kesi. Katika hali hii ni lazima Chadema kwa kushirikiana la Lema wakate rufaa kupinga hukumu hii. Sababu za kupinga hukumu ni kubwa kiasi kwamba Lema kwa kusaidiwa na Chadema lazima wakate rufaa

Haki haikutendeka

Hukumu ya kumvua Ubunge Lema siyo ya haki kwa kuzingatia mwenendo wa kesi. Hakuna ushahidi iliotolewa ambao haukuacha shaka yoyote kuwa Lema alitenda kosa la kumtukana Batilda. Na hata kama ushahidi usingeacha shaka yoyote hicho kinachoitwa tusi si kosa la kumvua ubunge Lema. Mwanasiasa yoyote anayegombea inabidi mwenendo wake wa maisha uhojiwe li kuona kama anaweza kushika madaraka ya kisiasa. Hata kama ushahidi mzito ungeonyesha kuwa Lema alidodosa maisha ya mgombea, hiyo haiwezi kuwa kosa la kumvua Ubunge. Wote tunatambua namna maisha ya wagombea wa Chadema yanavyohojiwa wakati wa chaguzi Mbalimbali, za ubunge na uraisi. Na hii ni haki kwa wananchi kujua, siyo kosa. Pamoja na mapungufu ya kutungwa kwa kosa, pia hakuna uthibitisho wa nguvu wa hicho kinachoitwa kosa kuwa Lema alikifanya. Ni ushahidi wa kutunga wa maneno, hakuna ushahidi wa maandishi wala sauti katika mkanda wala CD kuwa Lema alitoa matamshi yaliyotungiwa mashitaka

Kutekeleza M4C (Movement for change)- Vuguvugu la mabadiliko
Chadema lazima kielekeze vuguvugu la mabadiliko la M4C lililozinduliwa huko Arumeru katika maeneo yote. Kwa wananchi, kwa wabunge, kwa wana-CCM na katika mhimili wa Mahakama. Kwa sasa, Chadema kimpatie Lema kazi ya kutekeleza mikakati ya M4C wakati rufaa ya kupinga hukumu imekatwa. Lema hatakosa kazi ya kufanya katika chama wakati kesi ya rufaa inaendelea au wakati wa kusubiri kupangiwa kesi. Lema hana cha kupoteza kwa kukata rufaa kwa sababu tangu alipoamua kujiunga na Chadema alijiunga siyo kwa ajili ya kutafuta ufahari au mali bali kusaidia kuondoa ukandamizaji wa CCM. Ndiyo maana alikubali kukaa mahabusu ili kupinga ukandamizaji wa Polisi. Watanzania wote wanaojiunga na Chadema wanachagua kutetea wananchi, wanamapenzi na nchi yao na hawakimbiliii mali, wanaokimbilia mali za kifisadi hujiunga na CCM. Wanaojiunga na Chadema ni watu ambao wameweka rehani hata maisha yao wenyewe kwa ajili ya kuitetea na kuilinda nchi yao dhidi ya ufisadi na dhuluma ya CCM na serikali yake.

Kutathmini mhimili wa Mahakama
Kwa kukata rufaa Chadema kitaweza kutathmini mwenendo wa mhimili wa mahakama. Tunataka kujua kama jaji Gabriel Rwakibarila aliyetoa hukumu ametumiwa na CCM na serikali yake kama yeye binafsi au imehusisha mtandao wa majaji wengine katika mhimili wa mahakama. Tunajua kuwa kuna wanasheria ambao wamekuwa wakitumiwa na wanasiasa mafisadi kuhujumu uchumi wa nchi kwa kusaini mikataba ya kifisadi. Mikataba yote ya kifisadi imehusisha wanasheria wasiokuwa na uchungu na nchi yetu. Tumejua kwa mwenendo wa kesi ulivyokuwa kwamba jaji huyo ametumika na CCM kutekeleza azima yao. Tunajua jinsi Lema alivyokuwa mwiba bungeni kwa waziri wa mambo ya ndani na pia waziri mkuu pinda na jeshi la polisi. Siyo ajabu kwa CCM na Serikali yake kumtumia huyo jaji ili kumkomoa Lema na Chadema. Kwa Chadema kukata rufaa wananchi tutajiridhisha kama muhimili wa mahakama utalinda hadhi yake kwa kutengua hukumu hiyo isiyo ya haki. Kama itaibariki tutakuwa tumetambua tatizo kwa ujumla wake na kuwatambua kwa majina majaji wanaoshiriki katika kuua demokrasia na hivyo kuwa target ya M4C. Tunaamini kuwa mahakama ya rufaa italinda hadhi yake kwa kutengua humu hiyo isiyo ya haki ili mhimili wa mahakama na taaluma ya sheria visidhalilishwe.

Kutunga sheria zenye hadhi
Kwa kutata rufaa, Chadema na Lema watakuwa wamesaidia wananchi kukataa sheria dhalili. Maana kwa kuiacha hukumu hiyo kama ilivyo, itaingia kwenye kumbukumbu za sheria na hivyo kuwa sehemu ya nukuu katika taaluma ya sheria na katika muhumili wa mahakama. Tunataka Chadema ifanye kwa vitendo kukataa sheria za ovyoovyo na hasa tunapoelekea kutunga katiba mpya.
 
CCM are so smart lakini chadema are smarter. Nilikuwa na mtu mmoja wa CCM akaniambia mission ilikuwa ni kumwekea lema pingamizi ili ccm wapite kilaini. Kwamba walimhukumu kwa kifungu batili ila jaji hakusema kama anaruhusiwa kugombea au la. Hata kama ilikuwa kosa la jaji lazima ukate rufaa kuliondoa. Kama Lema angedanganyika kugombea jimbo lingeenda kwa technicalities. CCM wanajua kwa kura hawawezi kushinda.
CCM HI MANYANI MAKUBWA YASIYOTUMIA UBONGO,MWISHO WA SIKU WATAKOJOLEA PUANI,MIM NIACHE NILIVYo!!!!!!!!!!!!!!!!
 
CCM are so smart lakini chadema are smarter. Nilikuwa na mtu mmoja wa CCM akaniambia mission ilikuwa ni kumwekea lema pingamizi ili ccm wapite kilaini. Kwamba walimhukumu kwa kifungu batili ila jaji hakusema kama anaruhusiwa kugombea au la. Hata kama ilikuwa kosa la jaji lazima ukate rufaa kuliondoa. Kama Lema angedanganyika kugombea jimbo lingeenda kwa technicalities. CCM wanajua kwa kura hawawezi kushinda.
walisharuka majaji 3 baada ya kugundua siri ya magamba huyu wa sumbawanga alipewa chake mambo ikaisha!!
 
cdm naikubali ila lema sina imani naye naona kama uwezo wake wa akili uko chini ya kiwango
 
Back
Top Bottom