CCM waliombe radhi taifa kutokana na matusi ya Silinde

lakini wakuu...huyu dagaa tutakuwa tunamuonea tu. huyu kafuata nyayo za papa - aka mkapa.

mkapa kuanzia day 1 ya kampeni alitoa tusi zito ambalo sidhani kama lina tofauti yoyote na haya ya huyu bwana-mdogo. literally alimwita mtoto wa mtu (vincent nyerere)eti ni "bastard" , hilo ni tusi dogo?

tuanze na huyu chinga nkapa kwanza!!
ndiyo maana nawaza ya kwamba hapa CCM taifa ionyeshe heshima mbele ya watanzania kwa kusimama mbele ya vyombo vya habari au katika mikutano kama ile kuliomba radhi taifa kutokana na matusi waliyotutusi.
 
Sorry, I meant Lusinde (please ignore the name in the title)

Nimeisikiliza na kusoma baadhi ya matusi aliyoyatoa Lusinde kwa viongozi wa CHADEMA nchini, nimesikitika sana, nimefadhaika sana na nimefedheheshwa sana kwa chama chenye heshima kama CCM kusimama mbele za watu: akina mama, akina baba, watoto, vijana, mtu na mwanae, mtu na mkwewe nk waliokuwepo kwenye mkutano na kuongea maneno kama yale.

Kwa ajili ya kujenga harmony kati yetu, nadhani ni busara sana kwa CCM taifa ikiongozwa na mwenyekiti wake, kuliomba radhi taifa na wanameru wote waliodhalilishwa mbele ya watoto wao, wakwe zao na wazazi wao. Kushindwa kufanya hivyo, kutamaanisha kwamba Kikwete, Mkama, Nape, Makamu wa Rais, waziri mkuu, na baraza lote la mawaziri kwa pamoja wamekubaliana kutoa kauli kama hizi mbele ya jamii ya kitanzania, ambazo ni kinyume na maadili ya mtanzania na mwafrika kwa ujumla.

Napendekeza wana JF, tuwape CCM muda kamili wawe wameomba msamaha, la sivyo hatua makini zilichukuliwe dhidi ya chama hiki.
maneno gani mkuu we nukuu tu
 
Mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kukubaliana na kilichofanywa na lusinde.

Unless huyo mtu ana akili ya maiti aliyevishwa suti
 
Mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kukubaliana na kilichofanywa na lusinde.

Unless huyo mtu ana akili ya maiti aliyevishwa suti
Yafaa hatua stahiki zichukuliwe, maana kwa mwenendo huu ni aibu kubwa kwa taifa
 
Nani wa kuchukua hatua stahiki?
Uongozi wa juu wa CCM unapaswa kuchukua hatua stahiki, ambayo kubwa kuliko zote ni kusimama mbele ya umma na kuuomba radhi. La sivyo basi viongozi wa chadema wachukue hatua kutokana na kuvunjiwa heshima yao mbele ya watu. Hawa akina lema, slaa, mbowe na wengineo ni watu wazima wenye familia zao, ni aibu ilioje kwa watoto wao kusikia kauli kama hizi dhidi ya wazazi wao?
 
..sijui lakini. Maana nikikukumbuka hata JK alishawahi poromosha vimatusi vingi tu mfano:
  1. ....ni viherehere vyao
  2. ..........n.k
 
Mods badilisha title
Sorry, I meant Lusinde (please ignore the name in the title)

Nimeisikiliza na kusoma baadhi ya matusi aliyoyatoa Lusinde kwa viongozi wa CHADEMA nchini, nimesikitika sana, nimefadhaika sana na nimefedheheshwa sana kwa chama chenye heshima kama CCM kusimama mbele za watu: akina mama, akina baba, watoto, vijana, mtu na mwanae, mtu na mkwewe nk waliokuwepo kwenye mkutano na kuongea maneno kama yale.

Kwa ajili ya kujenga harmony kati yetu, nadhani ni busara sana kwa CCM taifa ikiongozwa na mwenyekiti wake, kuliomba radhi taifa na wanameru wote waliodhalilishwa mbele ya watoto wao, wakwe zao na wazazi wao. Kushindwa kufanya hivyo, kutamaanisha kwamba Kikwete, Mkama, Nape, Makamu wa Rais, waziri mkuu, na baraza lote la mawaziri kwa pamoja wamekubaliana kutoa kauli kama hizi mbele ya jamii ya kitanzania, ambazo ni kinyume na maadili ya mtanzania na mwafrika kwa ujumla.

Napendekeza wana JF, tuwape CCM muda kamili wawe wameomba msamaha, la sivyo hatua makini zilichukuliwe dhidi ya chama hiki.
 
..sijui lakini. Maana nikikukumbuka hata JK alishawahi poromosha vimatusi vingi tu mfano:
  1. ....ni viherehere vyao
  2. ..........n.k
Mmmh, kumbe ni vitabia vyao eeh!! Lakini kwa hili nafikiri viongozi wa CHADEMA wasinyamaze iwapo CCM haitaomba radhi.
 
...ni hatari sana. Kuna jamaa yangu alinisimulia kilichowasha moto mauaji ya Burundi ni kauli ya aliyekuwa wazirim mkuu. Baada ya mapinduzi fake ya wanajeshi wachache yule mama wakamuomba wafanye mazungumuzo kwani waliokuwa wameasi walikuwa wachache na hawakuwa na nguvu ila wenye nguvu walikuwa pembeni wanasikilizia, yule mama akasema tu kauli moja "siwezi kuongea na wauaji" hiyo kauli ikaigharimu nchi. Wachambuzi husema labda angeweza kuongea nao inawezekana wangefikia muafaka. Ndiyo huyu lusinde (L=herufi ndogo kumuondolea sifa ya utanzania) anachochea chuki kati yetu watanzania. Natamani kaka William aje amg'oe 2015. Nipo tayari kumuunga mkono!
 
Ng'wanakidiku, hawa watu huwa wanajisahau sana wakiwa madarakani. Ndiyo mantiki pia ya signature yangu hapo chini. Wakishaona wana jeshi basi wanadhani wapo salama kuzidi usalama. Ila kwa kweli kama jeshi nalo halitafika mahali fulani likawahurumia watanzania na kuamuaa kuipoka nchi kutoka mikononi mwa hawa mbweha, tutapata shida sana. How dare on the earth mtu atukane matusi makubwa kama yale halafu aendelee tu kudunda mitaani. Ningekuwa mimi ni Mbowe ningeshaandaa kundi la kumfunza adabu huye *****, wala nisingemwacha. lakini kwa sasa nafikiri hili sasa liwe kwenye level ya chama. Shutuma kipewe chama kwa sasa.
 
kabla ya kumuondoa kwenye timu yao ya kampeni ilibidi wamuache awaombe radhi watanzania kupitia hukohuko Arumeru. Hawajachelewa kwani wana kama siku mbili au tatu hivi zimebaki. This is too much matusi haya ni ya nguoni kabisa na wala si utamaduni wetu
 
kwakweli kama unasema Lema alipata bwana magereza, Dr. Slaa ni kama amejinyea, huyu jamaa inabidi akapimwe akili... ila nashukuru ccm wamemsimamisha uana chama kwa kuda usiojulika.. labda tuangalie maana JK ameingia jioni hii kwa kwandege ya serikali .. naye atakuwa na jipya? au naye ni utoto na pumba ataongea? JK atahutubia wana Arumeru kesho katika kufunga kampeni..........
 
Back
Top Bottom