CCM walalamika kuchewezewa rafu utoaji wa maoni

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=1]
DSC_0367.JPG
[/h]Written by administrator // 08/07/2012 // Habari // 2 Comments


Salma Said,
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimeitaka tume ya katiba kuchukua hatua dhidi ya watu wanaofanya vitendo vya udanganyifu kwa kuwasilisha barua za maoni kwa tume hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari huko Dunga Mkoa wa kusini Unguja Katibu wa CCM wa mkoa huo, Zainab Shomari alisema kumeanza kujitokeza vitendo vya udanganyifu wa watoaji maoni kwa kutumia majina bandia kwa wawasilishaji.
“Kuna jina la Said Mwema limejitokeza katika barua na baada ya barua hizo tume ilitaka kumjua huyo mtu anayeitwa Said Mwema lakini matokeo yake hakuna aliyejitokeza, kwa hivyo sisi tuna mashaka na hao watu wanaokwenda kupeleka maoni kwa njia ya barua tukiamini kuwa zinaandaliwa na baadhi ya wanasiasa” alisema Zainab.
Akivitaja vitendo vyengine vinavyofanywa katika mchakato huo, Zainab alisema ni pamoja na kuzomeazomea vilivyofanywa na vyama tofauti vya siasa, kuwatumia wanafunzi kutoa maoni baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa walimu wao pamoja na baadhi ya wanasiasa kuwaongoza wafuasi wao na kuwaelekeza maneno ya kwenda kutoa katika tume hiyo.
Katibu huyo alisema awali zoezi la utoaji maoni lilikuwa likiendelea vizuri lakini katika siku za hivi karibuni kumeanza kujitokeza vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakisimama kutoa maoni hali ya kuwa sio wakaazi wa maeneo husika.
“Kwa nyakati tofauti wananchi wa maeneo ya Mzuri na Mtende wameshuhudia baadhi ya wazanzibari wa kutoka maeneo mengiwakifurika huko kwa lengo la kutoa maoni mbele ya tume hiyo kinyume na taratibu za nchi” aliwaambia waandishi wa habari.
Katibu huyo alisema kwamba baadhi ya wazanzibari hao bila ya kigugumizi wala khofu “wakaanza kuandika mami ya barua za kughushi na hatimae kuziwasilisha mbele ya tume ya jaji Warioba ili zikubaliwe na kuyafanya ni miongoni mwa maoni yaliyotolewa na wananchi wa vijiji hivyo”.
Akitoa ushuhuda wa matukio hayo Katibu huyo alisema Kizimkazi Dimbani baada ya kutokea hayo Dk Salim Ahmed Salim alitoa karipio kali dhidi ya wavunjaji wa sheria ambapo wananchi wa kijiji cha Bwejuu na vijiji virani walikuwa wakishuhudia vitendo hivyo.
“Tume ya katiba ililazimika kusitisha zoezi hilo ili kutumia muda huo kwa kutoa ufafanuzi kwa wananchi juu ya kitendo hicho cha kihuni na atimae kuwataka waachane kabisa kuendelea kuvifanya kwa vile havina hatima nzuri kwao na wala taifa” alisema Zainab.
Aidha alisema baadhi ya walimu katika kijiji cha Bwejuu wamejitokeza baadhi ya walimu wa skuli za serikali wanaowashawishi wanafunzi wao kwenda kutoa maoni kwa matakwa ya walimu hao. Chama hicho kimesema kinaalaani vitendo hivyo vinavyokwenda kinyume na sheria pamoja na kuitaka tume iwe macho na vitendo hivyo na wasisite kuchukua hatia za kisheria dhidi ya wale wote ambao wana lengo la kuharibu zoezi hilo.
“CCM inatoa wito kwa wanachama na wapenda amani, utulivu na maendeleo ya taifa letu wa maeneo yote ya mikoa ya Zanzibar kuwa macho na wale wote wenye lengo la kuvuruga kwa makusudi zoezi hili, kwa kuwatolea taarifa mbele ya vyombo vya dola, ili sheria ichukue mkondo wake didhi yao” alisisitiza Zainab.
 
Wasiwachezee watanzania kama wanavyotaka kwani hao ccm ndio nani?dhaifu wa kubwa hao kulalamika tu hawana maana
 
Anatia aibu kulalamika kwamba baadhi ya watu wanatolea maoni mahali wasipoishi. Kwani sheria inamtaka kila mtanzania kutolea maoni pale anapoishi tu? Naona huyu anachanganya kati ya kupiga kura na kutoa maoni
 
Mwanzo kulitolewa shutuma kuwa Haroun Ali Suleiman na Samia suluhu Hassan, mwakilishi na mbunge wa Makunduchi, walihusika na shutuma hizi. Katika kujitetea kwenye Baraza la Wawakilishi, Haroun alisema:
"Mheshimiwa Naibu Spika nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii ya kukanusha uvumi ulioenea sehemu mbali mbali na katika mitandao na ujumbe wa simu ambao hata wawakilishi wenzangu hapa wanao ujumbe huo kuwa mimi nahusika na utayarishaji wa barua kwa kweli niseme sio kweli suala hilo na mimi sihusiki kabisa" alisema Haroun
Sasa CCM hao hao wanawalaumu watu wengine kuhusika na udanganyifu kama huo.
My take: Kodi za Watanzania zimepotea bure katika mchakato huu wa Katiba Mpya. Baada ya yote kumalizika, watasuka ripoti wanayotaka wao na kwa mara nyengine tena Watanzania kutiwa changa la macho kuhusu Katiba na Kero za Muungano.
 
Back
Top Bottom