taffu69
JF-Expert Member
- Feb 26, 2007
- 2,094
- 538
Mwaka wa fedha 2011/12 taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya serikali inaonesha ilikuwa zaidi ya asilimia 98 ya malengo yaliyokusudiwa lakini jambo la kushangaza na la kusikitisha ni kuwa hakuna wizara ama idara ya serikali iliyopata mgawo wa fedha za matumizi kwa kiwango kinachozidi asilimia 60 ya bajeti.
Kama ni mtu unaefuatilia na kutafakari ni lazima ujiulize hizo fedha zilizokusanywa zilielekezwa wapi, kwa matumizi gani na kwa idhini ya nani. Mlipaji Mkuu wa Serikali ambaye ni Katibu Mkuu Hazina anatakiwa aweke wazi/atoe ufafanuzi juu ya hilo pamoja na hizo tuhuma za CCM kujichotea kwa ajili ya kugharamia shughuli zao za chama.