CCM wakishirikiana na Jeshi la Polisi Tanga wamewanunua ndugu wa Marehemu Ally

uhai wa mtu hauna bei.
wewe ulitakaje labda??

1. Nakubali kaka ila kuna implied cost ya kupoteza mtu na kumuhifadhi (kuzika) kwenye familia.....haiishii kutoa laki saba kwa kwenda kuzika na kurudi morogoro tuu......hakuwa na familia....as in mke na watoto??? Mjane??? na kadhalika.... simaanishi familia ilelewe na chama la hasha ila je huo mchango ndo mwisho wa kumuenzi marhum kwa aina ya kifo chake???

2. Sasa hao waliomnunua (kama ni kweli) wametoa mchango say wa 5M rationally ni lazima ndugu wachukue huko unless ni familia well established and conscious enough to weigh the social, psychological and political value ya kukaa upande mmoja.....but huyu alikuwa muuza magazeti and this tells a lot on family and class he belongs.....nadhani hili walitakiwa kuliona hao walioshughulikia hii kitu na kama hawakuliona then hii ndo cost yake

3. Jana kulitoka uzi hapa ukipendekeza mmoja kati ya bigfishes aende kuzika ili kuweka uzito na sound political impact....sijasikia hilo kufanyiwa kazi mkuu.....sasa hao waliomnunua huyo the so called shemeji wakituma a remarkable figure pia tutahitaji uzi.....au tutalalamika kuwa fulani kaacha ofisi ya umma kwa jambo la kisiasa????

Nasisitiza tena uhai hauna price tag.....and thus there is no compensation but there are ways in which one can sugar-coat the bitter truth...............na hivi ndivyo ambavyo ningeshauri mimi mkuu....

Halafu swali la wewe ulitakaje sio a good probing skill ni kama unataka mtu ashindwe ili status quo i-prevail....as mimi na wewe hatuwezi kuwa na matakwa katika hili jambo.......
 
Pesa inafanya watu wasaliti misimamo yao.Hizo pesa alizohongwa shemeji mtu atazifanyia ukahaba tu
 
Hii siyo karne ya 19. Na watanzania wa sasa sio wale wa miaka ya 1940. Nape na ccm yake wanachofanya ni kujaza maji kwenye gunia na kamwe haliwezi kujaa. Kamanda Ally leo hii angepewa uwezo wa kufungua macho na kuwaona ccm na huyo ndugu yake aliyerubuniwa wanapanga mipango ya kidhalimu dhidi yake angepiga yowe na kuwatoa baru, ila kwa kuwa hayuko duniani ndo wanafanya mambo ya kipuuzi kama haya. Hakika mambo ya kidhalimu mnayoyapanga gizani iko siku yatakuwa hadharani. Kamanda Ally Mungu aiweke roho yako mahali pema peponi.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Ni lini tutapata mashujaa wa Chadema kutoka JF? Mpo watu kazi yenu kushabikia maafa kwa kisingizio cha M4C basi tunataka kusikia angalau Mwita Maranya au Molemo wamevunjwa miguu kwa ukereketwa wa M4C sio kila siku kuwatia watu wengine kwenye maafa na pengine wala hawaelewi nini maana halisi ya hiyo M4C.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Hizi siasa za nape na c.c.m zinazowagawa watanzania washiriki msiba zitalibomoa taifa. Na zaidi ni kwamba siasa za kibaguzi zinazofanywa na c.c.m zitawagawa hata wao 2015. Mtakumbuka maneno haya maana munatanguliza ubaguzi badala ya utaifa. Kuna ubaya gani watu kushirikiana msiba mpaka msemaje wa familia aseme munatufuatafuata nini wakati tunafahamu kwamba misiba huwa tunashirikiana. Mbona hata kikkwete anahudhuria misiba ya wapinzania na kutoa hotuba nzuri za kitaiofa? Nini kimetokea kwa familia hii kama si kuingiza siasa kwenye msiba
 
Huyu shemeji kwa kuoa ama kwa kuolewa?
Inaonekana huyu msemaji ni intruder kwenye hii familia.
Shemeji! Shemeji! Tafakarini hapa.
 
Habari za hivi punde kutoka Tanga zinadai familia ya ndugu wa Marehemu Ally aliyeuawa na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro wakati wakizuia Maandamano ya CHADEMA imeitisha mkutano na Waandishi wa Habari muda si mrefu na kudai kuwa CHADEMA Imesusia kushiriki katika msiba huo. Ukweli ni kwamba ndugu wa Marehemu hasa Shemeji yake alikubaliana na Viongozi wa Chadema kuwa wangetoa laki saba 7 ya kukodi gari la kusafirisha mwili wa Marehemu na Ndugu wa Marehemu na kuwarudisha Morogoro. Ghafla Shemeji huyo akakata mawasiliano na kupewa gari na watu wanaoaminika kuwa ni CCM na ndiye aliyefanya Press.

Inadaiwa huu ni Mkakati wa Nape na Propaganda zake za Udini na Ukanda. Watashindwa kwa hila zao na kwa maovu yao

huu ni uzushi wa kupindukia tunachofaham ally kijana wa kiislam ameuawa na vijana wenye rohombaya na wakatili wa cdm maandamano ya chadema ccm imeingia vipi chadema bebeni msalaba wenu
 
Kawaida ya CDM,hata igunga walimwambia mgombea wao akatafute hela za kesi,wao wakasepa. Ni tabia yao kutumia vijana kwenye siasa zao chafu na kuwatosa wakimaliza kazi nao. Hela inatumika kwa wakubwa wa chama tu, tena wa huko kwao.
Ukiona Police na serikali yake wanaogopa zali la wananchi ujue hakuna mbuzi wa kudanganywa Polisi limewachwea
 
huu ni uzushi wa kupindukia tunachofaham ally kijana wa kiislam ameuawa na vijana wenye rohombaya na wakatili wa cdm maandamano ya chadema ccm imeingia vipi chadema bebeni msalaba wenu
IGP Mwema ndio mwenye roho mbaya kazi kanenepa tumbo tuu anaendesha jeshi la mauaji,IGP gani ataruhusu ujinga wa aina hii wananchi wamehojiwa pale kila mtu kasikia leo wanakuja na propaganda za kuficha ukweli kama wana nguvu wako juu ya sheria wanaogopa nini kwenda kuzika haraka haraka hiyo si ni police case tunataka watuonyeshe ripoti ya postmortum nani alikuwepo nani alihudhuria tujue ukweli
 
Siku hizi mpaka msiba ni Dili-Kama CDM wamesema watagaramia laki Saba ccm wakasema watagaramia million Saba huoni gape kubwa hapo?? Mfiwa kachagua kondoo alionona ila it's shameless kupiga Dili maiti jamani

kama simba na yanga kwenye swala la Mbuyu...kuna taarifa nimezipata kuwa viongozi wa cdm wameshiri mazishi...
 
Kawaida ya CDM,hata igunga walimwambia mgombea wao akatafute hela za kesi,wao wakasepa. Ni tabia yao kutumia vijana kwenye siasa zao chafu na kuwatosa wakimaliza kazi nao. Hela inatumika kwa wakubwa wa chama tu, tena wa huko kwao.

Wakili wa kesi hiyo kwa mlalamikaji Prof. Safari ulimlipa wewe?
 
Itakuwa cdm hawakutoa msaada wa kutosha, ni kawaida ya cdm kuwatumia vijana alafu kuwa tosa , wanawafanya kama kondomu wakiwatumia wanawatupa wanahamia sehemu nyingine .
 
Bila shaka shemeji alitishiwa kupelekwa kule.............alikookotwa Dr. Uli kama asingetoa ushirikiano huo mchafu wa kukisafisha chama cha magamba. Haisaidii ukweli ni ukweli tu hata ukifukiwa nae Mungu atafukiwa?
 
damu ya mtu huwa haiendi bure tutasikia tu ukweli utakuja onekana hizo hizo pesa kama kweli wamepewa na ccm zitawagombanisha utaona
 
Back
Top Bottom