Elections 2010 CCM wakishindwa chaguzi hii kutukabidhi mali walizotupora ndani ya miezi sita

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Habari zilizonifikia hivi punde zinalonga ya kuwa wataalamu ndani ya Chadema wanaendelea kukusanya takwimu za mali ambazo CCM imelipora taifa hili masikini na chama hicho kongwe kuutumia mali dhalimu tajwa kama mtaji wa kuvifunika vyama vinginevyo vya siasa.

Baadhi ya mali ambazo zinazungumzwa kwa uchungu sana ni pamoja na fedha taslimu, majengo, miradi, viwanja vya mpira n.k

Haya yatakapofanyika usishangae kumsikia JK, Mkapa na Mzee Ruksha wamehamia Chadema wakitegemea kuna ulaji huko.

Yale yaliyowakuta Kanu huko Kenya wakajikuta hata KICC wamenyang'anywa sasa kukisibu CCM miezi sita tu baada ya Bunge kuupitisha muswada utakaoletwa bungeni na Waziri mtarajiwa wa Sheria na mambo ya kikatiba Bw. Lissu ambaye ushindi wa jimbo lake la uchaguzi sasa ni "foregone conclusion" yaani hakuna utata tena.........
 
Actually ndio maana tunataka kuchukua nchi!
Hizi fedha za kampeni ni za wananchi wote, wala si za CCM ni uongo wa mchana kweupe!
Wakae wakijua kuwa kuanzia 1/11/2010 hawana kitu...tutaanza pamoja 'square one'
 
Wasisahau viwanja vya mpira kama sokoine mbeya na smaora iringa
 
Habari zilizonifikia hivi punde zinalonga ya kuwa wataalamu ndani ya Chadema wanaendelea kukusanya takwimu za mali ambazo CCM imelipora taifa hili masikini na chama hicho kongwe kuutumia mali dhalimu tajwa kama mtaji wa kuvifunika vyama vinginevyo vya siasa.

Baadhi ya mali ambazo zinazungumzwa kwa uchungu sana ni pamoja na fedha taslimu, majengo, miradi, viwanja vya mpira n.k

Haya yatakapofanyika usishangae kumsikia JK, Mkapa na Mzee Ruksha wamehamia Chadema wakitegemea kuna ulaji huko.

Yale yaliyowakuta Kanu huko Kenya wakajikuta hata KICC wamenyang'anywa sasa kukisibu CCM miezi sita tu baada ya Bunge kuupitisha muswada utakaoletwa bungeni na Waziri mtarajiwa wa Sheria na mambo ya kikatiba Bw. Lissu ambaye ushindi wa jimbo lake la uchaguzi sasa ni "foregone conclusion" yaani hakuna utata tena.........

Na UNIP ya Zambia
 
Back
Top Bottom