CCM wajiwekea doa kwa wananchi wa Arumeru Mashariki

MAN OF CHANGES

JF-Expert Member
Jan 9, 2011
507
191
Baada ya kifo cha mbunge wa Arumeru Mashariki Jeremia Sumari katika hali ambayo wananchi wa jimbo hilo hawakuitegemea serikali jimboni hapo wiki hii iliyokwisha wamekuwa bize kutengeneza barabara inayoanzia eneo la Sanksi karibu na soko Tengeru inayoelekea kijiji alichotoka marehemu.

Wananchi wanahoji ni kwa nn ichimbwe na kufanyiwa marekebisho baada ya msiba kutokea? Na mbaya zaidi imechimbwa na kurekebishwa hadi nyumbani kwa marehemu tu,"Je sisi wa milimani zaidi hatuna haki ya kufikiwa na hiyo barabara"?

Alihoji mwananchi mmoja akiwa anazungumza na wengine ndani ya daladala. Jambo hilo limeibua hasira na chuki kwa wananchi wengi hasa kipindi ukarabati huo ulivyofanyika na sehemu ulipoishia.

UNADHANI KWA HILI CCM INA NAFASI NZURI YA KULITETEA JIMBO HILO AMBALO MWAKA JUZI KTK UCHAGUZI MKUU LILIKUWA NA UPINZANI SANA KUTOKA KWA MGOMBEA WA CDM KIJANA NASSARI?
 
hivi hawa magamba hawawezi kufikiri impact ya mambo wanayofanya kabla hawajatenda????????tunasubiri kampeni
 
Magamba wamepofushwa na shetani. Sasa hivi hawajui jambo la maana na lipi na walitende lini.
 
Hv cdm mbona uungwana mdogo 2zike kwanza,lkn hata hivyo ccm hamna jimbo atakaliachi ktk chaguz ndogo mpaka 2015
 
Vita vya kisiasa imehamia Arusha, jimbo hilo litakuwa gumu na si kama watu wengi wanavyifikiria.

Arusha si kama Igunga, uchumi na itikadi ya Igunga ni tifauti na wana Arusha. Huu ni mwanzo mengi yatakuja.
 
Hiyo si kwa ajili ya Marehemu........ni kwa ajili ya Mh Rais JK kwa taarifa yenu hapo inatumika kanuni ya non- contradiction...

.............washukuru hata hiyo itakayoishia kwa Marehemu itawasogeza..............kujongea milimani.........na wao ndio wale jeuri yao walitegema nini miaka yote hiyo kuendelea kuchagua chama kisichowajali...............na kwa nini wasubiri hadi Mbunge amekufa ndio waanze kudai kufikiriwa ??? ni wakati wao kuchangamka................yamkini kama kuna ambao hawajui kusoma japo PICHA WAMEIONA hawahitaji tena imani kama ya Tomaso......yaani mpaka wapapase alama za nyakati!!!!!
 
Hivi mantiki ya kufukia mashimo na kurekebisha barabara pale tu kiongozi mkubwa anapoenda eneo husika ni ipi hasa? Huu ni unafiki wa wazi kabisa.
 
hayo tumeshayazowea hapa nchini kwakuwa hata viongozi wetu wa juu wa kiserikali pindi wafanyapo ziara mikoani ndipo barabara hufanyiwa matengenezo ya kuzugia hao viongozi waone kama fedha za ruzuku toka serikali kuu zinatumika ipaswavyo kitu ambacho ni ujinga.
 
hii ni kawaida hata mwenge unapopita utakuta wako busy kurekebisha barabara zao sijui bajeti anapitisha nani
 
Ulitaka marehemu apitishwe njia mbaya nyie mmichizika kwa kweli

Hv katika machizi haujioni we ndio kilaza wa kwanza?kwani marehemu huyu ndio wa kwanza kupitishwa kwy barabara mbaya huko Alumeru?hacha kushikiwa akili wewe!
 
Ni aibu sana, matengenezo ya barabara yanaishia hapa nyumbani kwa Marehem tu, ina maana kweli hawa wa huku juu hawahitaji barabara nzuri?
Je wa Seela huko kwa J.Kaaya nao hawahitaji?
Watu Wa Poli Je??
Hizo Pesa zilikuwa wapi zipatikane leo?

Wanazuga na bendera za kijani barabara nzima.





Swali la Ziada nje ya mada,. Hivi Kimaro Yule Alekatiwa Migomba Yake na wananchi atakuja Msibani???
 
wananchi wa Arusha ni waelewa sana, hawababaki na kuyumbishwa hovyo hovyo
 
Back
Top Bottom