CCM wahofia mkutano wa CHADEMA, wadai kuna mamluki wameandaliwa kuhadaa umma

the horse

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
652
441
Habari zilizotufikia hivi punde ni kuwa CHADEMA wameandaa vijana mia mbili, ambao wametafutiwa fulana za CCM wazivae kesho katika mkutano wao jangwani lakini pia wamewafanyia semina vijana hao ili waseme kuwa ni wana-CCM ambao wataikana CCM hapo kesho katika viwanja vya jangwani.

Ni mkakati wa kilaghai kwa wananchi wa kujionesha kuwa wanakubalika kwa kuwarubuni baadhi ya watu ambao ni watu wao na kuwatumia kama wanaCCM wanaoikana CCM. Ili kuitangaza kauli mbiu yao ya “vua gamba vaa gwandwa”

Sehemu waliyofanyia semina hiyo imejulikana ni sinza, na mtu aliyewapatia jezi hizo pia amejulikana na hivi sasa yupo jengo la umoja wa vijana akihojiwa na kupewa stahiki nyinginezo. Wameumbuka...!
 
Habari zilizotufikia hivi punde ni kuwa CHADEMA wameandaa vijana mia mbili, ambao wametafutiwa fulana za CCM wazivae kesho katika mkutano wao jangwani lakini pia wamewafanyia semina vijana hao ili waseme kuwa ni wana-CCM ambao wataikana CCM hapo kesho katika viwanja vya jangwani.

Ni mkakati wa kilaghai kwa wananchi wa kujionesha kuwa wanakubalika kwa kuwarubuni baadhi ya watu ambao ni watu wao na kuwatumia kama wanaCCM wanaoikana CCM. Ili kuitangaza kauli mbiu yao ya "vua gamba vaa gwandwa"

Sehemu waliyofanyia semina hiyo imejulikana ni sinza, na mtu aliyewapatia jezi hizo pia amejulikana na hivi sasa yupo jengo la umoja wa vijana akihojiwa na kupewa stahiki nyinginezo. Wameumbuka...!

Mnaogopa kivuli chenu wenyewe!
 
ccm mnatapatapa km mfamaji, mmeshapitwa na wakati hata mfanyeje hampendwi teena! Kesho tunawaonesha jinsi M4C inavyobamba mioyo ya watu
 
Nape una ID nyingi...ingesoma senior expected ningekuamini.UNAANZA PROPA ZAKO.ivi nape kwa akili yko mkutano mkubwa wa cdm hapo kesho wakosekane vjana mia wa ukweli.MI NI KIONGOZI CHADEMA NA HATUJAWAHI KUFANYA UPUUZI HUO COZ TUNAKUBALIKA.KESHO MTAUMBUKA HATA MSEME WALIPANGWA.
 
kumbe ndio mbinu za magamba.! Mtakimbia sana vivuli vyenu.!
 
Moja ya mambo yanayoimaliza CCM ni muda mwingi wanaotumia kupiga umbeya badala ya kujadili njia bora zaidi za utekelezaji wa sera za serikali yake pamoja na tathmini. Hata kwenye biashara utafanikiwa tu pale utakapojua mteja anataka nini na ukajipanga vizuri. Huwezi kufanikiwa kwa kumpaka matope mshindani wako, tena wakati wewe unanuka uchafu wa kila aina.

Wakati wa uchaguzi mdogo Igunga aliibuka Mukama na kusema CHADEMA kimeingiza watu wa kuleta vurugu toka Libya and god knows where! Sasa hivi wanakuja na huu umbeya wa kitoto kabisa kuwa CHADEMA kimeandaa vijana 200! CCM hawana jingine la kusema badala ya kupaka matope? Miaka yote hiyo madarakani hawana cha kueleza wananchi zaidi ya kuimba CHADEMA?
 
Mbona hii story imekaa kipropaganda zaidi ya ukweli?
Inataka kujenga hisia wanaovua gamba ni watu waliopangwa kufanya hivyo na CDM ijapokuwa ukweli unajulikana kwamba kwa sasa watu wameichoka SISIEM. Jambo linalonitia shaka ni idadi ya hao vijana. Kwa kuwa CDM wanataka kuuaminisha na kuushawishi umma kwamba kuna wimbi la wananchi kuhamia chama chao ningetarajia idadi hiyo ingekuwa kama 500 kwenda mbele.
Anyway, hii thread inanipa mashaka.
 
Mara zote, ukiwa mtu makini huhitaji kujua kama hoja fulani ni uongo au la! Uongo mara zote huacha maswali mengi bila majibu!
Kama habari hizi ni za kweli ungesema exactly sehemu ya Sinza unayodai wapo na ungemtaja kwa majina huyo unayedai anawapa T-Shirt!!!
Hakuna atakayeamini habari hii dhaifu yenye lengo la kuhadaa umma!!!
 
kama haya hamyaamini subirini kesho...

tatizo la nape huwa anajichanganya humu jf anatumia id tofaut ili tusimjue lakin baadaye anajisahau anapokuwa anahojiwa na watangazaji na kutoa comment hizi hizi anazotoa humu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom