Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,564
- 7,973
- Thread starter
- #21
Huku baba yake anaomba msaada wazungu wa kupambana na rushwa!
FJM,
Sijawahi kushawishika hata moja kwamba Kikwete ana nia ya dhati ya kupambana na rushwa. Huo msaada anaoomba kwa wazungu utakuta kwa sehemu kubwa umelenga kujipatia fedha zaidi kuliko mafunzo na vitendea kazi.
Kama wananchi wamempelekea majina ya wala rushwa, vyombo mbalimbali kama CAG na kamati za bunge zinabaini rushwa kwenye miradi mbalimbali kama barabara, ndege ya raisi, rada, magari ya kijeshi pamoja na manunuzi mengine mengi lakini hakuna anayechukuliwa hatua, haitarajiwi kabisa kwamba mkuu wa kaya anaweza kupambana na rushwa tena wakati huu ambapo na mwanae amekuwa implicated kwenye matukio mengi ya rushwa.