Elections 2010 CCM Wafanyeje ili kuepukana na Aibu ya 31 October 2010?

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,452
Wakati tukielekea kwenye Uchaguzi Mkuu, naona mchecheto unazidi kukikumba moja ya chama Kikongwe kabisa barani Afrika yaani CCM, nasikia Mkuu wa Kitengo cha Propaganda ( Hivi inakuwaje chama kinakuwa na Dipatmenti kama hii ? Mh ngoja niwaachie wenyewe) Bwana Tambwe Hizza ambaye chama chake kimemuona hafai kuwa mwakilishi wa Wananchi yaani Mbunge na kumtoselea mbali amekanusha vikali kwamba Rais Jk hakuzikana kura za Wafanyakazi.

Je Hizi Kauli za Kutapatapa zinazotolewa na Viongozi wa CCM zinaonyesha kwamba wameanza kukata tamaa ya kushindana na CHADEMA iliyo chini ya mgombea anayeonekana na Watanzania wengi kama Musa au Nyerere wa pili?

Je CCM wamnyamazishe Tambwe kwa maana kauli zake zinazidi kuwatia Hasira Wafanyakazi, yaani anawafanya wafanyakazi wa Tanzania ambao wote ni Wasomi kuwa ni Mazuzu yasikuwa na Uwezo wa kusikia na kuelewa kitu alichozungumza Rais

Je Kuna haja ya CCM kuomba jukwaa kama lile na kuwaomba Radhi Wafanyakazi kwa Kuwadhalilisha?

Nataka kusikia maoni ya wana CCM
 
Hivi tunaweza kupata cv yake huyu ukiondoa uvuvuzela? I doubt kama upstairs yuko sawa! ndiyo maana CUF walimtosa
 
Mbona CCM wote VUVUZELAs only....Ndo maana hakuna wa KUKANUSHA...Sasa fulana zimeshavaliwa...Ngoma INOGILE...
 
Wakuu tuwe analytical.
CCM ni kama jiwe la mtoni, masika au kiangazi, haliendi na maji.Sana sana linazidi kuwa smoother and smoother!!
Ole wao wanao likanyaga vibaya jiwe hilo na kuteleza, utawaona wakienda kwa kasi down stream!!
CHADEMA wanajitahidi sana, lakini ni mbio za sakafuni, mpo hapo wakuu?
 
Back
Top Bottom