Elections 2010 CCM waanza rasmi?

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
2w2ph5k.jpg

oqy8h0.jpg

Jana vyombo vya habari (hasa magazeti) vimepewa 'in CASH' shilingi za kitanzania Million 8 kila moja kuweza kuyavalisha magazeti yao covers kama inavyoonekana kwenye magazeti niliyoambatanisha juu hapo kwa matoleo ya Jumapili (leo).

Ni magazeti mawili tu, Mwananchi na Tanzania Daima ambayo hayakuweza kuupata mgawo huu toka CCM (ni cash na si cheque) nadhani tokana na kuona aidha yana mrengo tofauti (Tanzania Daima), au yako kinyume na matakwa yao (Mwananchi).

BAHATI MBAYA wauzaji wa magazeti walio wengi jijini Dar es Salaam hawajapendezwa na hili wengi wameondoa hii cover kwa magazeti mengi.

Magazeti yanayotoka kila siku yote yamepewa mgawo huu isipokuwa mawili niliyoyataja.

Ni wapi tunaelekea?
 
Hayo magazeti ambayo hayajapewa huo mshiko ni vijarida vidogo ambavyo mafisadi papa na nyangumi wameona hayana ushawishi kwa wananchi,Tz daima ni la kaskazini na Mwananchi ni la wakenya ambao wenyewe siasa za uvumiliano zimewashinda!
 
Mmmmmmhhhh, Thanks for the news... Ngoja .... hawa jamaa wa CCM hajaelewa somo...!!

......wakamuulize Marin Hasan Marin wa TBC.... maana ya PEOLPLE'S POWER!!!

....NGUVU YA UTU WA MTU HAITISHWI NA VIJIMILIONI....WAIT AND SEE!!!!!
 
Mhhh Mkuu,

Leo nimechungulia magazeti karibia yote ila sijaona hiyo cover. Labda wauzaji wameitupa kwa sababu wanajua kiu ya wasomaji. Kama imetupwa basi CCM wajue kuwa imekula kwao.

Waendelee na EPA zao ila wananchi wanajua chaguo lao!!
 
ni kwasababu hawakuandika KUANGUKA KWA KIONGOZI WA CHADEMA........!?
 
Hivi hapoa wa kulaumiwa ni CCM au magazeti ambayo yamekubali kutumika kama mabango ya matangazo?
 
Nijuzeni Wakuu,huo upuuzi ni just a cover au ndio habari kuu za page ya kwanza? Mniwie radhi huku kwetu hayajafika, ni mpaka kesho!
 
Mhhh Mkuu,

Leo nimechungulia magazeti karibia yote ila sijaona hiyo cover. Labda wauzaji wameitupa kwa sababu wanajua kiu ya wasomaji. Kama imetupwa basi CCM wajue kuwa imekula kwao.

Waendelee na EPA zao ila wananchi wanajua chaguo lao!!
Mkuu,

Wauzaji magazeti wengi wamezitoa hizo covers, nadhani hili pia CCM wakiligundua wataona kuwa wametumia hela bure kwani wauzaji wamewaangusha.
 
Hivi hapoa wa kulaumiwa ni CCM au magazeti ambayo yamekubali kutumika kama mabango ya matangazo?
Mkuu, binafsi siwalaumu CCM... Hata chembe, wamepata opportunity na wameitumia. Sasa, wenye matatizo (njaa?) nadhani ni wenye magazeti kuruhusu gazeti kuwa covered na tangazo kwa tamaa ya fedha.

That's my concern
 
Mkuu,

Wauzaji magazeti wengi wamezitoa hizo covers, nadhani hili pia CCM wakiligundua wataona kuwa wametumia hela bure kwani wauzaji wamewaangusha.

And that's what I am saying. CCM wakubaliane na hali halisi badala ya kuwafanya watu wajinga. Wanachofanya ni kuwapandisha watu hasira na ni hatari sana kwa mustakabali wa Taifa letu!
 
Nijuzeni Wakuu,huo upuuzi ni just a cover au ndio habari kuu za page ya kwanza? Mniwie radhi huku kwetu hayajafika, ni mpaka kesho!
Gazeti zima liko covered na hilo tangazo... Ukinunua gazeti linakuwa ndani. Sasa, ndo hapo ninaposema kuwa wauzaji walio wengi ndo wameangusha mpango huu, baadhi wanauza kama ilivyotakiwa lakini wengi wameondoa na kuweka kando! HabariLeo, Mtanzania, Majira, Nipashe, Jambo Leo, etc
 
Nadhani ni vyema tukitofautisha hisia zetu na hali halisi yaani emotions and objective reality if it exists)
CCM wanajaribu kuuza chama na wagombea wake kama ambavyo Coca Cola inataka kuuza soda zake. Vivyo hivyo kwa upande wa Chadema. Mbinu wanazotumia alomuradi isipovunja sheria ya nchi zinakubalika.

Kama wao wameangalia wasomaji wanaotaka kuwafikia wanasoma magazeti so and so na hawataki wasomaji wa TZ daima na Mwananchi ni sawa na haki yao. Nadhani objectively naweza kuelewa hilo la Tanzania Daima lakini Mwananchi nadhani ni maamuzi mabovu ya marketing department ya CCM kuipuza eti ni ya wakenya.. haiwasaidi CCM na inawarudisha nyuma...

Ok sasa basi tuendelee kuangalia mbinu waliotumia ya kuyavisha cover magazeti. Mbinu hii inakubalika kama wataweza kuandika na kufahamisha wananchi kuwa hili ni tangazo. Hapo watakuwa wamefanya kila kitu ndani ya sheria. Tatizo ni kama mbinu hii itaachwa kama habari ya ukweli.

Mwisho kabisa ningependa tu kuongezea kuwa CCM wana tatizo kubwa sana kwani inaonekana kuwa wananchi hususan wafanyakazi wa kawaida ambao ndo wanunuzi wa magazeti (si wakulima vijijini) hawana mapenzi kabisa na CCM na hivyo wachuuzi wa magazeti wameamua kuyatoa cover hizi ili wapate biashara.

Action speaks louder than words.

Chadema take note.... it is possible.....
 
How pathetic! inatia kichefuchefu!

Saana tu mkuu, Yaani hadi kinyaa. watu sijui hawatumii ubongo siku hizi. Badala ya kuchambua hotuba za wagombea wanaendekeza siasa za kipuuzi hazina malengo ya kuwachambua wagombea. Natamani kuona waandishi walio huru, wenye kutoa makosa mbali mbali kwa wagombea iwe CCM, Chadema, CUF nk ili kuwatoa upuuzi watu/wagombea na kuwafanya watu wengine kujifunza. Lakini badala yake hawajui kuwa wanapotosha jamii kwa kiasi kikubwa sana.

Anyway, gonja tuone, lakini kazi ya waandishi inanipa wasiwasi sana hapa nchini kwetu. Inatakiwa waandishi ndo wawe kioo kwa jamii, chambueni wagombea bwana siyo kutulelea upuuzi, hakika mkitufanyia mambo mazuri, tutawakumbuka milele.
 
He hee! Ha ha haaa! Hapa Sinza nilienda kununua gazeti. Muuzaji akaniambia ile cover naweza kuchukua bure nikitaka. Nilikuwa nanunua gazeti lisilo na mgawo/tangazo huo wa kifisadi.

Ila muuzaji hakupendezwa na cover ile ya kijani. Ameziweka pembeni.
 
Sasa basi ni hasara tupu kufanya marketing kubwa kama hilo ... inachekesha kwa kweli... waste of time and money.... ila ni habari njema kwa Chadema!
 
He hee! Ha ha haaa! Hapa Sinza nilienda kununua gazeti. Muuzaji akaniambia ile cover naweza kuchukua bure nikitaka. Nilikuwa nanunua gazeti lisilo na mgawo/tangazo huo wa kifisadi.

Ila muuzaji hakupendezwa na cover ile ya kijani. Ameziweka pembeni.

Nadhani uamuzi wa hawa wauzaji kuelewa kuwa mustakabali wa maisha yao unatokana na kuuza magazeti mengi na si sera za chama ni ushindi mkubwa. Pia kwa wauzaji hao kuweza kuelewa matarajio ya wateja/wasomaji ni mabadiliko makubwa ya kifikra na kiutendaji katika ngazi ya chini. Free at Last! Amandlah!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom