Elections 2010 CCM waanza kumwaga damu mkoani Mara

nickname

JF-Expert Member
Dec 20, 2009
544
147
WATU watano wanashikiliwa na jeshi la Polisi mjini hapa kwa tuhuma za kuhusika katika tukio lililotokea jana(juzi) ambapo watu wanaosadakiwa kuwa ni wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi CCM na viongozi wa chama hicho kuhusika katika kuwakata na kitu chenye ncha kali wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kile kilichodaiwa kuwa wananchi hao kutoonyesha ushirikiano na chama hicho tawala.

Wakiongea kwa tabu baada ya kufanyiwa unyama huo katika hospital ya mkoa wa Mara majeruhi hao walisema kuwa kitendo hicho kimetokea jana jioni baada ya mkutano wa kampeni wa cha CHADEMA katika kata ya Buhare.

Sele Mwita(27) ambaye ni mmoja wa wahusika waliojeruhuiwa katika shambulio hilo alisema kuwa wakati anatoka kwenye kampeni za CHADEMA alikutana na kundi la watu wakiwa wamevalia bendera na skafu za CCM huku wakisema kuwa huyu naye anahusika.

‘Mimi wakati natoka kwenye mkutano nilikutana na vijana wakiwa na mapanga huku wakiwa wamevaa vitambaa vya CCM wakiongozwa na Kapul na kuanza kusema huyu naye ni wa CHADEMA na kuanza kunikata ndipo nikaanza kukimbia” alisema Sele

Naye Pambano Malima(30) mkazi wa Kigera ambaye mkasa huo ulianzia kwakwe alisema kuwa alikutana na kundi hilo la vijana wakati anapeleka pikipiki na kuanza kumshambulia kwa kumkata mapanga

Walisema kuwa vitendo hivyo vyote vinatokea huku viongozi wa Chama cha Mapinduzi mjini hapa wakiwa wanahusika kwa ukaribu,ambapo mmoja wa kiongozi wa tawi katika kata ya Kigera Kapul Charles alikamatwa kwa kuhusika na tukio la kwanza la kuwakata vijana wawili mapanga .

Mbali na tukio hilo ambalo limetokea jana usiku lakini leo asubuhi katika kata ya Nyakato mjini hapa wafuasi wengine wawili wa chama cha CHADEMA walivamiwa ndani na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa cha cha Mapinduzi wakisema kuwa washushe bendera zao za CHADEMA ambazo wameziweka katika nyumba zao.

Akiongea na waandishi wa habari mjini hapa leo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mara kamishina msaidizi ACP Robert Boaz alikiri kutokea kwa tukio hilo katika eneo hilo la Kigera Migombani.

Alisema kuwa watu waliojeruhiwa walikatwa na vitu vyenye ncha kali baada ya vurugu kutokea ambapo katika eneo hilo kulikuwa na mkutano wa CCM katika nyumba ya Mkono Salima ambaye kamanda Boaz alishindwa kuthibitisha kama alikuwa balozi au la katika hatua hiyo aliongeza kuwa baada kikao hicho ndipo ulizuka ugomvi huo kati ya vijana waliokuwa ndani na waliokuwa katika maeneo yale.
 
Sasa mvunjaji wa amani ni nani?ccm au vyama vya upinzani?miaka ya nyuma walikua wakiwatuhumu cuf kuwa wavunja amani kumbe ni ccm ndio tabia yao
 
Katika taarifa ya habari ya saa mbili ITV imetoa taarifa inayoonyesha Vijana wa Chadema wakiwa wameshambuliwa na kujeruhiwa vibaya yaani damu imemwagika.

Kuthibitisha hilo Polisi wanasema watu watano wakiwamo viongozi wa CCM na tayari hatua mbadala zinachukuliwa.
 
Shimbo aliahidi kuzuia umwagaji damu .. ... hivi alimaanisha nini? Na je, anaweza kutolea maelezo haya?
 
kulikuwa hakuna mapambano kati ya chadema na ccm. Hii heading ..... (&*(*#()&)#)@&))#*)8203 ...
imebadilika haraka hivi?
 
aliyebadilisha heading ya hii thread ana lake jambo ... (nadhani nina idea ya nani kafanya hivi ila sitamtaja hapa).

na kisha mafisadi ya ccm kina mchambuzi mnalialia hapa kila siku kuwa ccm inaonewa kwenye hii forum?!
 
WATU watano wanashikiliwa na jeshi la Polisi mjini hapa kwa tuhuma za kuhusika katika tukio lililotokea jana(juzi) ambapo watu wanaosadakiwa kuwa ni wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi CCM na viongozi wa chama hicho kuhusika katika kuwakata na kitu chenye ncha kali wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kile kilichodaiwa kuwa wananchi hao kutoonyesha ushirikiano na chama hicho tawala.

Wakiongea kwa tabu baada ya kufanyiwa unyama huo katika hospital ya mkoa wa Mara majeruhi hao walisema kuwa kitendo hicho kimetokea jana jioni baada ya mkutano wa kampeni wa cha CHADEMA katika kata ya Buhare.

Sele Mwita(27) ambaye ni mmoja wa wahusika waliojeruhuiwa katika shambulio hilo alisema kuwa wakati anatoka kwenye kampeni za CHADEMA alikutana na kundi la watu wakiwa wamevalia bendera na skafu za CCM huku wakisema kuwa huyu naye anahusika.

‘Mimi wakati natoka kwenye mkutano nilikutana na vijana wakiwa na mapanga huku wakiwa wamevaa vitambaa vya CCM wakiongozwa na Kapul na kuanza kusema huyu naye ni wa CHADEMA na kuanza kunikata ndipo nikaanza kukimbia” alisema Sele

Naye Pambano Malima(30) mkazi wa Kigera ambaye mkasa huo ulianzia kwakwe alisema kuwa alikutana na kundi hilo la vijana wakati anapeleka pikipiki na kuanza kumshambulia kwa kumkata mapanga

Walisema kuwa vitendo hivyo vyote vinatokea huku viongozi wa Chama cha Mapinduzi mjini hapa wakiwa wanahusika kwa ukaribu,ambapo mmoja wa kiongozi wa tawi katika kata ya Kigera Kapul Charles alikamatwa kwa kuhusika na tukio la kwanza la kuwakata vijana wawili mapanga .

Mbali na tukio hilo ambalo limetokea jana usiku lakini leo asubuhi katika kata ya Nyakato mjini hapa wafuasi wengine wawili wa chama cha CHADEMA walivamiwa ndani na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa cha cha Mapinduzi wakisema kuwa washushe bendera zao za CHADEMA ambazo wameziweka katika nyumba zao.

Akiongea na waandishi wa habari mjini hapa leo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mara kamishina msaidizi ACP Robert Boaz alikiri kutokea kwa tukio hilo katika eneo hilo la Kigera Migombani.

Alisema kuwa watu waliojeruhiwa walikatwa na vitu vyenye ncha kali baada ya vurugu kutokea ambapo katika eneo hilo kulikuwa na mkutano wa CCM katika nyumba ya Mkono Salima ambaye kamanda Boaz alishindwa kuthibitisha kama alikuwa balozi au la katika hatua hiyo aliongeza kuwa baada kikao hicho ndipo ulizuka ugomvi huo kati ya vijana waliokuwa ndani na waliokuwa katika maeneo yale.
 
Mods wataibalisha heading ya hii thread...
Sijui ni kwanini wanafanya hivi.... waliomwaga damu ni ccm, lakini jamaa wanasema kuwa ni mapigano kati ya chadema na ccm?!?!??!?!
 
Ngoja Tuwaone mods
 
Chanzo: Taarifa ya habari ya ITV saa mbili Usiku 12 Oktoba 2010.

Hali ni mbya kabisa, inasikitisha! Wale waliotazama taarifa ya Habari wataungana nami. Huko Mara, baada ya wanachama wa CHDEMA kumaliza mkutano wao kwa amani kama kawaida bila tatizo lolote, walijitokeza vijana wa CCM wakiwa na mapanga, wakawashambulia na kuwajeruhi vibaya wanachama wa CHADEMA waliokuwa wamevaa nguo zenye rangi za Chadema. Sasa jamani, Damu iliyokuwa inazungumziwa kwamba itamwagika, ndiyo hiyo imeanza, CCM wameanzisha. Je, tunaelekea wapi?
 
Shimbo alidai kuwa yuko tayari kuhakisha damu haimwagiki! Kumbe ni "Makamba in disguise!"
 
Mods wataibalisha heading ya hii thread...
Sijui ni kwanini wanafanya hivi.... waliomwaga damu ni ccm, lakini jamaa wanasema kuwa ni mapigano kati ya chadema na ccm?!?!??!?!

Mwafrika kuna wakati watu walikataa JF kusajiliwa na serikali. Haya ndiyo matokeo yake. Ule uhuru wa kuongea unaanza kupungua polepole. Kusajiriwa ni kuuza uhuru kwa yule anayesajiri.
 
Asante mods kwa kufanya la haja kwenye hii thread .... I love you guys much much much .. mwa mwa mwa mwa mwaaaaaa.
 
Back
Top Bottom