Hili ni jengo la kupokelea abiria mpaka sasa uwanja huu haujulikani utakamilika lini kwani toka mwaka jana walisema mwezi wa kumi na mbili 12 utaanza kufanya kazi lakini mpaka sasa uwanja huo unaendelea kujengwa na haijulikani utakamilika lini
Hii ni barabara ya kutua na kurukia ndege ikiwa imekamilika
Hii ndiyo hali ya halisi ya uwanjani hapo kitendawili chake hatujui kitateguliwa lini
Hivi kuna anayeweza kusaidia maelezo kwamba kwa nini majengo karibu yote yanayokuwa designed na "wataalam" wa Kitanzania huwa yanakuwa na mapaa yanayoezekwa? Nilikuwa sijawahi kuona picha za huu uwanja, lakini najiuliza kwa nini majengo yake hayana muonekano wa terminal buildings za uwanja wa ndege na badala yake yapo kama dispensary?
Architects na engineers wetu wengi hawana exposure ya wenzao wanafanya vipi mambo huko nje na ndio maana hata nyumba za National Housing wanazojenga hazinaubunifu wa ku incorporate environmental considerations kwenye michoro yao!!Nyumba zinajengwa tu kama mabox bila kujali mambo kama ya energy conservation.
Hivi hawa architects na engineers huwa wanafundishwa nini mfano pale chuo cha ardhi? Maana hata mtoto mdogo anaweza kwenda kwenye Google images na akapata picha kama milioni hivi za majengo ya viwanja vya ndege dunia nzima; wao wanafanya utafiti wao wapi?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.