CCM: Tumetumia Sh220mil, CHADEMA 600mil

Mwigulu nchemba na Nape kwa sasa hawana tena marafiki wazuri wamebaki na wale wanafiki tu
 
yakionekana magari ya serikali ktk kampeni leo inabidi magufuli achukue hatua
au vinginevyo wananchi wachukue hatua wenyewe.
 
Nashukuru Nape amekubali kuwa walitumia sh. 220m. Mwigulu alisahau kuwa katika hesabu zake, alikuwa ameiweka kando ile zero moja '0 ndo maana akapata sh. 22m
 
Nape amekubali kuwa chama chake cha Magamba kimetumia Sh. 220 milioni, wakati Mwigulu alijibu hapa juzi kuwa Magamba walitumia Sh. 22 milioni...!!:crazy: Naona waanaanza kuweweseka na kila mtu anaibuka kivyake! Leo kwenye uzinduzi wa kampeni tutasikia data zingine tena. :violin:
kaka umeniwahi, Mwigulu njoo hapa haraka sana kujibu la siyo Mod mpigeni toto ban, bunge zima linadanganya kitoto kabisa bhana
 
CHADEMA wajibu hili kwa kukubali au kukataa na watoe ufafanuzi kwamba fedha zilitumikaje.

Chadema watatoaje ufafanuzi wakati Nepi hajatoa pia ufafanuzi kuwazilitumikaje? wewe unaweza kujibu huu *****?ukiujibu upuuzi huu wa Nepi utaonekana na wewe ni Fyatu tu.:lock1:
 
nataka nim PM mwigulu asituletee mambo ya kitoto watu na heshima zao ni wazi anaweza jifanya hajaiona hii thread
 
CCM: Tumetumia Sh220mil, Chadema 600mil
Send to a friend
Monday, 12 March 2012 09:49
0digg

Elias Msuya
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimetetea matumizi ya Sh220 milioni katika kura ya maoni kumpata mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru Mashariki, huku kikirejesha tuhuma za matumizi mabaya ya fedha kwa wapinzani.
Utetezi huo wa CCM ulitolewa jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ambaye alipuuza tuhuma zilizotolewa na Chadema dhidi yao, akisema kuwa hadema ndiyo kimetumia fedha nyingi zaidi.
Akizindia kampeni katika uchaguzi huo juzi, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema CCM imekiuka sheria na taratibu za matumizi katika mchakato mzima wa uchaguzi, kwa kutumia Sh220 milioni katika hatua hiyo ya awali, tofauti na maelekezo yanayowataka kutumia si zaidi ya Sh80 milioni.
Mbowe pia alimtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa kutoa tamko juu ya CCM kukiuka Sheria ya Uchaguzi kwa kutumia kiasi hicho kikubwa cha fedha wakati wa mikutano miwili ya kupitisha mgombea wao wa ubunge.
 
“Tunamuomba Tendwa atoe tamko juu ya hili, kwani mkutano wa kwanza wa CCM walikuwa na wajumbe1,034 ambao kila mmoja alilipwa posho ya Sh50,000 na walitumia zaidi ya Sh100 milioni na mkutano wa pili ulikuwa na wajumbe1,044 ambao walitumia zaidi ya Sh120 milioni,” alisema Mbowe.
Licha ya kukiri matumizi hayo, Nape amekigeuzia kibao chama hicho akisema kuwa kimetumia zaidi ya Sh600 milioni katika kura za maoni zilizowawezeasha kumpata mgombea wao.
“Mbona wao (Chadema) wametumia zaidi ya Sh600 milioni, hamuwaulizi? Waulizeni Chadema kwa nini watumie fedha zote hizo, siyo kufuatilia tu fedha zetu” alisema Nape bila kufafanua madaia yake.
Tofauti na madai ya Nape, Mbowe alisema kuwa chama chake kilikuwa na wajumbe 888 na kilitumia kiasi cha Sh6.2 milioni pekee kutokana na usafiri na chakula kwa wajumbe.
Mchakato wa kumpata mgombea wa CCM, Siyoi Sumari ziligubikwa na mizengwe ambapo licha ya Siyoi kushinda kwa mara ya kwanza, kamati kuu ya CCM iliamuru kuwa uchaguzi huo urudiwe tena ambapo Siyoi alishinda tena.
Wakati Chadema kilichomsimamisha Joshua Nasari wakizindua kampeni zao juzi, CCM waliomsimamisha Siyoi Sumari wanatarajia kuzindua kampeni zake leo ambapo Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa ndiye atakuwa mgeni.
Akizungumzia maandalizi ya kampeni zao, Nape alisema kuwa watafunika kampeni za Chadema.
“Kwa nini tuandikie mate wakati wino upo, nyie mtaona kesho (leo) itakavyokuwa. Tutafunika tu,” alisema Nape.
Licha ya Chadema na CCM vinavyoonekana kuwa na wafuasi wengi katika jimbo hilo, vyama vingine vilivyosemamisha wagombea ni pamoja na TLP, SAU na UDP.

Sasa hizi propaganda za Nape hadi lini? mwenzie katoa mchanganuo wa jinsi pesa imetumika sasa mbona yeye bwana Nape mbona anatoa mambo kienyeji utadhani si msomi? atwambie hiyo 600mio imetumika wapi?aache ubabaishaji!na atwambie vizuri gaharama halisi walizotumia na atupe mchanganue wake kama hajaumbuka humu!
 
hoja ilikuwa kwa nini ccm walitumia milioni 220 kinyume cha sheria hivo nape alipaswa kujikita hapo kutoa mchanganuo mbadala wa ule aliotoa mh. mbowe,chadema kutumia hata bilioni moja hakuhalalishi ccm kutumia mil,220 kwani kosa la mtu mmoja halihalishi la mtu mwingine. Pili kama cdm nao walitumia kiasi kikubwa baada ya kujibu tuhuma za mbowe kwa takwimu alitakiwa atoe takwimu za ku support madai yake dhidi ya cdm kinyume cha hapo anaonekana kama debe tupu ambalo haliachi kutoa mlio
 
Back
Top Bottom