CCM toeni elimu kwa viwavi wenu mliowatuma hapa jamvini

Mkuu, mi nakubaliana na wewe kabisa. Tatizo la watu wa CCM hawataki kuambiwa ukweli, ukiwaambia wanasema unawatukana au huwapendi.

Hivi kweli jamani, kwa hoja za akina MS na akina Majimshindo wanategemea kweli kumshawishi mtu hapa JF na kumfanya aipende CCM? Kama huyo mtu alikosea njia akastukia tu yupo JF ni sawa. Lakini kama alijiunga JF as a GT, wasitarajie mabadiliko, badala yake wategemee maumivu tu.

Jamani, hivi huko CCM hakuna watu wanaoweza kuchambua hoja za hapa JF kwa kuendana na mtiririko wa hoja yenyewe? Kama hawapo, na CCM ikaona hao iliowatuma hapa ndo maGT wao, basi RIP CCM.
 
Natamani kweli kweli Waanzishe CCMForums nikawashukue huko huko

CCMForums haitatafautiana na gazeti la uhuru, haiwezekani kwani kwa CCM mijadala yote ni siri na inafanyika katika vikao vya chama.

CCM inamiliki vyombo vikuu vya habari ambavyo vinaendeshwa kwa kodi za watanzania wote. Wanavitumia kusambaza upupu wao,hata vyombo hivyo vinapotoa nafasi ya midahalo wanaikimbia mfano wakati wa uchaguzi mkuu.

Sababu kuu ni kwamba wanaogopa kwani kwa kufanya hivyo kutatupa nafasi ya kujua maovu yao zaidi. Wameamua kufuata utaratibu wa "Kukaa kimya ili tueendelee kushuku kua waovu kuliko kufungua mdomo na kutufanya tuthibitishe kua waovu".

Hivyo hapa hawatutishi kwa wanaingia katika mjadala wakati CCM imeisha wakakataza kuzungumza masuala ya CCM ila kwenye vikao tu.

KUTOKA KWAO TUTEGEME POROJO TU.:A S-baby:
 
CCM haitakagi kuambiwa ukweli mfano ni pale aliyewahi kuwa kaibu mkuu wa chama hicho marehemu Horace Kolimba alipobaini mapungufu ndani ya chama chake na akasema "CCM imepoteza dira".

Laiti kama wangejitafakari kipindi hicho labda sasa hivi wangekuwa mbali. Badala yake wakambana vilivyo mpaka pressure ikampanda na kufa siku hiyo hiyo.

CCM ilishapotea njia siku nyingi hata mahali pa kuanzia hawapajui.
 
Kwa thread yako hii, naendelea kusadiki kabisa kuwa yaliyosemwa na Mukama yanaendelea kuwa kweli
 
Kwa thread yako hii, naendelea kusadiki kabisa kuwa yaliyosemwa na Mukama yanaendelea kuwa kweli
Hivi na wewe pia ni kiwavi tatizo lenu ni kudhani kujaza page kwa kupinga chochote kinachofanywa na CDM ni kumsaidia Mukama.
 
new+blood.jpg


Du! Kwenye hiyo picha hebu mwangalieni Mwakembe vizuri jamani, nini kinaendelea kichwani mwake?
 
When you argue on hearsay(maneno ya wasukuma mikokoteni) would you expect any great thinker or simply a thinking man to compliment you?.
This type of presentation is what makes this thread CHEAP,your comments included.
hapo ccm ndipo mnapofeli kwani sisi WASUKUMA MIKOKOTENI sio watanzania mpaka kipindi cha kampeini na uchaguzi ndo tunakuwa na thamani?
 
Gwakisa, i doubt of your thinking capacity,how can you despise wasukuma mikokoteni,as you have mentioned them,or is just because you belong to the exploitation class!!,no more room for you chama cha magamba.you have exploited us a great deal!
 
Wasiwasi wangu ni kuwa hao viwazi wa CCM wasijeishia kujiunga CDM maana jinsi great thinkers tunavyochambua na kuukemea uozo wao huku ndani ni ngumu kwa mwenye akili timamu kuupigania na ku convice wenye akili zao kuwa si kweli kila siku.....................
 
hapo ccm ndipo mnapofeli kwani sisi WASUKUMA MIKOKOTENI sio watanzania mpaka kipindi cha kampeini na uchaguzi ndo tunakuwa na thamani?
Wengi waliosupport hii thread ni WASUKUMA MIKOKOTENI kwa kufikiri na hata hadhi ya post yenyewe.Ndio maana hakuna kitu cha maana hapa.
Ile adage"dont argue with a f...l, people might not note the difference" seems to make sense here.
 
Gwakisa, i doubt of your thinking capacity,how can you despise wasukuma mikokoteni,as you have mentioned them,or is just because you belong to the exploitation class!!,no more room for you chama cha magamba.you have exploited us a great deal!
Use your white matter mister and dont worry about MY thinking capacity.
Please refer to the post above!! The difference between me and you is like the far ends of the Pacific.
 
This is CHEAP!
Written by a cheap character,with a cheap line of thought.
Cheaper than a two dollar ho!

Sasa Ndio Umeandika nini Mkuu? Mbona Unazidi Kuithibitisha Kauli yangu juu ya Uwezo wa Viwavi Jeshi wengi wa CCM hapa jukwaani. Anyway Najua Viongozi wako hawataudharau Ushauri wangu Maana Umetolewa JF ambayo tayari Walishasema kwamba Ni Threat tatizo ni kwamba wameshindwa kujua kwa nini ni Threat.

JF is Threat To CCM not because of the Members who are against it ( CCM) but those Members who Defend it ( Of Course like you )
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kiliunda tume ya Iliyoongozwa na Bwana Wilson Mukama katika kutafuta sababu hasa ya CCM kuchukiwa na Wananchi hasa Vijana.

Kwa Mujibu wa Bwana Mukama ni kwamba Tume hiyo ilifanya Kazi Kisayansi na moja kati ya Scientific Findings zao ni kwamba Mtandao wa Jamiiforums unamilikiwa na CHADEMA.

Bwana Mukama alienda mbali na kupendekeza kwamba CCM nayo ianze kutumia social media ili iweze kupendwa na Vijana. Vile vile Bwana Mukama alipendekeza CCM ijivue Magamba yaani badala ya kufahamika kama Chama Cha Mapinduzi sasa Kijiite Chama Cha Magamba ( Wao what a wonderful creativity)

Tokea Bwana Mukama atoe ripoti yake ya Kisayansi, kumetokea Wimbi kubwa sana la Watu wanajiunga Jamiiforums na Kuimba wa Magamba Magamba

Nilikuwa na Pendekezo Moja kwa Bwana Mukama

Kazi mliyowapa Vijana wenu hapa JF ni Ngumu sana, yaani Badala ya kuwasaidia kuokoa Jahazi wao wanalizamisha kabisa.

Nawashauri mngewapeleka Vijana wenu mliowatuma hapa Ngurdoto kwa Semina Elekezi juu ya Namna nzuri ya Kujibu hoja na kuacha Uongo.

La sivyo hata mkianzisha CCMForums baada ya Muda Mtaikimbia na mtaanza kulalamika kwamba inamilikiwa na CHADEMA maana ninyi kila anayewapinga basi ni CHADEMA
Mkuu mimi nafikiri hawa waheshimiwa waliitangaza JF kwa sana ndo maana imepata wanachama wengi sana kwa muda huo. Tujadili hoja wanazoleta wanachama na siyo watu au wanachama kwani sisi sote ni Jamii moja kutoka familia mbalimbali zenye malezi mbalimbali. Kumhukumu mwanachama wa JF kwa tarehe aliyojiunga na kumhisi kuwa wa itikadi fulani kunawapunguzi uwezo wa kujibu hoja na kukimbilia kuwa kuna watu wametumwa. Focus kwenye ideas na siyo lazima uchangie kila thread.
 
Umenifurahisha sana hapo,
Tatizo la CCM ni kutojifunza mbinu mpya bado wanafikiri kushinda vita lazima uwe na jeshi kubwa la wanajeshi laki 9 wenye rifle kama hawa viwavijeshi.

MBWA MZEE hafundishiki!
Ukimuangalia Mukama, kila wakati yeye anahangaika na theory za ideologies alizopata mashariki. Kumbe sasa hivi hakuna m-tz anayehitaji nadhalia hizo.

Nahisi kwamba wangeweza kumpa nguvu Nape, anaonekana anaweza kujifunza, akashika hata mouse ya kompyuta. Lakini hata yeye kama lengo itakuwa ni kushawishi vijana, atakwama tu.

CCM Timizeni wajibu wenu tukiona ubora tutawapenda.
 
Back
Top Bottom