CCM - The Master Magician - na wale wanaosubiri kushangilia!!!

Azimiojipya

Kwanza kabisa nadhani kiswahili kina neno zuri sana kuliko "magic tricks" ambalo ni "mazingaombwe" nitafafanua!!
 
YAKOWAZI amakweli mie nayaona mazingaombwe lakinu HAYA yatadumu kwa mda gani hivi kweli JMk na huyo PM WAKE wako radhi kutuchezea mazingambw kwa hiki kipindi chao kilichobakia mie siioni salama yeyote
 
Azimiojipya

Kuzinga kwa kiswahili ni kuzuia au kuziba jambo lisionekane. wale waliocheza rede hapa Dar es salaam watakumbuka "kuzinga" kama kitendo cha kuzuia mpira usipite ili uudake na kumlenga nao aliye kati akicheza. Ombwe ni utupu (Vacuum) kwa hiyo Mazingaombwe ni kitendo cha "kuuziba utupu".

Hawa watawala wetu wanajua kwamba kuna "ombwe" kubwa sana la utawala lililosababishwa na wao kushindwa kukidhi haja za kiuongozi. Kwa bahati mbaya sana ombwe lililopo ni la uongozi lakini watu wanadhani tatizo letu ni wale walioko kwenye nafasi za uongozi. Watu wa aina hii wanaamini tukiwatoa baadhi ya watu matatizo yetu yatakoma. KOSA LA KWANZA.

Tangu mwaka 1987 CCM ilipoandika andiko lake (Doctrine) la mwisho " Program ya chama 1987 - 2012" hakuna andiko lolote lililoandikwa na CCM kuonyesha jinsi gani wataongoza nchi hii. Lakini hata hilo andiko lao ambalo linafikia mwisho wa uhai wake mwaka huu halijawahi kufanyiwa tathimini wala marekebisho yoyote.

Andiko la chama (siyo ilani) ndiyo ramani ya kuongozea nchi. Sasa kama CCM hawana andiko lolote la kuonyesha jinsi gani wataendesha nchi hii na wananchi wanaendelea kuwachagua, tatizo si lao ni letu sisi. Kuichagua CCM ni sawa na kukubali kupanda ndege yenye rubani asiye na ramani ya kule mnakokwenda. HILI NI KOSA LA PILI.

Wakati watu wengine wanapiga kelele ya kutaka abiria waliomo kwenye ndege yenye rubani asiye na ramani washuke, wamiliki wa ndege wanawaambia abiria kwamba wale wanaowashawishi washuke wana wivu kwa sababu wao hawajawahi kupanda ndege. Abiria nao wanachachamaa wanasema kwamba tatizo siyo rubani kukosa ramani bali vioo vya ndege kupigwa "tinted",Safari inaendelea!! Watanzania wengi wanaamini kwamba tatizo si CCM bali ni la wanaoingoza CCM. KOSA LA TATU.
 
Back
Top Bottom