CCM tatizo ni maendeleo duni si CHADEMA!!

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,600
8,741
Chanzo cha mwamko tulio uona Tanzania wakati wa uchaguzi ni kwasababu wananchi wengi kwa muda sasa wamechoshwa na maendeleo duni ya nchi huku rushwa ikiwa kama mchezo ambao wachezaji hawaogopi.
Umeme:Mimi naishi ugaibuni kwa muda sasa lakini ndugu zangu wananieleza Tanzania kuna mgao wa umeme sasa hivi wakati huohuo serikali ya CCM imesaidi mkataba wa IPTL na Richmond ya mabilioni ya shilingi na pesa imeishia kwa viongozi wachache na hizo kampuni feki huku Watanzania wa kawaida wakibaki na mgao!. Card za luku unalipia kabla ya kupata huduma (pre-paid) sasa ni kwa nini kuna mgao wakati Tanesco imechukuwa pesa kabla ya kutoa umeme halafu hawakupi umeme kwasababu ya mgao. Hii ipo Tanzania tu!!!
Elimu: Viongozi wengi wa Tanzania wamesomeshwa bure wakati wa Nyerere, ingawa nyerere alikopa sana kuendeleza elimu lakini ni watu wengi walisomeshwa na elimu ya kiwango cha juu sana. Sasa kuna matabaka ya elimu, kwa ujumla elimu imeshuka Tanzania. Kwa watu wa vijijini hawana walimu kwa sababu walimu ni wachache na hakuna kitu chochote cha kuhamasisha vijana kwenda kufundisha vijijini barabara mbovu, mishahara duni, hadhi ya shule nyingi ni ya chini na Watanzania wengi hasa wadogo wamepoteza uzalendo hivyo ni vigumu kupata walimu. Kwa wale walio mijini hata kama ni shule za serikali wanafunzi wanasoma kwa tution tu, hii inamaana wanaenda shule kama ushahidi lakini shule ya ukweli Tanzania kwa vijana wa mijini ni tution. Vilevile kuna shule za masister au za makanisa ambazo ni za wachache wenye vipaji na shule hizi zina ubaguzi wa hali ya juu. Mimi ni mkatoliki lakini najua kabisa kwa utundu niliokuwanao udogoni nisingekubaliwa kwenye hizi shule kwasababu wanachagua wanafuzi wachache wasio na utundu na wenye uwezo. Ingawa nimetokea familia yenye uwezo ningeishia kufukuzwa na hili mimi naona ni ubaguzi wa wanafunzi. Shule nyingi za kidini hasa za katoliki zina wanafunzi wachache kwasababu wengi wao wanafukuzwa kabla ya kumaliza shule, hatuwezi kama nchi kutegemea seminari pekee kwa viongozi wetu wa baadaye. Vilevile kuna shule chache za kislaam ambazo ukiacha Agha Khan hazifanyi vizuri na watoto wanafelishwa kila mwaka lakini serikali ina ziacha hizi shule kwasababu inaogopa siasa. Kama shule inafelisha watoto 80% inatakiwa kufungwa kwasababu inaibia wazazi pesa sio bure kusomesha watoto. Kwa ufupi ni kwamba serikali ya CCM haina agenda ya nchi mfano. Wanafunzi wote wa mwaka wa mwisho wa vyuo vikuu ni kwanini wasifundishe kwa miezi sita shule kabla ya kupewa maganda yao kama ilivyokuwa JKT. Hawa ni vijana wanaopewa mikopo ya serikali ambayo inatoka kwa wanachi na wengi wao hawatalipa! ni kwanini tuna tatizo la walimu wakati kuna vyuo vingi tu JKT ilisaidia nini je ni kwanini vijana wetu wasomi wasifundishe wadogo zao!!.
Maji: Ni kwanini watanzania hawana maji safi wakati technology ya maji safi ni ndogo sana! mimi hapa USA kwa miaka zaidi ya kumi sijawahi kusikia hata mtu mmoja kati ya watu milioni 300 amepata kipindupindu au taifodi na tunakunywa maji ya bomba! mimi kwa mfano sikumbuki ni lini nimenunua maji! cha kuongeza hapo kwasababu hakuna mito mingi huku maji mengi tunayotumia ni ya ****** ambayo yamesafishwa hivyo maji uki flash ****** yanaenda kusafishwa na kurudi maji safi kwenye bomba, hatukhitaji hata kuchemsha. Je kuna ugumu gani kutuma wataalamu wa maji waje hapa kuangalia ni jinsigani wenzetu wanaweza hili, hizo pesa za bili za maji zinaenda wapi?.
Barabara:Houston, TX mji wa watu milioni 4.5 una magari milioni mbili na dar mji wa watu milioni karibu 4 una magari laki mbili tu na raisi amesema miaka mitano yanaweza kufika magari laki tatu. Tatizo la foleni si wingi wa magari bali wembamba wa barabara, lakini pamoja na kujua huu ukweli bado serikali ya CCM inajenga barabara nyembamba. Japan rafiki mkubwa wa Tanzania walifanya study na kuwapa free plan ya kujenga barabara za Tanzania lakini barabara zinajengwa kisiasa badala ya kiuchumi. Serikali inakazania wingi wa barabara wakati wamesha elezwa barabara zinatakiwa kupanuliwa na pesa ni ya msaada lakini wanataka kupeana tenda na plan ya lane tatu wanaweka mbili halafu pesa wanakula. Vijijini hakuna barabara kabisa!! je wenzetu waliwezaje kujenga barabara miaka ya 1940 wakati kulikuwa na hali ngumu ya kiuchumi dunia nzima, vita na technology ilikuwa ndogo! Watanzania wengi hawaelewi hapa!!!
Rushwa:Tanzania inarushwa kila mahali kuanzania bandarini mpaka kwenye idara ya vizazi na vifo. Mimi nilienda kwenye msiba wa ndugu yangu na kupata cheti cha kifo niliombwa posho!!. Document za viwanja kila siku unaambiwa vimepotea ili uanze vipimo upya na waweze kupata rushwa tena, TRA wanachelewesha mizigo ya wafanya biashara ili gharama za storage ziwe juu wa waweze kupata posho kwenye mnada wa hivyo vitu.Hivi vitu vyote hapa ni Watanzania wenyewe kwa jasho lao wanafanya kujenga, biashara n.k lakini badala serikali kuwa upande wa msaada hivyo kuhimiza maendeleo serikali yetu iko upande wa rushwa na kuzuia maendeleo. kwa ufupi rushwa kubwa kwenye serikali ya CCM imefanya serikali kuwa kikwazo cha maendeleo ya wananchi badala ya msaada! je tutafika hivi!!. Raisi kwa upande mwingine watu walewale wenye kashfa na rushwa anawaita marafiki je tumuamini nani!!.

nina mifanya kila sehemu lakini nitaishia hapa
Watanzania hawana tatizo la udini, ukabila wala aina yeyote ya ubaguzi Watanzania wengi wamechoshwa na serikali na wanataka maendeleo. CCM badala ya kujaribu kumzuia CHADEMA ni bora mdumishe maendeleo kwani habari kwa miaka ya sasa huwezi kuzizuia mtapoteza muda bure.Dunia inabadilika kwa kasi sana na muda wa siri umepita na hautarudi tena. Je wajukuu wetu tutawaachia nini!
 
ndugu yangu kama ulikuwa mawazoni kwangu nimetoka kuchangia hoja kwenye hoja ya mtu mmoja akikitabiria cdm kifo ndani ya mwaka mmoja na kusema tatizo sio cdm bali ni hali ngumu walio nayo wananchi.hebu fikiri hivi ss chama tawala kina fanya kila mbinu kuwamaliza cdm badala ya kutimiza ahadi millioni walizoahidi wakati wa kampeni.kweli inatisha kitu ambacho ccm hawakijui ni kwamba watu wamechoka na ahadi hewa zao huku wakiona mengi yanatendeka na baadhi ya vigogo wanajifanya hii nchi ni yao jinamizi la ufisadi na kuendelea kuwakumbatia vinara wa sakata hilo kutakimaliza chama.wananhi ss wameamka hata huko vijijini walikokuwa wakiwafunika mambo yamebadika.
 
Chanzo cha mwamko tulio uona Tanzania wakati wa uchaguzi ni kwasababu wananchi wengi kwa muda sasa wamechoshwa na maendeleo duni ya nchi huku rushwa ikiwa kama mchezo ambao wachezaji hawaogopi.
Umeme:Mimi naishi ugaibuni kwa muda sasa lakini ndugu zangu wananieleza Tanzania kuna mgao wa umeme sasa hivi wakati huohuo serikali ya CCM imesaidi mkataba wa IPTL na Richmond ya mabilioni ya shilingi na pesa imeishia kwa viongozi wachache na hizo kampuni feki huku Watanzania wa kawaida wakibaki na mgao!. Card za luku unalipia kabla ya kupata huduma (pre-paid) sasa ni kwa nini kuna mgao wakati Tanesco imechukuwa pesa kabla ya kutoa umeme halafu hawakupi umeme kwasababu ya mgao. Hii ipo Tanzania tu!!!
Elimu:
Viongozi wengi wa Tanzania wamesomeshwa bure wakati wa Nyerere, ingawa nyerere alikopa sana kuendeleza elimu lakini ni watu wengi walisomeshwa na elimu ya kiwango cha juu sana. Sasa kuna matabaka ya elimu, kwa ujumla elimu imeshuka Tanzania. Kwa watu wa vijijini hawana walimu kwa sababu walimu ni wachache na hakuna kitu chochote cha kuhamasisha vijana kwenda kufundisha vijijini barabara mbovu, mishahara duni, hadhi ya shule nyingi ni ya chini na Watanzania wengi hasa wadogo wamepoteza uzalendo hivyo ni vigumu kupata walimu. Kwa wale walio mijini hata kama ni shule za serikali wanafunzi wanasoma kwa tution tu, hii inamaana wanaenda shule kama ushahidi lakini shule ya ukweli Tanzania kwa vijana wa mijini ni tution. Vilevile kuna shule za masister au za makanisa ambazo ni za wachache wenye vipaji na shule hizi zina ubaguzi wa hali ya juu. Mimi ni mkatoliki lakini najua kabisa kwa utundu niliokuwanao udogoni nisingekubaliwa kwenye hizi shule kwasababu wanachagua wanafuzi wachache wasio na utundu na wenye uwezo. Ingawa nimetokea familia yenye uwezo ningeishia kufukuzwa na hili mimi naona ni ubaguzi wa wanafunzi. Shule nyingi za kidini hasa za katoliki zina wanafunzi wachache kwasababu wengi wao wanafukuzwa kabla ya kumaliza shule, hatuwezi kama nchi kutegemea seminari pekee kwa viongozi wetu wa baadaye. Vilevile kuna shule chache za kislaam ambazo ukiacha Agha Khan hazifanyi vizuri na watoto wanafelishwa kila mwaka lakini serikali ina ziacha hizi shule kwasababu inaogopa siasa. Kama shule inafelisha watoto 80% inatakiwa kufungwa kwasababu inaibia wazazi pesa sio bure kusomesha watoto. Kwa ufupi ni kwamba serikali ya CCM haina agenda ya nchi mfano. Wanafunzi wote wa mwaka wa mwisho wa vyuo vikuu ni kwanini wasifundishe kwa miezi sita shule kabla ya kupewa maganda yao kama ilivyokuwa JKT. Hawa ni vijana wanaopewa mikopo ya serikali ambayo inatoka kwa wanachi na wengi wao hawatalipa! ni kwanini tuna tatizo la walimu wakati kuna vyuo vingi tu JKT ilisaidia nini je ni kwanini vijana wetu wasomi wasifundishe wadogo zao!!.
Maji: Ni kwanini watanzania hawana maji safi wakati technology ya maji safi ni ndogo sana! mimi hapa USA kwa miaka zaidi ya kumi sijawahi kusikia hata mtu mmoja kati ya watu milioni 300 amepata kipindupindu au taifodi na tunakunywa maji ya bomba! mimi kwa mfano sikumbuki ni lini nimenunua maji! cha kuongeza hapo kwasababu hakuna mito mingi huku maji mengi tunayotumia ni ya ****** ambayo yamesafishwa hivyo maji uki flash ****** yanaenda kusafishwa na kurudi maji safi kwenye bomba, hatukhitaji hata kuchemsha. Je kuna ugumu gani kutuma wataalamu wa maji waje hapa kuangalia ni jinsigani wenzetu wanaweza hili, hizo pesa za bili za maji zinaenda wapi?.
Barabara:Houston, TX mji wa watu milioni 4.5 una magari milioni mbili na dar mji wa watu milioni karibu 4 una magari laki mbili tu na raisi amesema miaka mitano yanaweza kufika magari laki tatu. Tatizo la foleni si wingi wa magari bali wembamba wa barabara, lakini pamoja na kujua huu ukweli bado serikali ya CCM inajenga barabara nyembamba. Japan rafiki mkubwa wa Tanzania walifanya study na kuwapa free plan ya kujenga barabara za Tanzania lakini barabara zinajengwa kisiasa badala ya kiuchumi. Serikali inakazania wingi wa barabara wakati wamesha elezwa barabara zinatakiwa kupanuliwa na pesa ni ya msaada lakini wanataka kupeana tenda na plan ya lane tatu wanaweka mbili halafu pesa wanakula. Vijijini hakuna barabara kabisa!! je wenzetu waliwezaje kujenga barabara miaka ya 1940 wakati kulikuwa na hali ngumu ya kiuchumi dunia nzima, vita na technology ilikuwa ndogo! Watanzania wengi hawaelewi hapa!!!
Rushwa:Tanzania inarushwa kila mahali kuanzania bandarini mpaka kwenye idara ya vizazi na vifo. Mimi nilienda kwenye msiba wa ndugu yangu na kupata cheti cha kifo niliombwa posho!!. Document za viwanja kila siku unaambiwa vimepotea ili uanze vipimo upya na waweze kupata rushwa tena, TRA wanachelewesha mizigo ya wafanya biashara ili gharama za storage ziwe juu wa waweze kupata posho kwenye mnada wa hivyo vitu.Hivi vitu vyote hapa ni Watanzania wenyewe kwa jasho lao wanafanya kujenga, biashara n.k lakini badala serikali kuwa upande wa msaada hivyo kuhimiza maendeleo serikali yetu iko upande wa rushwa na kuzuia maendeleo. kwa ufupi rushwa kubwa kwenye serikali ya CCM imefanya serikali kuwa kikwazo cha maendeleo ya wananchi badala ya msaada! je tutafika hivi!!. Raisi kwa upande mwingine watu walewale wenye kashfa na rushwa anawaita marafiki je tumuamini nani!!.

nina mifanya kila sehemu lakini nitaishia hapa
Watanzania hawana tatizo la udini, ukabila wala aina yeyote ya ubaguzi Watanzania wengi wamechoshwa na serikali na wanataka maendeleo. CCM badala ya kujaribu kumzuia CHADEMA ni bora mdumishe maendeleo kwani habari kwa miaka ya sasa huwezi kuzizuia mtapoteza muda bure.Dunia inabadilika kwa kasi sana na muda wa siri umepita na hautarudi tena. Je wajukuu wetu tutawaachia nini!

Hii ni ya 2010 Je yapi yamebadilika? Kwenye umeme nilikuwa sawa mapema sana
Pascal Mayalla
 
Back
Top Bottom