CCM Tatizo lenu ni nini?

wiseboy.

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
2,932
4,534
Kila nikijaribu kuwafikiria jinsi mnavyoshinda humu mkibwabwaja nashindwa kabisa kuwaelewa Kwa Sababu zifuatazo.

1. Serikali ipo chini yenu.
2. Wabunge wengi ni wenu.
3. Kwa mujibu wa Twaweza, Serikali inakubalika Kwa 96%.
4. Kwa mujibu wa Gavana wa BOT, uchumi Wa nchi upo vizuri hakuna tatizo.

Baada ya uchaguzi,Rais alipiga marufuku mikutano ya kisiasa na shughuli za kisiasa hadi 2020.Na hakuna aliyevunja hiyo sheria hadi sasa nchi ipo shwari.

Sasa nawauliza ndugu Zangu wana ccm, kisebusebu cha nini kila Siku mnashinda humu mkiitetea serikali inayopendwa na kukubalika?

Kwa nini hicho kisebusebu msituachie siye wapinzani ambao hatuna wabunge wengi, hatupendwi, na hatujashika dola?

Kuna haja gani ya kutetea serikali inayopendwa na kutokwa povu kila Siku?
Kwa ushauri wangu, tuacheni sisi wapinzani ndo tutokwe povu maana ndo kwanza tunatambaa na nyie mnakimbia.

Ukumbukeni huu msemo "Kizuri chajiuza na Kibaya Chajitembeza ".

cc/Lizabon, Mudawote, Barbarosa na wengineo.
 
Hakuna kuongozwa na machizi wa chadema na cdm ndiyo inakufa kama nccr mageuzi ya mrema
 
Back
Top Bottom