CCM Taifa Ikemee Vijana wake, Vinginevyo...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,463
39,929
Kama mtu ambaye nimemuunga mkono Dr. Slaa na kuamini kuwa ni mtu aliyepaswa na anayestahili kupewa nafasi ya kuliongoza taifa nimeshtushwa na kusikitisha na tamko la UVCCM hususan mashambulizi yao ya mtu - ad hominem thidi ya Dr. Slaa. Ninawasihi viongozi wa CCM Taifa kukemea na kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya kundi hilo la viongozi wa vijana.

Kutokuchukua hatua mara moja na kukaa kimya binafsi naamini iwakuwa ni halali kuamini kuwa uongozi wa taifa wa CCM umetoa baraka zake. Which brings me to my observation: it won't be pretty! Yatakapoanza kuporomoshwa matusi na mambo mengine dhidi ya viongozi wa CCM wa kitaifa isije kuoneekana "ni kuvunja heshima, kuchochea, matumizi mabaya ya vyombo vya habari" na upuuzi wa kawaida tuliouzoea.

Maana naamini walichofanya UVCCM kimewapa watu wengine haki ya kuwatukana na kuwasema viongozi wa taifa wa CCM katika masuala yao binafsi. That will be a tragedy.

Ukiniuliza mimi CCM (T) hawana zaidi ya masaa ishirini na nne ya kutoa kauli ya kinidhamu dhidi ya vijana wao.
 
Wakati mwingine huwa ni busara sana kuongea na 'Mfuga Mmbwa' kuliko mtu mstaarabu kuanza kupigiana kelele ovyo na 'Mmbwa' mwenyewe anapokubwekea hovyo.

Mzee Mwanakijiji, asante kwa kulitambua hilo.
 
Mkuu MM umenena ila naamini lile tamko limeandaliwa na kikundi fulani ndani ya UVCCM kwa faida yao binafsi na kuwa DOWANS imetumiwa kama njia ya kupitishia matusi waliyokusudia kwa hao waliotukanwa.
 
hao ni baba na mtoto siku zote tumewazoea,akili zao ni moja hawawezi kukemeana,ila sasa wameanza kugawanyika hili la Dowans litawatesa sana kwa sababu ni jasho la wanyonge,wajichunguze kwanza wasimseme hovyo Dr Slaa sisi hatuna muda wa kuwasema baba zao tuko bize tunajenga taifa
 
Hapana.. kama CCM Taifa hawatachukua hatua yoyote dhidi ya viongozi hawa wa vijana ambao naamini wamevunja maadili ya uongozi wa CCM (I know I know) na vile vile nadhani wamevunja miiko ya uongozi basi ni wazi kuwa tamko lao limepata baraka toka juu. Kama hili ni kweli basi siku zinazokuja zitakuwa ni za aibu sana kwa uongozi wa taifa letu.
 
Mimi nahisi kuna kigogo yuko nyuma yao anawatumia UVCCM kuwatukana Sitta na Mwakyembe, vijana wanaongea maneno bila adabu, eti WANAKITAKA chama cha mapinduzi kutoilipa dowans, wanakitaka chama cha mapinduzi kuipundua bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu......
 
Wakati mwingine huwa ni busara sana kuongea na 'Mfuga Mmbwa' kuliko mtu mstaarabu kuanza kupigiana kelele ovyo na 'Mmbwa' mwenyewe anapokubwekea hovyo.

Mzee Mwanakijiji, asante kwa kulitambua hilo.

Uwezo Tunao, tatizo ni kuwa Mwenye Mbwa (CCM) na Mbwa (UVCCM) wote ni sawa, mwenye mbwa anaona ni sawa mbwa wake akibweka au asipobweka
 
Mimi nahisi kuna kigogo yuko nyuma yao anawatumia UVCCM kuwatukana Sitta na Mwakyembe, vijana wanaongea maneno bila adabu, eti WANAKITAKA chama cha mapinduzi kutoilipa dowans, wanakitaka chama cha mapinduzi kuipundua bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu......

Of koz behind the thick brains za hawa UVCCM yupo mtu ambaye ana remote control, vijana gani wanaongea maneno ya kipuuzi na kuporomosha matusi na kashfa kubwa
 
Nimeongea kule kwenye tamko kuwa kuna mwanaume nyuma ya hawa vijana, na wanatumika!...Tamko lao lingekuwa na nguvu kama wasingechanganya na matusi ya aibu kwa Dr.
Wanaanzisha moto hawa, ambao naamini hawataweza kuzima!
 
Yaani ni bora kama wangeongelea ishu zao tu sasa kuanza kumchafua Slaa kwa matusi hapo ndipo wamekosea na wamewasha moto ambao naamini kinachokuja nyuma yao huko au kitachokuja kusemwa mbele na huyu waliyemtusi wasubiri
 
I'm very serious; kuna msemo wa kiingereza kuwa "all is fair in love and war".. na UVCCM wamethibitisha hilo. Tatizo ni kuwa kikaango kitakapogeuzwa kwa upande mwingine patakuwa pachungu kweli.
 
Hao vijana ni walevi-hawana lolote,wanajaza kavarej za magazet,then hao wana interest zao,kuropokaropoka il 2015 waje kugombe,Nnape c huyo.
 
Hao ndio vijana wa ccm ambao wameelimika tayari kushika hatamu za uongozi wa taifa,
Inatisha sana, Kama hawatakemewa basi mlango wa matusi kwa viongozi wa ccm utakuwa umefunguliwa.
 
Because hypocrisy stinks in the nostrils one is likely to rate it as a more powerful agent for destruction than it is.

Hicho ndicho wanachofanya UVCCM.
 
nimeshangazwa sana na matusi kwa Dr.Slaa hivi hakukuwa na mtu mwenye akiri nzuri hata mmoja ambaye angewashauri wasiandike upuuzi wao. uvccm ndiyo tamko hilo? mi nadhani anayestahili kwenda milembe kupima akiri ni JK na hilo halina ubishi, na watu makini wote wanajua kuwa ubongo wa JK una matatizo. uvccm wamenivunja nguvu sana mi nilidhani angalau wao ndio lingekuwa kimbilio letu. kweli ccm imeoza juu mpaka chini.
 
Katika hali ya kawaida lazima viongozi wa juu wa CCM lazima waliliona na kulibariki hilo Tamko kabla halijatoka (TISS). Labda kama watagundua madhara yake sasa baada ya kulitoa
 
Kama mtu ambaye nimemuunga mkono Dr. Slaa na kuamini kuwa ni mtu aliyepaswa na anayestahili kupewa nafasi ya kuliongoza taifa nimeshtushwa na kusikitisha na tamko la UVCCM hususan mashambulizi yao ya mtu - ad hominem thidi ya Dr. Slaa. Ninawasihi viongozi wa CCM Taifa kukemea na kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya kundi hilo la viongozi wa vijana.

Kutokuchukua hatua mara moja na kukaa kimya binafsi naamini iwakuwa ni halali kuamini kuwa uongozi wa taifa wa CCM umetoa baraka zake. Which brings me to my observation: it won't be pretty! Yatakapoanza kuporomoshwa matusi na mambo mengine dhidi ya viongozi wa CCM wa kitaifa isije kuoneekana "ni kuvunja heshima, kuchochea, matumizi mabaya ya vyombo vya habari" na upuuzi wa kawaida tuliouzoea.

Maana naamini walichofanya UVCCM kimewapa watu wengine haki ya kuwatukana na kuwasema viongozi wa taifa wa CCM katika masuala yao binafsi. That will be a tragedy.

Ukiniuliza mimi CCM (T) hawana zaidi ya masaa ishirini na nne ya kutoa kauli ya kinidhamu dhidi ya vijana wao.

ad hominem

Ahsante kwa msamiati Mzee Mwanakijiji

(hao mavuvuzela wa uvccm wanafikiri wao ndo vijana pekee katika nchi hii. hawana hata habari kuwa upande wa pili kuna vijana wengi kuliko wao. tunatafuta wa kulianzisha tu, ama wao ama sisi.)
 
Mimi ninahisi kwa tamko hili la UVCCM kuna mambo mawili tata hapa. Moja yawezekana hawa vijana wameandaliwa na chama kutoa tamko hili, ili kuonyesha Umma kuwa hata wao baadhi ya wana CCM hawaridhishwi na mambo ya DOWANS, kwa maaana ya kwamba, ilegeze nguvu ya Umma kuwa kuna wanaounga mkono kutolipwa kwa Dowans ili wananchi walegeze nguvu ya malalamiko, eti wanaungwa mkono na baadhiya wafuasi wa chama tawala.

la pili yawezekana hawa vijana wamepewa baraka za juu na viongozi wa juu ili kufifilisha/kuzima matamko ya akina Sita na Mwakembe, na ndio maana wakatoa maneno ya nguvu vile, haiwezekani tamko liandaliwe wakuu wa chama wasiwe na nakala!!!
Hapana ni kamchezo tu kamechezwa, vijana wametumwa kutuliza umma, nao waonekane wako pamoja na wala hoi.
 
Walichofanya UVCCM ni muendelezo wa mafisadi katika kuhakikisha wanafanikisha malengo yao
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom