CCM:Tahadhari!!!

Chama changu cha Mapinduzi, sasa umefikia wakati sina nguvu ya kukutetea.
Matukio yanayoendelea sasa hivi ni kama mchezo wa kuigiza.
Nilikutetea sana na dhana ya kuvua gamba, kwa kifua mbele.
Nilikutetea sana kwa suala la posho, ingawaje kwa shingo upande
Hili la kuwatetea tena na tena kundi la RA,AC na EL linaanza kuniondolea uzalendo.
Mbaya zaidi ni la kutomchukulia hatua Chenge na rushwa ya RADA.
Kwa kifupi CCM sikuelewi.

Mkuu Lole Gwakisa,

CCM lazima iwatetee hao mnaowaita mafisadi. Aliyepata mgawo wa change ya Rada hakuwa Chenge peke yake, bali ni pamoja na viongozi wengine ndani ya serikali na uchunguzi wa kina ukifanyika mtamkuta na Mkapa naye anahusika na ndio maana akina Chenge wanatamba kwamba wao ni wasafi. Mkapa alitetea "dili" ya rada mpaka povu linamtoka na akawaambia nchi wahisani kwamba hawawezi kutupangia tununue nini maana Tanzania ni nchi huru. Ni dili hili hili la rada ndiyo lililosababisha Bi Clare Short ajiuzulu uwaziri wa serikali ya Blair. Kama mlitegemea kwamba Chenge atashughulikiwa, hiyo ni ndoto. Tatizo la CCM kukumbatia ufisadi lilianzia kwa Mkapa, ni kwenye utawala wa Mkapa ndipo tuliposhuhudia mikataba mibovu ya kifisadi iliyopindukia na wote waliofanya ufisadi huo mpaka leo bado wanatanua mitaani na hakuna atakayekuja kufungwa, zitapelekwa kesi mahakamani lakini mwisho wa siku watuhumiwa wataachiwa.

Lowassa anasemwa kwa sababu ya Richmond, lakini Dr. Mwakyembe anasema kuna mambo hawakuyaweka kwenye ripoti ili kulinda heshima ya serikali, maana yangewekwa ingekuwa aibu kubwa. Sasa ni aibu ipi iliyokuwa inalindwa? Je, walikuwa wanaficha ushiriki wa JK kwenye hilo sakata? Hayo ya kuficha baadhi ya mambo aliyasema Bungeni na zilipoanza chokochoko upya, alisema warudishe ripoti Bungeni ili atapike kila kitu. Wenye kuona mbali walimlaumu Mwakyembe kwamba kwanini alificha baadhi ya mambo na hilo lilipunguza credibility ya hiyo ripoti kwa kiasi fulani na matokeo yake maazimio ya Bunge hakuna yaliyotekelezwa kikamilifu, maana Dr. Mwakapugi na Bwana Mwanyika walistaafu kazi na kupewa haki zao zote. Dr. Hoseah na Bashir Mrindoko mpaka leo bado wako kazini, Mrindoko juzi kaongezwa sembe. Kwa hiyo ukichunguza hilo sakata kwa undani lazima JK anahusika mahali fulani.

Rostam anazungumzwa sana kwenye EPA, hususan, KAGODA na pia ndiye aliyewaleta Dowans ambao wameongeza chumvi kwenye kidonda kwa kudai mabilioni. Lakini ni hela hizo hizo za EPA ndizo ambazo baadhi zilitumika kumpigia kampeni JK ili aingie Ikulu na alifanikiwa kuingia Ikulu. Je, leo hii unategemea JK achukue hatua? Hivi uliwahi kusikia wapi Rais anaagiza kwamba mwizi akirudisha fedha basi asipelekwe mahakamani? Halafu Kikwete huyo huyo ndiyo anasema anafuata utawala wa sheria, sheria ipi ya kubembeleza wezi warudishe fedha halafu wanapewa msamaha wa kufungwa?

Mkapa alijigawia Kiwira, mpaka leo CCM na serikali imefanya nini? Pinda alisimama Bungeni kumtetea Mkapa kwamba watarudisha mgodi wa makaa ya mawe, na mpaka leo jamaa anadunda tu mtaani.

Ni wishful thinking kuamini kwamba CCM ilidhamiria kujivua gamba. Gamba la kwanza linalotakiwa kuvuliwa ni Mkapa kwanza, then Kikwete ambaye urais wake ameupata kwa kutumia fedha za kifisadi. Kama mtaweza kuwavua hao wawili, basi itakuwa rahisi sana kukisafisha chama chenu. Kikwete hana jeuri ya kuwashughulikia AC, RA na EL. Mfano mzuri ni kesi ya Prof Mahalu, hujiulizi kwanini Mkapa kajitosa kwenda kumtetea kwa hati ya kiapo?

Akina Pinda wamebaki kutudanganya kila siku kwamba Meremeta ni swala la Usalama wa Taifa, hata KAGODA nayo Meghji alidanganywa hivyo hivyo kwamba fedha zilitumiwa na usalama wa Taifa. DPP na Mheshimiwa Chikawe wanasema hawana ushahidi wa kuwatia hatiani watuhumiwa wa Rada na KAGODA. Rais wa nchi anamtetea Mramba kwamba kesi yake ni ndogo na kwamba atashinda, so kama atashinda kwanini alipelekwa mahakamani? Ina maana alipelekwa kwa ajili ya usanii?

Hoja ya CCM kujivua gamba ni usanii uliolenga kuwahadaa wananchi (watanzania tulishaonekana ni wajinga kwamba tunaweza kudanganyika kirahisi na slogan za mbwembwe). Maisha Bora kwa kila Mtanzania, mpaka leo hii watu wanalala gizani, watoto wanasoma chini ya miti, hakuna vyoo vya kujisaidia, hakuna madawati na hakuna walimu. Lakini mabilioni yanateketea. Ukiona BAE wanasema change watapitishia kwenye NGO maana yake ni kwamba hawana imani na serikali, maana BAE wanajua viongozi wa serikali ndio waliohongwa mpaka wakakubali hiyo dili ya rada, halafu leo hii unarudisha change kwa serikali hiyo hiyo ili zikafisadiwe tena au ipewe kampuni nyingine tenda hewa. Ujinga mtupu!

Mkuu wangu Lole Gwakisa, pole sana kwa kukata tamaa, lakini hicho ndiyo chama chenu na ndiyo kilichotufikisha hapa tulipo leo hii. Serikali imewekwa mifukoni mwa mafisadi na ndio maana Pinda alisema mafisadi wana nguvu sana, inabidi kwenda nao taratibu. IGP Mwema alisema mafisadi wakishikwa nchi itatikisika. DPP anasema hana ushahidi wa kuwapeleka mahakamani mafisadi. CCM ambacho ni chama tawala kinasema kinajivua gamba, lakini wakati huo huo kinasema hakina ushahidi wa tuhuma ambazo makada wake wanatuhumiwa na kuandikwa sana magazetini. Kaazi kweli kweli!
 
Mkuu Keil.
Umenena mambo mazito ambayo msingi wa yote ni uovu wa viongozi wetu.
Viongozi inabidi watuombe radhi wanachama kwa uongo na wizi mkubwa wa rasilmali za Taifa kwa manufaa binafsi na tamaa ya madaraka.
Wananchi wa Tanzania ni waelewa ,lakini kama mmoja wa viongozi wakongwe wa Tanzania alivyosema, "kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe".
Sakata la kukosa maendeleo na migongano kati ya viongozi kwa leo ni mzigo tosha kwa umma wa kiTanzania.
Sasa imetosha.
Viongozi ni lazima waanze kubebeshana mizigo wanayostahili ili kurudisha imani kwa chama na nchi.
Ni kichekesho kwa serikali yetu kufikiri waTanzania tutaunga mkono kurudishwa kwa chenji ya BAE wakati hata wezi wenyewe hawajachukuliw hatua.
Kwa serikali kuaminika nchi za nje inabidi iaminike kwanza hapa nchini kwa wananchi wake.
Siku ikifika wananchi tutajiuliza hivi hiki chama chetu CCM kinamuwakilisha nani hasa kwa mazangira ya leo?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom