CCM Songea na chaguzi za kishirikiana

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
images
images
images

Ruvuma katika kata ya Mletele Manispaa ya Songea, nako wafuasi wa vyama hivyo walichapana kwa mapanga na fimbo na kusababisha zaidi ya watu watano kujeruhiwa wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo.


Tukio hilo ambalo lilitokea juzi saa tisa jioni huko katika kijiji cha Lihumbu, wafuasi wa CHADEMA akiwemo mbunge wao wa viti Maalumu, Chiku Abwao, walivamiwa na kupigwa na wafuasi wa CCM ambao wanadaiwa kuwa walikuwa na gari ndogo.


Hata hivyo wafuasi wa CHADEMA walifanikiwa kulikamata gari dogo la wafuasi wa CCM akiwemo Mwenyekiti wa UVCCM wa wilaya hiyo, ambayo ndani yake inadaiwa ilikuwa na mapanga, vipande vya nondo, mundu, fimbo
na bundi akiwa hai.


Mmoja wa wafuasi wa CHADEMA Frank Mgao alisema kuwa baada ya kukamatwa gari hilo, askari ambao waliongozwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo, Nico Mwakasanga, waliwakamata na kuwapeleka kituo kikuu cha polisi cha Songea ambako wanaendelea kuhojiwa.


Mgao alisema kuwa baadhi ya wanachama wenzake na wanachama wa CCM wamejeruhiwa kwa kupigwa na panga sehemu mbalimbali za miili yao na wengine wamelazwa katika Hospitali ya Serikali ya Mkoa wa Ruvuma ambako wanaendelea kupata matibabu zaidi.
 
izi iman ukiziamin sana utakuwa mtumwa wa iman
JAMANI chadema MPAKA WAMEWEKA NGOME RUVUMA, HII SI UTANI KTK UCHAGUZI WA 2015! maana mkoa wa Ruvuma uliongoza hapa TZ kwa kukiabudu chama cha CCM,ingawa pia walikuwa wanaongoza kwa ukosefu wa kazi kwa wananchi wake. Tena hawana hata viwanda, mashirika wala miradi ya ujenzi.

Kumbuka Nyimbo za wangoni za kukufuru hizi: KIla nikienda naenda huku nikilinga, ninaye baba mlezi wa chama! Mwalimu mwenye hekima, siasa safi kootee na uongozi boraaa! Walikuwa hawasemi uchumi mzuri kote nchini bali walikuwa wansema siasa safiii kote na uongozi boraa!

Kama kweli wangoni wamefikia kujua nini maana ya upinzani, kweli Tanznaia tumeiva sana ktk maswala ya kujenga nchi kwa misingi ya kisheria . Hongera ma home boys!!!zikomo kwa mbiliii!!!!
 
Ndugu yangu kwa sasa songea kumechafuka kuna maeneo CCM hawatii mguu nenda mgazini,magagula,kata za mjini songea zote CHADEMA, PERAMIHO ipo matatani hapo madaba fiftfifty 2015 Utaona maajabu usichezee M4C Inawatafuna acha
 
nimesoma Songea kuanzia la kwanza mpaka kidato cha tatu.. sikuwahi kuona kama CCM kama itakuja kuondoka na kuchukiwa pale Songea kweli zama za CCM zimepita sasa
 
CCM bana,zao ni akili ndogo kuongoza akili kubwa,sasa mpaka na bundi tena?

Hili ndilo lililonishangaza mno, mchana kweupe watu licha na mapanga na marugu wanafuga bundi ndani ya gari wanayotumai ili iweje na itafsirike vipi? Laba wamefunzwa hivyo na wahamiaji wayao wa Msumbiji kutoka vijiji vya kule Mputa, aka undendeuleni.
 
Ndugu yangu kwa sasa songea kumechafuka kuna maeneo CCM hawatii mguu nenda mgazini,magagula,kata za mjini songea zote CHADEMA, PERAMIHO ipo matatani hapo madaba fiftfifty 2015 Utaona maajabu usichezee M4C Inawatafuna acha

Tatizo vyama vya upinzani vinahangaikia zaidi mijini, kumbi mtaji wa kijijini ni bomba zaidi.
 
Back
Top Bottom